Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya
Mrisho Kikwete kwenye ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
jijini New York, Marekani 24/12/2013.
Bwana
Ban Ki Moon alimwalika Rais Kikwete ambapo viongozi hao wawili
walijadili masuala mbalimbali ya kimataifa hususan masuala ya amani na
ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika kudumisha amani sehemu mbalimbali
Afrika na katika nchi nyingine duniani. Tanzania ina majeshi ya kulinda
amani katika nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Darfur nchini Sudan na Lebanon.
Rais
Kikwete yupo jijini New York nchini Marekani ambapo anaendelea vyema na
ukaguzi wa kawaida wa afya yake.(picha na Freddy Maro)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwaajili ya kufanya mazungumzo nae.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Mazungumzo na Mwenyeji wake,Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon alipomtembelea ofisi kwake jijini
New York, Marekani 24/12/2013
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyeji wake,Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa,Ban Ki Moon mara baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini New
York, Marekani 24/12/2013.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni