Jumatatu, 11 Novemba 2013

IRAN YAUNDA KOMBORA JIPYA LA KUJIHAMI ANGANI


Kombora la Sayyad 2
 Kombora la Sayyad 2

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua uzalishaji wa kombora jipya la kujihami angani lijulikanalo kama Sayyad 2.
Akizungumza Jumamosi, waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Hussein Dehqan amesema kuwa kombora hilo la kisasa lina uwezo mkubwa wa kukabiliana na adui angani. Aidha amesema Iran imefanyia majaribio mfumo wa makombora ya kujihami angani ujulikanao kama Talash wenye uwezo wa kutungua ndege mbali mbali za kivita. Amesema zana hizo za kivita ni muhimu sana katika kukabiliana na hujuma za ndege za kisasa kabisa za kivita ambazo hutumiwa na adui.
Ikumbukwe kuwa mwezi Septemba Brigedia Jenerali Farzad Esmaili Kamanda wa Kitengo cha Jeshi la Iran cha Kujihami Angani cha Khatamul Anbiya (SAW) alisema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kati ya nchi 10 bora duniani katika uga wa utengenezaji zana za kujihami angani. Mafanikio yote ya Iran katika sekta ya ulinzi yametokana na juhudi za wataalamu wa hapa nchini. Iran imejitosheleza katika ujenzi wa zana muhimu za kivita kama vile ndege, makombora, vifaru, rada, manoari n.k. Iran imetoa hakikisho la mara kwa mara kuwa uwezo wake mkubwa wa kijeshi si tishio  kwani sera zake za ulinzi zimejengeka katika msingi wa kujihami.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD