Jumapili, 24 Novemba 2013

KINANA AWASILI KYELA BAADA YA SAFARI YA ZAIDI YA SAA 24 KWA MELI KUTOKA MBAMBA BAY MKOANI RUVUMA

Sunday, November 24, 2013
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24,2013.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana 'akiwasaluti' Wananchi baada ya kuwasili katika bandari ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengerema na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiri (kulia), wakishuka kutoka katika mv Songea, baada ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Godfrey Zambi, baada ya kushuka katika Mv Songea, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013.
 Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe akimlaki wa furaha, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipompokea katibu mkuu huyo, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi, baada ya kuwasili katika bandari ndogo ya Kiwira, wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24,2013.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Kushoto, aliyenyoosha mkono) akikagua kivuko katika bandari ya zamani ya Itunge, baada ya kuwasili  wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Mbamba Bay, Songea, leo Nov 24, 2013. Bandari hiyo ambayo imekufa kwa miaka mingi sasa, ipo katika mpango wa kufufuliwa na serikali.
 Nahodha wa mv Songea Tom Faya akimpatia maelekezo ya namna meli hiyo inavyofanya kazi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, wakati katibu mkuu huyo alipokuwa  akisafiri na meli hiyo kutoka Mbamba Bay mkoani Ruvuma kwenda Kyela mkoani Mbeya, leo Nov 24,2013. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Kwenye usukukani ni Nahodha Msaidizi, Conrad Shauritanga.
Baadhi ya abiria waliosafiri na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika mv Songea, alipokuwa alitokea Mbamba Bay mkoani Ruvuma kwenda Kyela mkoani Mbeya. Meli hiyo iliyoanza kazi katika Ziwa Nyasa, mwaka 1974, ina uwezo wa kubeba abiria 213 wakiwemo wafanyakazi 13 wa meli hiyo.

KINANA AMALIZA ZIARA WILAYANI NYASA, AKWEA MELI KWENDA KYELA KUENDELEA NA ZIARA MKOANI MBEYA

Saturday, November 23, 2013
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, asubuhi hii amemaliza ziara yake katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na kuanza safari ya kwenda Kyela ambako ataanza ziara katika mkoa wa Mbeya. Pichani, Kinana na wajumbe wa sekretarieri ya CCM, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi) na Dk. Asha-Rose Migiro (Siasa na Uhusiano wa KIImataifa), wakiwapungia mikono wananchi wa Nyasa, baada ya kupanda Mv Songea katika bandari ndogo ya Mbamba Bay, kuanza safari ya kwenda Kyenla. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyasa, Ernest Kahindi 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na wananchi wa Mbamba Bay, Nyasa, kabla ya kupanda meli kwenda Kyela
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migirob akisalimiana na Nahodha wa Mv Songea Tom Faya, katika bandari ndogo ya Mbamba Bay, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma kabla ya safari ya kwenada Kyela
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Nahodha wa mv Songea, kabla ya safari ya kwenda Kyela kutoka bandari ndogo ya Mbamba Bay, Nyasa. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa Oddo Mwisho
 Mkurugenzi na Mtayarishaji Mkuu wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye ni baadhi ya abiria walioko katika msafara wa Kinana,akipanda mv Songea.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipanda mv Songea. Wanaomfuata na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho na katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Wananchi na wanachama wa CCM wa Mbamba Bay, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, wakisindikiza kwa boti mv Songea wakati ikiondoka bandarini
Nahodha wa ,mv Songea na Kinana wakizungumza na waandishi wa habari. Imetayarishwa na theNkoromo Blog

KINANA AVUNA WANACHAMA KIBAO KUTOKA UPINZANI

Friday, November 22, 2013
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya jinsi ya kutumia vifaa vya maabara katika kufanikisha kutambua kemikali kutoka kwa wanafunzi wa kidato cha nne Erasto Ndumba na Stella Hyera wa shule ya sekondari ya Kata ya Mtakatifu Paul kata ya Liuli wilaya ya Nyasa
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi nyumba za madaktari zilizochini ya mradi wa Taasisi Benjamini Mkapa katika kituo cha afya  Mkili kata Liundi wilayani Nyasa.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishauri jambo kabla ya kuvuka mtu Ruhuhu kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM Ndugu Oddo Mwisho.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Ndugu Ernest Kahindi wakivuka kwa mtumbwi kuelekea kijiji cha Kipingu wilaya ya Ludewa.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa, Kijiji hicho kipo mpakani wa mkoa wa Ruvuma na Njombe.

Katibu Mkuu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata Kipingu kijiji cha  Kipingu wilaya ya Ludewa ambapo aliwaambia ahadi ya kujengwa kwa daraja la mto Ruhuhu, uzalishaji wa umeme utakotosheleza mahitaji ya  wilaya ya Nyasa na Ludewa pamoja na mradi wa umwagiliaji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipungia wananchi wakati akirejea kijiji cha Lituhi kwa Mtumbwi  baada ya kutoka kuwasalimu wakazi wa kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa,wengine pichani ni Dk.Asha-Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na kikundi cha akina mama wakulima wa mpunga na mboga mboga wa kijiji cha Lituhi katika viwanja vya Lituhi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Verena Shumbusho wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa  Mbinga Magharibi Kapteni John Komba wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mikutano Lituhi ambapo vijana 12 kutoka vijiji mbali mbali walipewa mabati kwa ajili ya kuezeka nyumba zao.
 Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba akimtambulisha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kama Ndugu yake wa karibu kwani mafanikio yake yametokana na mchango mkubwa wa Marehemu Mzee Nnauye ,Pia Komba alimuelezea Kinana kama mmoja wa walimu wake wazuri wa masomo ya kijeshi pamoja na siasa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akionyesha kadi za wanachama  wa Chadema waliorudi CCM baada ya chama chao kuanza kuparanganyika,mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya Lituhi ambapo wanachama zaidi ya 400 wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama waliojiunga na CCM kutoka vyama vya upinzani.

KINANA AANZA ZIARA YA NYASA

Thursday, November 21, 2013

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Rudisha baada ya kumsimamisha na kumtaka asalimiane wananchi .
 Ujumbe unaomtaka Katibu Mkuu wa CCM Ndugu asimame kwenye kijiji cha Maganagana japo wamsalimi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na wananchi wa kijiji cha Makatani wakati akielekea wilaya mpya ya Nyasa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Luhangarasi  wilaya mpya ya Nyasa.
 Katibu wa NEC  Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimia  wananchi wa kijiji cha Luhangarasi wilaya mpya ya Nyasa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubeba  matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Kata ya Luhangarasi.
 Wanachama  wa shina namba 1 kwa Balozi Joseph Nduguru tawi la Luhangarasi wilaya ya Nyasa wakicheza kwa furaha wakati wa kumaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Kingerikiti wilaya ya Nyasa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la ofisi ya CCM  wilaya ya Nyasa kulia ni Mbunge wa Mbinga Kapteni Jonh Komba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Kilosa wakati wa  ukaguzi,timu ya Kilosa ilicheza mechi ya kujipima nguvu na timu ya Mbamba Bay.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga mpira kama ishara ya ufunguzi wa mechi kati ya timu za mpira za wanawake Kilosa na Mbamba bay

Mbunge wa Mbunge wa Mbinga Magharibi Ndugu Kapteni John Komba akihutubia wananchi kwenye viwanja vya michezo Mbamba bay.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD