- Rais kikwete azishuku Kenya, Uganda na Rwanda kujimilikisha jumuiya hiyo na kuitenga Tanzania
Rais wa jamhuri ya muungono wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete aonyesha kutolizishwa na uamuzi wa Kenya,Uganda na Rwanda kuitenga Tanzania katika Jumuiya hiyo.
Asema ujenzi wa miundombinu, mambo ya anga nk yote yapo kwenye malengo ya Jumuiya ya Afrika mashariki ashangaa nchi hizo tatu kutekeleza mambo haya peke yao huku wakiitenga Tanzania.
Matitizo yetu yako kwenye himaya ya ushuru wa forodha alisema kikwete.
Pia Rais amesema Tanzania haiko Tayari kujitoa jumuiya ya Afrika ya mashariki,kwa kuwa Tanzania haina makosa.Tanzania ni wavumilivu. Tanzania ni mtekelezaji wa itifaki halali ya jumuiya ya afrika ya mashariki.
Tanzani imetumia mali, nguvu na muda mwingi kwenye Jumuiya ya Afrika mashariki. Kwa mwaka tunachangia bilioni 12 ,iweje tusiwe na uchungu wa jumuiya. Tatizo kubwa alilobaini mheshimiwa Rais Kikwete hata tukafikiwa kutengwa ni pamoja na Ardhi, ajira,uhamiaji nk.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni