Alhamisi, 28 Aprili 2016

UFUGAJI WA KIBIASHARA


Kwa kawaida incubator inayochukua mayai 5500, full capacity yake ni mayai 16500. Mashine kama hiyo hupaswi kujaza mayai yote kwa kuwa mfumo wa mashine za kutotolea vifaranga unavyotengenezwa si kwa ajili ya kujaza mayai at its full capacity. Kwanini, kwa sababu ukijaza mayai kadiri ya uwezo wa mashine, maana yake ni kuwa utatakiwa ukaa siku 21 za kusubiri mayai uliyoyaingiza katika mashine hiyo hadi yatotolewe.
Na kwa kawaida mayai yanayofaa kutotoleshwa yanapaswa yasizidi siku kumi toka mayai hayo yatagwe lakini inafaa zaidi yawe yaliyotagwa ndani ya siku saba na siku ya nane yaingizwe katika mashine kwa ajili ya kuanza kuatamishwa. Mayai yaliyokusanywa ndani ya siku saba na siku ya nane yakaingizwa katika mashine yanakuwa na ufanisi mkubwa katika kutotolewa. Kwahiyo kama ukisema ujaze mayai mashine yako yote maana yake ni kwamba utapoteza mayai yatakayotagwa kabla ya siku 21 wakati ukisubiri mayai ya mwanzo yaweze kutotolewa.
Kwa msingi huo machine nyingi zimetengezwa katika mfumo ambao, kama uwezo wa mashine ni kuingiza mayai 3186 hatcher yake itaingiza mayai 1062. Hii inakufanya kila wiki uwe unaingiza mayai. Na kama kila wiki utakuwa ukiingiza mayai maana yake kuwa kila wiki utakuwa ukizalisha vifaranga. Mfumo huu hauruhusu kupoteza mayai, mayai yote yatakayokuwa yakitagwa yataingizwa katika mashine.
Mayai ya kuatamishwa hukaa siku 21 toka siku ya kwanza kuatamishwa hadi kupata vifaranga.
Kinasoru East Africa (T) Ltd

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD