Ni katika hali isiyo ya kawaida, mtendaji wa kata ya Kitanda wilayani Namtumbo Bwana Fidea Mbawala amekuta jeneza likiwa limefunikwa vizuri kana kwamba kuna maiti ambayo inahitajika kwenda kuzikwa hivi punde. Tukio hilo limetokea katika kijiji cha kitanda ambapo watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo walimwekea jeneza hilo mlangoni kwake kwa sababu ambazo bado hazijaweza kufahamika.
Taarifa zaidi zinadai kuwa mtendaji huyo alipoamka asubuhi na kutoka nje ndipo alipokutana na jeneza hilo mlangoni baada ya kufungua mlango mkubwa wa nje. Bwana Mbawala alipoona jeneza hilo alishituka huku akioneka mwenye huzuni iliyoambata na uwoga.
Bwana mbawala hakuweza tena kutoka nje, ilibidi afunge mlango na kuingia tena ndani huku akiwa analia kwa simanzi kama mtu aliyefiwa. Ilibidi apige simu polisi kwa ajili ya kutoa taarifa.
Tukio hilo limevuta hisia watu wengi kwani halijawahi kutokea kijijini hapo. Baada ya watu kuwasili walimtoa mlango wa pili huku ule mlango wenye jeneza ukibaki umefungwa na jeneza kuendelea kubaki kama lilivyo pale mlangoni huku umati mkubwa wa watu ukiwa umejaa nyumbani kwa mtendaji huyo.
Awali mkuu wa wilaya ya Namtumbo aliagiza watendaji wakusanye michango kwa wananchi kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari ya kata ya Kitanda ijulikanayo kwa jina la Mkomanile, na akamwagiza dawani wa kati hiyo Bwana Titus Fedinand Ng'oma na Mtendaji wake bwana Mbawala wahamasishe watu katika utoaji wa michango hiyo na kwamba yeyote asiyetoa michango hiyo akamapatwe mara moja.
Uhamasishaji ulifanyika lakini mwitikio ulikuwa mdogo na mtendaji hakuweza kuwakamata watu walioshindwa kutoa michango hiyo.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ya Namtumbo alimwagiza diwani wa kata hiyo Bwana Ng'oma pamoja mtendaji wake bwana Mbawala wakamatwe na wapelekwe polisi kwa kupuuza agizo lake. Mnamo tarehe 24/09/201, diwani na mtendaji walikamatwa na kufikishwa polisi. Baada ya maelezo diwani aliachichiwa akiambiwa arudi siku ya pili kwa mahojiano zaidi huku mtendaji wa kata akiendelea kushikiliwa na polisi ingawa badae waliachiwa na kutakiwa kwenda kukusanya michango hiyo na kwamba atakaye kataa akamatwe mara moja. Baada ya kuwatangazia wanachi walipe michango hiyo na kwamba asiyelipa atakamatwa na kufikishwa mahakamani, ndipo mtendaji akakumbana na zahama hili.
Wadadisi wanalihusisha tukio hilo na michango iyoendelea kukusanywa na kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari ya kata ya kitanda ya Mkomanile, na kwa kufanya hivyo ni kujaribu kumtisha mtendaji huyo ili aogope kuwachangisha pesa wananchi hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni