Jumanne, 12 Novemba 2013

100 WAFARIKI DUNIA KWA KIMBUNGA PUNTLAND,SOMALI

Watu wasiopungua 100 wamefariki dunia baada ya kutokea kimbunga kikali katika eneo lenye Mamlaka ya Ndani la Puntland huko Somalia. Rais wa Puntland Abdirahman Mohamud Farole amesema kuwa, hadi sasa watu 100 wamethibitishwa kupoteza maisha kufuatia tukio hilo la kimbunga.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, mbali na maafa hayo, kimbunga hicho kimesababisha hasara kubwa ya uharibifu wa mali za watu.
Maeneo yaliyoathiriwa zaidi na kimbunga hicho yametajwa kuwa ni miji ya Bandarbeyla na Ely. Mamia ya  nyumba na mifugo imesombwa na maji kufuatia mafuriko yaliyoambatana na kimbunga hicho.
Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Puntland huko Somalia amesema kuwa, wanautaka Umoja wa mataifa na mashirika ya misaada kuisadia Puntland. Habari zaidi zinasema kuwa, kimbunga hicho kilikuwa na kasi ya kilomita 90 kwa saa na kiliambatana na mvua kubwa.

100 wafariki dunia kwa kimbunga Puntland, Somalia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD