Jumatano, 8 Januari 2014

BREAKING NEWS: WASAFIRI WANAOTUMIA RELI YA KATI WAANDAMANA KUELEKEA KWA MKUU WA MKOA WA DODOMA KUSHINIKIZA WAPEWE USAFIRI KUFUATIA KUKWAMA DODOMA ZAIDI YA WIKI MBILI

 Waandamanaji wakielekea kwa mkuu wa mkoa wa Dodoma

Kufuatia kukwama  station ya dodoma kwa zaidi ya wiki mbili sasa, abilia wanasafiri kwa usafiri wa treni ya kati inayotoka Dar es salam hadi Kigoma wameamua kuandamana kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Rehema Nchimbi ili awasaidie abilia hao kupatikana kwa ufumbuzi juu ya suala lao la usafiri.
Abilia hao  wakiwa wanaongea kwa uchungu wanamwomba mkuu wa mkoa awapatie ufumbuzi wa tatizo lao ili waweze kusafiri kuelekea makwao hasa ukizingatia kuwa hadi sasa ni zaidi ya wiki mbili wamekwama hapa Dodoma huku wakiwa hawana pesa kwa ajili ya kula na kulala.

Waandamanaji hao waliandamana bila kuleta vurugu zozote kuelekea kwenye ofisi za mkuu wa mkoa huku wakipita kuimba kuwa wanataka usafiri wa mabasi ikiwa kama njia mbadala wa usafiri wa treni. Kwa mantiki hiyo walimtaka mkuu wa mkoa wa Dodoma awasaidie kuwashinikiza uongozi wa shirika la reli kanda ya kati wawapatie usafiri wa mabasi abiria hao ili waweze kurudi makwao.

Abiria hao wanasema wamevumilia kwa muda mrefu sana huku viongozi wa reli kanda ya kati hawakuonekana kujali matatizo yanayowapata abilia hao.

Waandamanaji hao waliweza kuzuia kwa muda shughuli za watu huku wakisababisha msangamano wa magari hali iliyolazimu polisi kuingilia kati ili kuyaongoza maandamano hayo. Maandamano hayo yalianza majira ya saa 3:20 hivi asubuhi.

 Waandamanaji wakizidi kusonga kuelekea kwa mkuu wa mkoa

Hakatwi mtu hapa!!waandamanaji wakidai haki yao ya kusafirishwa kufuatia treni yao kuharibuka Dodoma na kushindwa kuendelea na safari 

 Waandamanaji wakipita kuimba kuelekea kwa mkuu wa mkoa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD