Mwenyekiti wa Cuf Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba akihutubia wananchama na wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa hadhala uliopewa jina la mchakamchaka mpaka 2015 ambao ulifanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Katibu mkuu wa Cuf, Maalim Seif Hamad
akihutubia wananchama na wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa
hadhala wa mchakamchaka mpaka 2015 uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya
msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
Mwenyekiti wa Cuf Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba kushoto,
Katibu mkuu wa Cuf, Maalim Seif Hamad na Mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi kulia wakifuatilia matukio kabla ya viongozi wakuu wa chama hicho kuhutubia wananchi.
Katibu mkuu wa Cuf, Maalim Seif Hamad na Mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi kulia wakifuatilia matukio kabla ya viongozi wakuu wa chama hicho kuhutubia wananchi.
Wafuasi na wanachama wa Cuf wakiwa
wamekunja ngumi juu wakati viongozi wakuu wa chama hicho wakihutumia
maelefu ya wakazi wa Morogoro.
Mwenyekiti wa Cuf Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba akisalimia wananchama na wafuasi wa chama hicho mara baada ya kuwasilia katika ofisi za wilaya za chama hicho mkoani hapa.
Wananchama
na wafuasi wa chama hicho wakiwa katika maamandano kutoka katika ofisi
za chama hicho mtaa wa Boma kuelekea uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege katika mkutano wa hadhala.
Sehemu ya magari kutoka Dar es Salaam
ambayo yamebeba wanancha na wafuasi wa chama hicho yakielekea katika
uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege.
Wanachama wa Cuf wakiwa katika
maandamano huku Mwenyekiti wa Cuf Taifa Profesa Ibrahim Lipumba akiwa
katika gari huku akiwapungia wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakati
akielekea katika ofisi za wilaya hiyo mtaa wa Boma.
Mmoja wa wasanii akitumbuiza kabla ya viongozi kuhutubia.
KWA UFUPI.
Awali kabla ya kufanyika kwa mkutano huo uliopambwa
na shamra shamra za ngoma zilizoanza siku mbili kabla ya uzinduzi huo
zikiambatana na baadhi ya wafuasi na wapenzi wa chama hicho kupita
katika mitaa mbalimbali ya mji wa Morogoro wakiperusha bendera,
uliingia dosari baada ya kutanguliwa na mvua kubwa iliyokwamisha baadhi
ya shughuli na kuchelewa kuanza kwa mkutano huo.
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemnadi Mwenyekiti wa chama hicho,
Profesa Ibrahim Lipumba kugombea kwa mara nyingine kiti cha urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015,
huku yeye binafsi akitangaza neema kwa Watanzania ya kuwajaza fedha
mifukoni.
Katika mkutano wa uzinduzi wa operesheni ya
mchakamchaka kuelekea mwaka 2015 uliofanyika juzi katika Viwanja vya
Shule ya Msingi Kiwanga cha Ndege Morogoro, viongozi wengi wa chama
hicho akiwamo Katibu Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, walimnadi Prof Lipumba
jukwaani wakidai kuwa bado ni kiongozi anayestahili kugombea wadhifa
huo kupitia CUF.
Awali kabla ya kufanyika kwa mkutano huo
uliopambwa na shamra shamra za ngoma zilizoanza siku mbili kabla ya
uzinduzi huo zikiambatana na baadhi ya wafuasi na wapenzi wa chama hicho
kupita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Morogoro wakiperusha bendera,
uliingia dosari baada ya kutanguliwa na mvua kubwa iliyokwamisha baadhi
ya shughuli na kuchelewa kuanza kwa mkutano huo.
Mvua hiyo ilianza kunyesha Saa 9.40 jioni mara
baada ya mabasi madogo takriban 15 yaliyowabeba wanachama, wafuasi na
viongozi wa CUF kutoka Dar es Salaam kuwasili katika viwanja vya
mkutano,hali ambayo iliwalazimu viongozi wa juu kuanza na zoezi la
kufungua matawi ya jumuiya za vijana na jumuiya ya akinamama kabla ya
kwenda kuhutubia.
Akizungumza katika mkutano huo, Profesa Lipumba
alisema utatifi uliofanywa katika baadhi ya nchi duniani zikiwamo nchi
za Brazil na Mexico umebaini kuwa njia nyepesi ya kumuondolea mwananchi
umasikini ni kumpatia fedha taslimu.
Prof Lipumba ambaye ni mtaalamu wa masuala ya
uchumi,alisema kuwa jambo hilo linawezekana kufanyika nchini kwa kutumia
teknolojia ya simu za mikononi na kuwapo kwa vitambulisho vya taifa
vinavyotumia alama za vidole kama alama za ulinzi.
Alisema India yenye watu zaidi ya bilioni 1.2
imefanikiwa kutumia vitambulisho vya taifa katika masuala mbalimbali
ikiwa ni pamoja na uhifadhi na usalama wa fedha zao na hivyo kuwataka
wananchi kujitokeza kwa wingi kuchukua vitambulisho hivyo vinavyotolewa
na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Mwenyekiti huyo wa CUF alisema chama chake
kikipewa ridhaa na Watanzania ya kuongoza nchi kitatumia rasilimali
zilizopo nchini za madini, gesi, mafuta, mbuga za hifadhi na maeneo ya
utalii kuweza kuboresha miundombinu, lakini kuwapatia fedha taslimu
wananchi ikiwa ni njia rahisi ya kupambana na umasikini.
NISHATI YA GESI
Mwenyekiti wa CUF alisema nchi nyingi duniani zilizopata nishati ya gesi na mafuta zimejikuta katika mgogoro mkubwa ikiwa usimamizi wa raslimali hiyo utawanufaisha wachache na kutolea mfano wa Nigeria.
Profesa Lipumba alidai kuwa watafiti wamegundua kuwa gesi iliyogunduliwa Mtwara inafuti za ujazo trioni 33, kiwango ambacho kinaweza kuvunwa kwa zaidi ya miaka 10 na kina uwezo wa kuingizia serikali wastani wa pato la Sh 6.5 bilioni (USD 4 milioni) mpaka Sh 8.1 bilioni (USD5 milioni) kwa mwaka.
Mwenyekiti wa CUF alisema nchi nyingi duniani zilizopata nishati ya gesi na mafuta zimejikuta katika mgogoro mkubwa ikiwa usimamizi wa raslimali hiyo utawanufaisha wachache na kutolea mfano wa Nigeria.
Profesa Lipumba alidai kuwa watafiti wamegundua kuwa gesi iliyogunduliwa Mtwara inafuti za ujazo trioni 33, kiwango ambacho kinaweza kuvunwa kwa zaidi ya miaka 10 na kina uwezo wa kuingizia serikali wastani wa pato la Sh 6.5 bilioni (USD 4 milioni) mpaka Sh 8.1 bilioni (USD5 milioni) kwa mwaka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni