Jumatano, 1 Januari 2014

KUELEKEA KATIBA MPYA: TASISI ZA KIJAMII, VYAMA VYA SIASA NA VYA KITAALUMA WAPELEKA KWA RAIS WANAOPENDEKEZA WAWEMO BUNGE LA KATIBA



Taasisi mbali mbali za kijamii, vyama vya kitaaluma na vyama vya siasa vipatavyo 50 hadi leo, Jumanne, Desemba 31, 2013, vimewasilisha majina ya watu vinaowapendekeza wafikiriwe kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

Taarifa iliyotolewa leo mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue na kusambazwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu pia Dar es Salaam, imesema taasisi hizo zimewasilisha majina yao kwa mujibu wa mwaliko uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa makundi yaliyobainishwa katika Kifungu cha 22(1) (c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba (Sura ya 83).

Taarifa hiyo imesema kuwa makundi hayo 50 yaliyowasilisha majina yanayopendekezwa kwa ajili ya uteuzi yanatokana na barua 169 zilizopokelewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar.

Makundi ambayo yamewasilisha majina ni yafuatayo: Shirika la Wasaidizi wa Jamii Kabila la Wagogo, Tanzania Association of Social Workers (TASOWA), Teachers and Student Forum Tanzania, Tanzania Women Teachers Association, Umoja wa Wanawake Wajane Wilaya ya Karagwe na Kyerwa (UWK), Tanzania Peace and Development Society, Better World Organization (BWO), Youth Focus and Development, Association of Traditional Medicine Man, Registered Centre for Good Governance and Development in Tanzania, Chama Cha Kijamii (CCK), CHANETA na Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania.

Makundi mengine ni Legal Aid Iringa Village, Tanzania Kilolo Orphans and Social Development Organization, Legal aid and Social Welfare Association, Legal and Human Right Centre, Tanzania Lift Initiative NGO, Kilolo Paralegal Unit, Women Development and Social Activities Association, Defence of Human Right/Citizen Rights, DAWSEN Trust Fund, Baruti Development Association (BADEA), Living Hope Ministries Trust, EFATHA Ministry, Bethel Assemblies of God Tanzania, Muslim and Christian Brotherhood Society, Baraza Kuu la Waislamu wa Kondoa – Tanzania na Jesus Temple Inner Transformation News.

Taasisi nyingine ni Jumuiya ya Waithna Asharriyyah Tanzania,   Rehmatfi Sabilillah Trust of Tanzania,  Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), National Reconstruction Alliance (NRA), Sauti ya Umma (SAU), Chama cha Demokrasia Makini, African Progressive Part – APPT Maendeleo, National League for Democracy, Tanzania Film Federation, Taasisi ya Maendeleo ya Utamaduni, Al-Amoud General Enterprises, Blue Belt and Water Sources Control, Community Development Training Institute – Tengeru,  Tanzania Medical Student Association, Tanzania Sea Farmers Union, Medical Association of Tanzania, Chama cha Wastaafu wa Mbinga, Union of Tanzania Press Clubs, Umoja wa Wanawake Tanzania, Alliance for Tanzania Farmers Party, Tanzania Social Economic and Environment and Wellbeing.

Kwa vile mwisho wa kupokea orodha ya majina hayo ni tarehe 02 Januari, 2014, Balozi Sefue ametoa mwito kwa makundi mengine ambayo hayajawasilisha orodha hiyo kufanya hivyo kabla muda uliowekwa kuisha. Aidha, wakati wa kuwasilisha ni muhimu kuzingatia vigezo vilivyowekwa na sheria na kama vilivyofafanuliwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 443 lililochapishwa tarehe 13 Desemba, 2013. Vilevile ni muhimu kuzingatia kuwa majina yanayopendekezwa na Taasisi au makundi yaliyoainishwa kwenye sheria na siyo mtu binafsi kujipendekeza mwenyewe.

 Kwa wale watakaojipendekeza wenyewe wajue kuwa watakuwa wanakwenda kinyuma na maelekezo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD