Jumatatu, 9 Juni 2014

UZALENDO NA NIDHAMU KATIKA MATUMIZI YA RASILIMALI ZA UMMA

Kwanini Tanzania masikini. Mimi nadhani viongozi wetu tuliowachagua hawawajibiki vyakutosha kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu. Wanapenda kuishi maisha ya anasa kana kwamba Tanzania na Watanzania ni Matajiri. 

Wanasiasa pia wanalifilisi taifa hili. Ebu fikiria kuna ulazima gani wa mbunge mmoja kulipwa tsh 300000/= kwa siku ili hali nchi yetu ni masikini. Kuna ulazima gani wa kununua magari ya kifahari ya shilingi milioni 200 ili hali watanzania wezetu wanakufa kwa njaa, wanafunzi hawana madawati ya kukalia, walimu wanalalamika maslahi madogo, madaktari nao pia.

Ningekuwa Rais ningeagiza viongozi wote wa serikali watumie tax gari zinazoendana na uwezo wetu. Wabunge wa bunge la katiba na bunge la bajeti ningewalipa tsh elfu 85 tu kwa siku kama wafanyakazi wengine wanapoenda kufanya kazi nje ya mkoa wake.

Ili tuendelee lazima tukubali kuishi kwa ubahiri na mikati mikubwa ya kuhakikisha kuwa Tanzania na Watanzania tunawakomboa kutoka kwenye lindi la umasikini.

Tujenge miundo mbinu itakayo rahisisha kuchumi wetu upae.

Hakuna faida ya kwenda kuficha nje mabilioni ya pesa ili hali watanzania wenzako wanakufa njaa hapa nchini kwako.

Tujifunze kuhurumiana. Kwa pamoja tunaweza kutokomeza lindi la umaskini katika nchi yetu 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD