Kampuni yetu ya KINASORU EAST AFRICA (T) LTD iliitwa kwa ajili ya
kumshauri mheshimiwa mmoja ambaye alikuwa na wazo la kufuga kuku wa
asili walioboreshwa kama sehemu ya kazi yake ya ziada. Alitaka apate
mwongozo wa kitaalam namna gani anaweza kutengeneza pesa kupitia ufugaji
wa kuku hao.
Kitu cha kwanza tulimuuliza, anashilingi ngapi kama
mtaji alioandaa kwa ajili ya mradi wake. Mheshiwa akasema ana Milioni
50. Tukamwambia tunatambua unapenda sana kufuga lakini kwasababu
umetuita, tunaomba tukushauri. Badala ya kufuga anzisha mradi wa
utotoleshaji wa vifaranga walioboreshwa. Badala ya kufikiria kuuza kuku
chotara kama wa nyama baada ya miezi 3 au 4 au mayai mara baada ya
kuanza kutaga, utakuwa ukiuza vifaranga.
Akauliza kwa hiyo
itabidi nianze kufuga kuku hao kama wazazi ili wanipatie mayai
nitakayotumia kwa ajili ya kuatamisha ili kuzalisha vifaranga hao kisha
niwauze?
Kampuni yetu ikamwambia hapana. Utotoleshaji wa
vifaranga na ufugaji wa kuku wa asili walioboreshwa ni vitu viwili
tofauti. Ni miradi miwili inayojitegemea. Tukamwambia, Ukitaka ufanikiwe
katika mradi wako kwanza shika mradi mmoja ili umudu kuusimamia vyema.
Wapi nitayapata mayai bora yenye mbegu ya kuweza kuendesha mradi huo.
Tukamwambia kampuni yetu ina wafugaji wa kutosha wa kuku wa asili
walioboreshwa ambao tunawaita kama outgrowers. Tunawauzia vifaranga
kisha tunawasaidia kwenye huduma za ugani pale kuku wanapokuwa wanaumwa
au chakula pale wanapokosa pesa. Wafugaji wakituita tunaitika haraka
kutoa msaada wetu wa kila hali na kuku wakianza kutaga wanatuletea mayai
hayo ofisini kwetu na sisi tuwauzia wateja wetu wanaozalisha vifaranga
. Kwa mantiki hiyo tukamwambia mayai kwa ajili ya mradi wake wa
utotoleshaji wa vifaranga kampuni yetu itamuuzia.
Kampuni yetu
inauza tray moja la mayai ya kuku wa asili walioboreshwa kwa shilingi
17,000. Ni mayai ya uhakika yanayotoka kwenye vyanzo salama.
Tukamwelekeza anunue mashine mbili moja hatcher na nyingine ni setter
zenye uwezo wa kuingiza mayai 5500 kwa wiki. Bei za mashine hizo zote
mbili ni shilingi milioni 25.
Kwa kawaida mashine ya kutotolea
vifaranga ina sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni ile sehemu ya
kuatamishia mayai na sehemu hiyo tunaiita setter na sehemu ya pili ni
ile ya kutotoleshea vifaranga tunaiita hatcher. Kuna mashine zingine
Setter na hatcher zote ziko kwenye mashine moja ambapo setter inakuwa
juu na hatcher inakuwa chini na wakati nyingine huwa kwenye mashine 2
tofauti kama tulivyokwisha kubainisha hapo awali.
Uwezo wa
utotoaji wa mashine hizo ni asiliamia 96. Maana yake ni kwamba kama
kila wiki mayai 5500 yatakuwa yanaingizwa katika mashine na mayai yakawa
mazuri kwa maana yametoka kwenye kuku wazazi waliotuzwa vyema, maana
yake ni kuwa katika mayai 5500 yatakayoingizwa katika mashine, mayai
5280 yataanguliwa na kutoa vifaranga.
Kwa sababu wewe unakuwa
mzalishaji, basi utauza kila kifaranga mmoja kwa shilingi 1700 kwa
maagent au wafugaji binafsi wanaokuja shambani kununua au kufuata
vifaranga hao. Na maagent, wao watapanga bei zao ili nao wapate faida.
Wewe mzalishaji umezalisha na kila kifaranga ukakiuza kwa shilingi
1700, kwa vifaranga 5280 maana yake utaingiza tsh 8,976,000/= kwa wiki
na kwa mwezi utakuwa na shilingi 35,904,000. Kama wiki moja mashine
inaingiza mayai 5500, kwa mwezi mzima utahitaji mayai tray 22000 sawa na
tray 733 kila tray ni tsh 17,000/= ukizidisha hapo utapata tsh
12,461,000 kama gharama za ununuzi wa mayai ya mbegu ya kuku asili
walioboreshwa. Mshahara wako kwa mwezi tsh 1,200,000/=, Mshahara wa
hatchery attendant 700,000/=, gharama ya umeme kwa mwezi ni tsh
500,000/=, Maji tsh 150,000/= usafari tsh 400,000/=. Jumla ya gharama
zote kwa mwezi itakuwaa tsh 15,411,000/=. Ukichukua mauzo yote ukatoa
gharama utajikuta unabaki na tsh 20,493,000/= kama faida sawa na tsh
5,123,250 kwa wiki.
Baada ya kumpigia hesabu hizo alikubaliana na
wazo letu na akanunua mashine na kuanza rasmi mradi wake wa
utotoleshaji wa vifaranga.
Sasa hivi anaiona faida ya kuzalisha
vifaranga na sisi tumebaki kama watoaji wa mayai ya kuku wa asili
walioboreshwa kwa ajili ya Biashara yake. Kwa kushika kazi moja
unapunguza maumivu ya kichwa kuwahangaikia kuku mara waumwe mara utagaji
usiwe mzuri kutokana na matunzo na mambo mengine.
NB: Mashine za kutotolea vifaranga zinaitwa Incubators.
Kwa mahitaji ya mayai ya kuku asili walioboreshwe na ushauri wa
miradi ya ufugaji, Biashara, Masoko na Mitaji usisite kuwasiliana nasi
kwa simu namba 0767989713, 0786989713 na 0715989713.
KINASORU EAST AFRICA (T) LTD
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni