Jumamosi, 21 Desemba 2013

LAITI TUNGEMSIKILIZA SHEIKH PONDA MAWAZIRI WASINGEJIUZURI


ALLAH WALAU AMEANZA KUTOA MAJIBU YA MAOMBI YA WAISLAMU, YALEYALE ALIYOWAHI KUYASEMA MWANAHARAKATI ANAYEPIGANIA HAKI ZA WAISLAMU NCHINI SHEIKH PONDA ISSA PONDA KUHUSU DHULMA NA MAUAJI YANAYOFANYWA NA POLISI WA TANZANIA, YAMESEMWA JUZI NA WABUNGE HADHARANI.

SIO TU KWAMBA HAWAKUKAMATWA AMA KUTWANGWA RISASI ZA BEGA!, BALI MANENO HAYO AMBAYO HAYANA TOFAUTI NA YANAYOSEMWA NA WAISLAMU YAMEFANYA MAWAZIRI WANNE KUFUKUZWA KAZI.

SASA KOSA LA SHEIKH PONDA LIKO WAPI ANAPODAIWA KUWA ALISEMA POLISI WAMEUA WANANCHI WASIO NA HATIA KULE MTWARA PAMOJA NA KUBAKA ILIHALI RIPOTI YA KAMATI YA JAMES LEMBELI IMEKIRI KIASI CHA KUWALAZIMISHA KINA NCHIMBI, NA VUAI NAHODHA KUFUKUZWA KAZI?

NAJUA SHAURI LA SHEIKH PONDA LIKO MAHAKAMANI, LAKINI MADHAMANA NI LAZIMA MUJUWE KUWA LEO MNAWAONEA NA KUWANYANYASA VIONGOZI WA WAISLAMU KWA KUWAWEKA NDANI BILA KUWAPATIA DHAMANA, KESHO ALLAH ATAWAHUKUMU TU!!

HATA MKIONA INACHELEWA MUJUE IPO SIKU, KWANI DK EMMANUEL NCHIMBI ALIJUA KUWA ATAONDOKA KATIKA OFISI ILE? TENA KWA KUFUKUZWA?

BILA SHAKA SASA WASUBIRI KUPANDISHWA MAHAKAMANI, DUA YA MWENYE KUDHULUMIWA HAIJAPATAPO KUREJESHWA NYUMA TOKEA DUNIA HII ILIPOUMBWA!!
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD