Leo
nimeamua kuwakumbusha watu juu ya mambo mengi yanayowekwa kwenye
mitandao nikitaka tuyatafakari pengine ni ya kweli kutokana na uhusiano
wa matukio na kile kinachokuwa kimeandikwa kabla.
Mtu
aliweka jf habari hii ndefu sana na ile ya sakata la mbowe kupanga
mbinu za kumuondoa zitto uongozini na leo yametimia, sasa swali
waliopinga na kusema ilitungwa leo wako wapi, je hli la kujiteka na
kumwagia saed kubenea tindikali tutabisha kwa kiwango gani?
Habari kamili ilkuwa hii hapa chini
SAKATA
LA CHADEMA ‘‘KUJITEKA’’
NA
SAED
KUBENEA KUMWAGIWA TINDIKALI.
Ndugu
Wananchi,
Taifa letu la Tanzania linapitia katika wakati wa
upevukaji wa uhuru wa kusema kwa uwazi, pia Taifa letu linapitia katika
harakati za demokrasia na maozezi ya deomkrasia.
Katika kipindi hiki tumeshuhudia mambo mengi
yakitokea ikiwa ni pamoja na baadhi ya watu na taasisi zao kuutumia uhuru huu
wa kusema vibaya kwa lengo la kutimiza malengo yao binafsi au kutimiza wajibu
wa uhuru wao wa kusema.
Pia tumeshuhudia baadhi ya watanzania wakiitumia
vibaya demokrasia na wengine wakiitumia vizuri kwa manufaa ya umma na wengine
kwa manufaa yao wenyewe.
Baada ya utangulizi huo sasa nianze makala hii kwa
kina na kwa kusema kila kitu ninachokifahamu kuhusu mada hii.
Ndugu
Wananchi,
Mimi nimekuwa mtumishi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) toka 2003 nikiwa mwanachama wa kujitolea na baadae 2004/8 nikiwa
kiongozi wa chama makao makuu,
Mwaka 2006 secretariat ya makao makuu ilipanga
mikakati ya namna ya kukifanya chama kiwe maarufu na namna ya kuwafanya
wananchi wakichukie chama tawala ili watafute mbadala wake ambao tulilenga uwe
ni chadema.
Katika mikakati ile tuliazimia mambo mawili makubwa
yatakayoleta matokeo yote mawili kwa wakati mmoja yaani kukifanya chama kiwe
maarufu na wakati huo huo wanachi wakichukie chama tawala ili wajiunge na
CHADEMA.
Mkakati namba moja ulikuwa kuandaa timu ya red
brigade ya watu wenye weledi wa kijeshi wenye uwezo wa kucheza karete au kong
fou ili tuwaandae wawateke viongozi wa taifa wa chama (CHADEMA),
Mkakati ule uliwalenga wabunge maarufu Dr Slaa na
Zitto Kabwe, lakini pia ulilenga kumteka Mwenyeikiti wa Taifa Mbowe Alkaeli
Freeman. (Lakini haya ya kutekwa viongozi yalipangwa nyuma ya uficho bila dr
slaa kuhusishwa kwa sababu maalum nitaeleza baadae)
Ili kulifanya tukio lile lihusishwe na Chama tawala
tulipanga yatolewe matamko makali dhidi ya serikali na chama tawala kwa lugha
kali itakayosababisha serikali ijibu na ikibidi ijikanganye kutoa kauli ili red
brigade watakapotuteka iwe sababu ya moja kwa moja kuwahusisha.
Katika mkakati ule mbinu na namna ya kuwateka
viongozi hawa uliandaliwa vyema vijana wakiwa chini ya uangalizi wa mlinzi wa
Mbowe aliyetolewa tarime (kwa jina la Chacha suguta) wakipewa mafunzo namna ya
kutokomea baada ya kuwateka viongozi wetu na kuwapora computa na simu zao bila kuwadhuru.
SIKU
YA TUKIO
Tukiwa makao makuu mida ya saa 3 asubuhi tukingojea
muda wa matamko kutolewa na viongozi wa chama, alikuja Marehemu Chacha Wangwe
akiongozana na kijana aliyekuwa mahili sana kwa siasa za tarime Chacha Okong’o
aliyeshinda kura za maoni kugombea Ubunge jimbo la Nyamagana lakini akaondolewa
na wenje akapewa nafasi yake kwa misingi ya Mbowe kuogopa damu ya marehemu
chacha wangwe ingeweza kumrudia mapema sana endapo Okong’o angepata nafasi ya
uongozi.
Marehemu Wangwe alipoingia na kuambia juu ya tamko
lililoandaliwa kutolewa kuisema serikali kuwa imepanga mbinu ya kuwaua Mbowe,
Zitto na Dr Slaa, Marehemu alipinga issue hiyo na kuonya kuwa itaweza kukidhuru
chama chenyewe kama haikupimwa kabla ya kuitoa,
Wangwe akaonya kuwa sio kila umaarufu huwa na tija,
Mbowe aliwakaripia sana Mnyika na Zitto kwa
kumshirikisha Wangwe ambaye yeye alimwita ni mvuta bangi tena akisisitiza kuwa
kama ni bangi wengi tunavuta lakini zake ni za wehu.
Kwa misimamo ya wangwe aliyekuwa mbunge wakati huo
hajawa Makamu Mwenyekiti wa chama taifa, Mbowe alizuia tamko lile, waandishi waliokuwa wamealikwa walipofika
waliambiwa kuwa kikao kilihairishwa.
MIPANGO
YA KUTEKWA YAKAMILIKA.
Mbowe aliwaita vijana wake wa red brigade akiwa na
vijana wake wa mipango Mnyika na Zitto(zitto wakati huo akiwa miongoni mwa
wanaompinga wangwe kwa nguvu zote bila kujua afanyalo akiwa mkono wa kazi wa
Mbowe akiamini kuwa anapambana na wahujumu wa chama kumbe anapambana na
demokrasia) ikumbukwe kuwa Zitto aliamua kujitoa kwa mbowe baada ya mbowe
kushagilia kifo cha wangwe wakiwa musoma wakitoka msibani, wakiwa hotelini
Mbowe alianza kumsema marehemu vibaya akiamini kuwa aliokaa nao wote ni vijana
wake, hapo zitto aliinuka na kusema kwa uchungu sana kuwa sikujua kama
mwenyekiti unaroho mbaya kiasi hiki, alipomaliza hayo aliondoka na ndio ukawa
mwanzo wa mwisho wa uhusiano mzuri wa mbowe na Zitto.
Sasa
tuendelee namipango ya kujiteka,
Mbowe akiwa na Zitto na Mnyika ndani ya ofisi yao makao makuu mitaa ya
ufipa, walipanga mikakati ya kuwaita vijana wao walioandaliwa kufanya utekeji
bila kumtaarifu katibu mkuu wao wakihofia ataogopa na pengine atatoroka, lakini
waliamua kumficha pia ili atakapotekwa na kuporwa computa yake ya mkononi na
simu zake kisha mwenyekiti atamwamuru katibu atoe tamko huku akiamini ni ccm
wametuma watekaji ilia toe tamko lenye lugha kali kwani walijua akipaniki huwa
na hasira na kumwaga maneno mengi ya hovyo kama tunavyomuona akifanya leo.
Ndugu
Wananchi,
Ikiwa ni saa
7 mchana mpango ukiwa umepangwa siku ya jumapili siku waliyoipanga na kuiona ni
siku muafaka ya kutekwa, mwenyekiti alimwambia Dr slaa kuwa siku hiyo usiku
watakuwa na kikao pale ofsini kwao makao makuu Ufipa kuanzia saa 4 usiku
akamuomba ajiandae tu lakini ajenda atakuja nazo yeye, dr slaa alikubali bila
kujua kuna nini nyuma ya pazia,
Baadaye Mbowe alimwagiza Mnyika kuwataarifu watekaji
kuwa wajiweke tayari,
Mnyika alitekeleza agizo hilo lakini kama kawaida
yake alitoa uzuru wa kutokuwepo kwenye tukio kwa kusingizia jukumu la
kifamilia,
Ikumbukwe hii imekua tabia yake kwa mlolongo
ufuatao;-
Wakati kambi ya upinzani bungeni iliazimia kuondoka
bungeni kupinga kumtambua Rais Kikwete, Mnyika yeye aliomba ruksa kuwa anaumwa
na hakuingia bungeni kwa uoga wake na kwa kumuonea aibu kikwete kwani kikwete
alimchangia Mnyika Tsh 5,500,000/= wakati wa kampeni kwa sababu ya kutompenda
hawa ng’umbi ambaye aliingia kwa nguvu za lowassa na ndio maana jk alimteua
Nape kuwa mkuu wa wilaya masasi wakati wa kampeni,
Kikao cha kumshughulikia Zitto kilichokaliwa kwa
Mbowe kilipoiva Mnyika aliomba ruksa na kuondoka,
Kadhalika na kwenye mpango ule wa kutekwa Mnyika
alifanya hivyo (alidanganya kuwa mjomba wake ametoka Botswana na hakuna mtu wa
kumpokea bali yeye anategemewakumpokea)
Zitto na Mbowe waliwasili makao makuu wakamkuta Dr
Slaa amekaeti akiwangojea,
Mkakati ulikuwa watekwe wote ikibidi wapigwe japo
sio kwa kiwango kikubwa cha kuumizwa, wakati wakizugazuga kuisubiri saa6 usiku
ifike Zitto alipigiwa simu na mkuu wa kikosi cha watekaji na kuomba pesa za
mafuta kwa kuwa gari lao moja limebuma, wakati huo hakukuwa na M-Pesa wala kitu
kama hicho,
Mbowe alitoa tsh 200,000/= zitto akapewa apelike msasani
walipokuwa, zitto alifikisha pesa kasha akaacha maagizo kuwa wasubiri
atakapofika makao makuu atawapa alerting sign.
Zitto alifika makao makuu akamkuta mbowe
anajadiliana na Dr slaa kama viongozi wakipanga ajenda za vikao,
Zitto akampa alama ya dole kuonyesha amekamilisha
kazi huko huku Dr slaa haju lolote,
Baada ya dakika kadhaa mbowe aliaga kuwa anaenda
kutoa pesa kwenye ATM mitaa ya mwanamboka manyanya,
Lakini muda anaaga zilikuwa zimebaki dakika chache
sana kabla ya kutimu saa6 muda muafaka kwa kutekwa walikojiandalia,
Mbowe aliondoka na derva wake akiwaacha wajumbe
wamekaa ndani ya makao makuu ili hali mpango huu ukiwa unajulikana kwa zitto,
mbowe na mimi tu, wajumbe wengine hawakujua kitu, sisi tulijiandaa kisaikolojia
lakini nilishangaa kuwaona akina Mnyika na Mbowe wanaanza kutoroka, nikajiuliza
je walitoa maagizo kuwa tuuwawe au walitoa maagizo kuwa tuumizwe?
Nikamvuta Zitto kando nikamng’ata sikio juu ya jambo
hili nay eye akashituka, wakati huo wale maghaidi feki walikuwa wakipiga simu
kutaka kupata ruksa ya wao kuvamia,
Zitto akampigia Mbowe lakini Mbowe hakupokea simu,
bali akatuma sms kuwa waambie hao makamanda waje mie nitafika kabla hawajafika,
Nilimkataza Zitto asiwape ruksa hao maghaidi feki
kwani yawezekana kuna mchezo umetegwa bila sisi kujua na tunaweza kudhurika
kasha tukajuta nae akanisikiliza tukaazimia tumngojee Mbowe arudi kwanza,
Tulingojea kwa muda wa saa nzima mpaka saa 6:40 bila
mbowe kufika toka umbali wa kilomita moja ambayo kwa miguu ungeweza kutumia
dakika 20 tu,
Mimi niliamua kuondoka kasha zitto nae akanitxt kuwa
ameondoka,
Ilipofika saa 8 usiku mbowe alipiga simu kwangu na
kuniuliza kama tuko salama au la!!
Nikamjibu wewe uko wapi mwenyekiti wangu?
Akajibu nilipata mgonjwa ghafla nikampeleka hosp.
Ikumbukwe kuwa mbowe ana tabia ya kuanzisha zogo
kasha kuwaachia iwatafune.
Mtakumbuka Mbowe alipowadanganya vijana na Dr slaa
wakeshe wakiota moto kuitaka serikali imwachie Lema huko Arusha, lakini Mbowe
alitoroka baada ya kuona zogo linawaka moto mkali akamwacha Dr Slaa akakamatwa
peke yake na wapambe wao.
Tuendelee
na sakata la kutekwa
Usiku ule tulimwacha dr slaa alikesha mpaka saa tisa
usiku hakuna aliyepokea simu yake tena na hata anaposoma makala hii atakumbuka
vizuri sana usiku ule!
Siku iliyofuata kila mmoja alikuja na sababu zake za
uongo ili mradi wajumbe waliokuwa wakisubiri kikao ambao wote walikuwa
watumishi wa makao makuu waamini.
Hakuna anaejua wale maghaidi feki waliishia wapi!
KWA
HIYO MSIONE VYAELEA MJUE TU VIMEUNDWA
SAKATA LA SAED KUBENEA KUMWAGIWA TINDIKA
Ndugu
Wananchi,
Baada ya mkakati wa kujiteka kukwama Mbowe hakukata
tama, aliandaa timu mpya ya kazi ya kukifanya chadema kuhurumiwa na kukifanya
ccm kuchukiwa,
Mbowe alimpa Mnyika jukumu mpa la kuandaa vijana
wenye uwezo wa kuteka kiukweli na sio waigizaji tena, wenye uwezo wa kuteka
kudhuru na hata kuua,
Mnyika kama alivyotajwa na gazeti Fulani kuwa ni
mwanachama mtiifu wa Mbowe alitimiza agizo hilo haraka na kukabidhi hadidu za
rejea kwa Mbowe,
Timu yake ya utekaji iliundwa na watu wafutao:-
1. Sabra aliyepewa jina la kazi kama VX (i) (mlinzi wa
makao makuu chadema) badae akapewa kuwa mkurugenzi wa ulinzi, huyu bwana
aliwahi kutumikia jeshi la magereza na sasa ni msaidizi wa bwana Rwakatare,
2. Deus
mallya au Deus Aman VX(ii) huyu atakumbukwa kwa tukio la Chacha Wangwe na
inaweza kuwa ushahidi wa kifo cha utata cha marehemu Wangwe.
3. Henry
Kilewo VX (iii) huyu atakumbukwa kwa tukio la kutekwa kwa kijana wa Igunga na
kumwagiwa tindikali
4. Kasha
walikuwepo wasaidizi wao walioitwa ‘WATINDI’ ikimaanisha wabeba tindikali
Kikosi kazi hiki kilofanya
organization kwa umakini sana na kilifanikiwa vyema kabla ya mmoja wao kutoboa
siri kwa wahusika waliodhurika.
Siku ya tukio kulizuka mabishano
kati ya Mnyika na Deus Mallya kuhusu malipo yaliyokuwa yamebaki.
Mnyika alipewa majina ya vijana wao
‘watindi’ ili awalipe pesa ya awali yaani advance,
Aliwalipa kila mmoja Tsh 300,000/=
na baki yao iliwa Tsh 200,000/= kila mmoja,
Wakubwa wao yaani akina sabra na
deus walilipwa Tsh 700,000/= kama advance na baki lao likiwa 300,000/= kila
mmoja.
Wakati huo mbowe na mkurugenzi wa
pesa makao makuu ya chama bwana Antony Komu (mmiliki wa gazeti la MwanaHalisi)
walikuwa katika mahusiano mazuri kabisa yasiyo na migogoro,
Mbowe alikuwa tayari kashawapa
target ya kupiga ili wananchi wapate hasira na kuichukia serikali ya chama cha
mapinduzi ili pia iwe namna ya wao kutafuta njia mbadala ya kisiasa ambayo
aliamini ni chadema,
Vijana walipanga mipango na
kufanikiwa kumwagia saed kubenea tindikali waliyoipata toka kwa mbowe mwenyewe
na akijua alipoipata mwenyewe.
Baada ya mpango ule kufanikiwa na
Saed Kubenea kupata nafuu, chama hakikupata mrejesho ambao mbowe aliutarajia,
badala yake waandishi wa habari waliiteka ile issue na kuwa ajenda ya jukwaa la
wanahabari na sio la chadema kama ilivokuwa imetegemewa.
GHAIDI
MMOJA AJILIPUA KWA ANTONY KOMU
Wakati issue ikishika kasi mmoja wa
wale maghaidi aliyekuwa amepunjwa pesa zake na kiongozi wao aliamua kumatafuta
Sabra mguu kwa mguu,
Sabra hakuwa na majibu yenye adabu
badala yake alikuwa akimtolea vitisho vingi vya kutishia maisha yake,
Bila hiyana kijana aliamua
kujilipua akamfuata Kubenea na kumpa mkanda wote ulivyokuwa na akampa ushahidi
wa sms na hata akajaribu kumtumia sms Sabra ili kubenea aone itajibiwaje,
Kubenea alipigwa na butwaa baada ya
sabra kujibu kuwa ‘hata ukienda polisi wewe ndiye utashughulikiwa kwa kushiriki njama za
kumwagia mtu sumu sisi tutakanusha na tena hujui mbowe ni nani wewe cheza
utapotea’
Kubenea aliamua kumshirikisha boss
wake yaani Komu,
Komu alimtafuta Mbowe kwa jazba
sana na kumuomba wakutane kuna jambo la hatari kamfanyia,
Mbowe alikubali wito wa Komu kwa
hofu kubwa kwani alijua deal limesanuka,
Alimfuata nyumbani kwake Tegeta
alipowakuta wapo wote kubenea na komu pamoja na kijana Yule,
Baada ya kupewa mkanda mzima mbowe
aliinuka na kutoa Tsh 300,000/= na kumpa Yule kijana na kumuomba wawasiliane
ili ampe kazi ya kufanya na sasa kijana huyu ni baunsa wa billcanas club pale
anaitwa SWAI.
Mbowe aliamua kumuomba radhi Komu
na kujieleza ajuavyo mwenyewe lakini wakawekeana yamini ya kwamba Mbowe
atachangia uchapishaji wa MwanaHalisi matoleo 10 na kumpangishia kubenea Nyumba
nzima yenye mkataba wa miaka miwili.
Wengi huwa wanajiuliza kwanini
kubenea anashindwa kuwabaini waliomteka na kummwagia tindikali mpaka leo?
Majibu ni hayo.
MBOWE SIO BINADAMU WA KAWAIDA
KABISA,
HATA MIE NAOGOPA KUWEKA HADHARANI
JINA LANGU KWA SABABU NAJUA NAWEZA KUFA WAKATI WOWOTE KWA MANUFAA YAKE
Kwa hisani ya Bongo Africa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni