Kuku anayetaga mmoja kwa siku anakula
wastani wa gram 123. Kwahiyo kwa mfano ukiwa na kuku 1000 kwa siku
utahitaji kilo 123 ambazo ni karibia sawa na mifuko 2.5 ambapo kila mfuko mmoja ukiwa
na Kilo 50. Na kama utakuwa na kuku 100 watahitaji kilo 12.3 kwa siku.
Wastani kilo moja kwa sasa kwa chakula kile Super ambacho kinauzwa tsh 55,000/=
kwa mfuko ni tsh 1100 kwa kilo moja kwahiyo kwa kuku 1000 ambao wanakula
kilo 123 kwa siku utahitaji sh 135,300 kwa siku. Kwa hiyo ili uweze
kupata faida inatakiwa kuku wako utagaji uanzie 60% ambapo utakuwa na
uwezo wa kutengeneza faida ya kama Tsh 34,700/= kwa siku. Kama utagaji
utakuwa zaidi ya 80% faida itakuwa kubwa zaidi. Bei ya mayai kwa sasa
hivi kwa jumla ni kati ya Tshs 8,500/= na 9000/= kwa tray.
Kuku kukosa
madini ya chuma Calcium huwafanya waanzishe tabia mbaya ya kudonoana wao
kwa wao na mwingine kula mayai yao. Lakini sababu nyingine za kudonoana
ni pamoja na mrundikano wa kuku katika nafasi ndogo ya banda, vilevile
mwanga mkali, upungufu wa madini kama hayo ya chuma,na pia kukosekana
kwa mabox ya kutagia ambako hufanya kuku watage chini na kusababisha
wenzao wawadonee pale wanapotaga.
Nini kifanyike, hakikisha kuku
wanakaa kwa nafasi iliyoshauriwa kitaalam, pia wawekewe bembea
zitakazikuwa zikiwashughulisha na michezi, pia wakati wa mchana wawekewe
mboga mboga za majani mfano mchicha, chinese au majani yoyote
yayopendelewa na kuku hao kuyatumia mfano Lusina nk. Vile vile chakula
kiwe na chokaa pamoja na dcp ya kutosha. Lakini njia zote hizo
zikishindikana basi kuku wakatwe midomo mara moja. Na mdomo tunaokata ni
ule wa juu kwababu ndiyo unaotumkika kwa ajili kudonolea wenzake. Mdomo
wa chini hutumika kwa ajili ya kulia chakula hivyo ukikata yote miwili
utamuathiri katika ulaji wake kitu ambacho kitampa mshituko na kama ni
watakaji watashusha ghafla utagaji wao.
IIli kudhibiti kuku
kudonoana,tunashauri ukataji wa midomo ufanyike wiki 15 umri ambao kuku
wanakuwa bado hawajaanza kutaga lakini ikiwa wataanza kudonoana mapema
zaidi basi itabidi mara moja kuku wakatwe midomo yao bila kuchelewa ili
kuzuia athari ya vifo vitakavyotokana na tabia hiyo.
Kuku
kushindwa kula vizuri sababu kubwa mara nyingi ni Ugonjwa, huenda kuku
wako wanaumwa au kama watakuwa wamebadilishiwa chakula kutoka kile
walichokizoea. Vile vile joto kali linapunguza ulaji wa kuku pia kama
kuna makelele kuku hushituka na kuwafanya wapunguze ulaji wao. Kuku
wakiwa sawa chakula chote wanachowekewa kwa siku kama share yao huwa ni
lazima wakimalize vinginevyo kuna kitu kinakuwa hakijaenda sawasawa na
hivyo lazima ukiwa kama mfugaji ufuatilie ili uweze kujua sababu hasa ya
tatizo hili kama ni Ugonjwa au Vinginevyo.
Idadi ya vyombo vya
maji na chakula inategemea na idadi ya kuku ulionao lakini kwa mfano
ukiwa na kuku 1000 hapo utahitaji drinkers 22 na feeders 43. Hapo kuku
wote watapata nafasi ya kula wanapowekewa chakula. Faida ya kuwa na
vyombo vya chakula vyenye uwiano sawa na kuku huwafanya kuku wako wasiwe
wanapishana katika ukuaji wao na hivyo kama ni kuku wa mayai
itawasaidia wasipishane katika kuanza utagaji wao na kama ni kuku
wanyama itakufanya wewe mfugaji uwauze kwa wakati mmoja kwa kuwa ule
uzito wa kuwauzia yaani market weight watakuwa wamefikia kwa wakati
mmoja.
AMAN NG'OMA
Mshauri wa Miradi ya Ufugaji, Uchumi Kilimo, Biashara na Masoko
0767989713, 0715989713 NA 0786989713
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni