Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Semina. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Semina. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 28 Septemba 2014

TAREHE MPYA YA SEMINA YA UFUGAJI BORA WA KUKU SONGEA NA DAR ES SALAAM


Kutokana na sebabu zilizo nje ya uwezo wetu, ile Semina ya ufugaji bora wa kuku sasa kufanyika tarehe 01/11/2014 badala ya kuhairishwa tarehe 27/09/2014, tunaomba radhi kwa usumbu uliojitokeza.


Kwa taarifa kamali pitia tangazo hilo hapo chini au piga 0767989713/0715989713 au kwa mratibu wa semina hiyo kwa namba 0655663900


Click image for larger version. 

Name: IMG-20140926-WA0000.jpg 
Views: 0 
Size: 242.1 KB 
ID: 188785

Tarehe 11/10/2014, kutakuwa na semina kama hiyo Songea katika ukumbi wa Familia Takatifu Bombambili, tiketi zinapatikana kwa bwana Siphael Mgeni, wakala maarufu wa kusambaza vifaranga wa kuku mkoani Ruvuma anapatikana mtaa wa Zanzibar jengo la CCM, au waweza mpigia kwa simu namba 0717705614 au 0684812938.

Kwa ufugaji wenye tija, unakaribishwa katika semina
Tangozo hilo hapo chini ni kwa ajili ya semina ya Songea. Hii ni fursa pekee wala si ya kuikosa, njoo kama una jambo lolote linakutakutatiza katika ufugaji wa kuku utapata ufumbuzi siku hiyo, kwa hakika tumejipanga kuwahudumia watanzania.

Click image for larger version. 

Name: SONGEA.jpg 
Views: 0 
Size: 228.2 KB 
ID: 188789





Alhamisi, 26 Juni 2014

NI LANDMARK HOTEL


Kumekuchaaa Dar es salaam. Ni tarehe 20/09/2014 ndani ya Landmark Hotel, ni semina ya aina yake kuwahi kufanyika. Nitakuwemo katika wale watakao toa mada siku hiyo. Ni fursa pekee kwa wale  wanaofuga na wanaohitaji kuanza kufuga nk. Karibu tukutane tuonyeshane utajiri uliojificha katika ufugaji wa kuku, hakuna haja ya kulalamika. Anza sasa kufuga kuku unufaike Kiuchumi. 


Ni semina ya aina yake kwasababu mambo mengi yatahusika siku hiyo kama ambavyo yamebainishwa kwenye hilo tangazo hapo juu.



Siyo siku ya kukosa siku hiyo. Ni fursa pekee kwa wafugaji  na wadau wa kuku Dar es salaam na maeneo jirani. 

Karibu nyote.




Jumatano, 18 Juni 2014

TANGAZO LA SEMINA YA WADAU WA TASNIA YA KUKU WA DAR-ES- SALAAM


Habarini wadau,


Still niko humu uwanjani.

Leo nina habari njema kwa waazi wa Dar es salaam. Kuna semina kabambe inaratibiwa  soon nitawapa habari kamili. Mimi pia nitakuwa mjengoni katika wale watakao wasilisha maada siku hiyo. Kaani mkao wa kula ni semina ya siku moja kiingilio ni tsh 20000/=

Kama kweli  wewe ni mfugaji ama unakusudia kuanza ufugaji basi tafadhali usikose siku hiyo. Ukikosa utakuwa umepitwa na mengi. 

Wadau mbalimbali wa kuku watakuwepo siku hiyo, mabenki yanayotoa mikopo kwa wafugaji, wafugaji wakubwa wa kuku waliofanikiwa katika ufugaji wao watatoa ushuhuda  siku hiyo, wanunuzi wa mazao ya kuku, watu wa mahoteli mbalimbali, supermarkets,nk madaktari na watu waliobobezi  katika tasnia ya kuku nk. Watakuwepo pia wazalishaji wa vifaranga, watengenezaji wa vyakula mbalimbali vya kuku, watengenezaji wa Incubators wa ndani ya nchi na wawakilishi wa watengenezaji wa mashine za nje.

Kila kitu utakachohitaji kukifahamu siku hiyo utafahamu. Je wajua ukitaka kuanzisha hatchery hatua gani muhimu za kufuata, nini kinahitajika na wapi uanzie, siku hiyo ni siku muafaka.

Mambo yakikaa sawa tutawajulisha,lini na ukumbi gani semina hiyo itafanyika. Kwa wale watakaohitaji basi tuwasiliane kupitia namba zangu 0767989713, 0715989713 na 0786989713

Kwa pamoja tunaweza kuutokomeza umasikini.

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD