RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete amefanya ziara ya kikazi mkoani Ruvuma. Akiwa katika ziara hiyo ambayo imefanyika kwa siku saba kuanzia Julai 17 hadi 23, Rais KIKWETE amefanya mambo makubwa ya kimaendeleo ikiwemo kukagua, kuzindua, kufungua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wananchi waliopo katika maeneo mbalimbali mkoani humo, ambako Rais Kikwete alipita kufanya shughuli hizo muhimu ikiwemo mikutano ya hadhara katika kila wilaya zilizopo mkoani Ruvuma, walijitokeza kwa wingi huku wakiimba nyimbo za kumsifu na kumshangilia. Wananchi wengi wamefarijika na ujio wa Rais Kikwete hasa wakikumbuka kazi nzuri inayoendelea kufanywa chini ya utawala wake mkoani Ruvuma.
Rais Kikwete akiwa katika Manispaa ya Songea aliweka jiwe la msingi nyumba bora za gharama nafuu ambazo zinajengwa na shirika la nyumba la Taifa (NHC). Aidha, Rais KIKWETE alifungua Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mkoa wa Ruvuma ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja.
Kadhalika alikagua na kuzindua ghala jipya la hifadhi ya Taifa ya chakula (NFRA) lililopo mjini Songea. Akiwa ziarani wilaya ya Nyasa, Rais KIKWETE alizindua daraja jipya la Ruhekei na mradi wa umeme vijijini (REA) uliopo Mbamba Bay.
Kwa wilaya ya Mbinga, Rais KIKWETE alifungua barabara kuu ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ya kutoka Mbinga hadi Songea ambayo ni sehemu ya miradi ya changamoto za milenia (MCC). Aidha, Rais KIKWETE alifungua kituo kikuu cha mabasi ambacho kimejengwa Mbinga mjini.
Rais Kikwete akiendelea na ziara yake mkoani Ruvuma, alifungua soko la kimataifa la Mkenda ambalo limejengwa mpakani mwa nchi ya Tanzania na Msumbiji ambalo litawanufaisha wananchi wa pande hizo mbili.
Wilayani Namtumbo Rais KIKWETE alizindua hospitali ya wilaya hiyo. Pia alizindua barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Songea hadi Namtumbo. Pia aliweka jiwe la Msingi ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Namtumbo, Tunduru hadi Sauti moja wilayani Tunduru.
Wilayani Tunduru Rais KIKWETE alizindua nyumba 40 ambazo zimejengwa na taasisi ya Mkapa Foundation zilizopo katika kijiji cha Matemanga. Nyumba hizo ni sehemu ya nyumba 400 zinazojengwa na taasisi hiyo Mkoani Ruvuma. Pia Rais KIKWETE alizindua mradi wa maji uliopo tarafa ya Nalasi wilayani humo.
Rais Kikwete amehitimisha ziara yake jana Julai 23, kwa kufanya majumuisho ya ziara yake Tunduru mjini na kuondoka wilayani humo kuelekea Masasi na Nachingwea ambako amezindua na kuweka mawe ya msingi ujenzi wa barabara na kufungua Mradi wa Maji wa Ngwinji ambao utawanufaisha wakazi wa miji ya Nachingwea na Masasi.
Sisi wana Ruvuma hakika tumefarijika sana kutokana na ujio wa Rais wetu Mpendwa. Katika kumbukumbu yangu, hii ni mara ya kwanza kwa Rais yeyote wa Tanzania kuwa na ziara ya siku nyingi Mkoani mwetu na yawezekana pia mkoa wowote ule. Ninaamini kuwe uwepo wa Rais KIKWETE kwa siku zote hizo hakujatokana na matakwa yake hasa ikizingatiwa kuwa ana majukumu mengi ya kitaifa bali umesukumwa na juhudi za wana Ruvuma kujiletea maendeleo yao chini ya usimamizi wa Chama Tawala, CCM na serikali yake. Kwa hakika Rais KIKWETE hakukaa bure wakati wote alipokuwa Ruvuma na hadi anaondoka, kuna miradi mingi alikuwa hajaipitia.
Ziara ya Rais KIKWETE mkoani Ruvuma inapaswa kuwa somo kwa mikoa mingine. Hii ni kutokana na ukweli kuwa si kila mradi una hadhi ya kufunguliwa, kuwekewa mawe ya msingi au kuzinduliwa na Rais. Wana Ruvuma tumejituma sana na tumetumia nguvu zetu, fedha zetu na vitu vingine kwa lengo la kufanikisha miradi husika. Huwa nawahurumia sana wananchi wa mikoa mingine ambao kila mara wamekuwa wakidanganywa kuwa wananchi hawatakiwi kuchangia maendeleo yao kwa madai kuwa ni wajibu wa serikali. Hakika huko ni kuchelewesha maendeleo. Wananchi wengi waliojitokeza kumlaki Rais KIKWETE walisikika wakisema kuwa hawataki upinzani kwenye maeneo yao kwa vile wao ni adui mkubwa wa maendeleo. Kwamba mwaka 2015 CCM watapata ushindi mkubwa sana hasa kwa vile wananchi wanakiamini na hivyo ni wajibu wao kuk
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni