Jumatano, 27 Novemba 2013

NAFASI ZA KAZI SERIKALINI MWISHO 10/12/2013

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
 
Kumb. Na EA.7/96/01/E/26                                                                                                                               27 Novemba, 2013
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 2748 za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo,Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpanda, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nkasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sumbawanga na Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni.

Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chato, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misenyi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ngara, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya 2

Bukoba, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkinga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilindi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Korogwe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Pangani, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Korogwe na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muheza.

Nafasi hizo pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulyankulu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uyui, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nzega, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Nzega, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Manispaa ya Tabora, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ikungi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iramba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Manyoni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Singida, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Itilima na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ushetu.

Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Msalala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kishapu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukombe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Meatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bariadi, Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyasa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Namtumbo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbinga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Manispaa ya Songea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyang`wale, Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misungwi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ukerewe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Geita na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Magu. 3

Nafasi hizo za kazi pia ni kwa aajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tandahimba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Newala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Masasi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Gairo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mvomero, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilombero, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ulanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Morogoro, Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Tunduma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Momba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbarali, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ileje, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyela, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chunya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbozi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbeya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rorya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Serengeti, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bunda, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tarime, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Butiama, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ruangwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nachingwea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Lindi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mwanga na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Hai.

Katika nafasi hizo waajiri weengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rombo, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Moshi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uviza, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Monduli, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Babati, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Hanang, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Simanjiro, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kisarawe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iringa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Makete, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chamwino, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi 4

Halmashauri Wilaya ya Kongwa na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bahi,

Waajiri wengine katika nafasi hizo za kazi ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Chemba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kongwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilolo, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ludewa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Wanging`ombe, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kasulu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kakonko, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu Tawala Mkoa Pwani, Katibu Tawala Mkoa Dodoma, Katibu Tawala Mkoa Iringa, Katibu Tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu Tawala Mkoa Mtwara, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Katibu Tawala Mkoa Ruvuma, Katibu Tawala Mkoa Tabora, Katibu Tawala Mkoa Kagera, Katibu Tawala Mkoa Dar es salaam, Katibu Tawala Mkoa Rukwa, Katibu Tawala Mkoa Katavi, Katibu Tawala Mkoa Njombe, Katibu Tawala Mkoa Njombe, Katibu Tawala Mkoa Simiyu na Katibu Tawala Mkoa Geita.

MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.

ii. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa.

iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

v. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.

- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

- Computer Certificate

- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

5

- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.

ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xii. WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES SALAAM WANAOMBWA KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO MENGINE.

xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 10 Desemba, 2013

xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.

xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

xvi. Kila mwombaji kazi atapangwa katika kituo chochote cha kazi bila kujali eneo/mahali alipoomba kutokana na mahitaji ya mwajiri pamoja na idadi ya waombaji katika eneo husika.


Katibu,                                                   AU                                               Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika                                                                       Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,                                                                                  Secretariat,
SLP.63100,                                                                                               P.O.Box 63100
Dar es Salaam.                                                                                         Dar es Salaam.

1.0 AFISA UVUVI DARAJA LA II (FISHERIES OFFICER GRADE II) – NAFASI 39

1.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kutekeleza Sera ya Uvuvi.

 Uhifadhi wa samaki na viumbe wengine wa majini na mazingira yao.

 Kuratibu na kusimamia uhifadhi wa mazingira.

 Kuendeleza uvunaji endelevu wa samaki na viumbe wengine wa baharini, maziwa, mito, mabwawa na malambo.

6
 Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu Uvuvi bora, utengenezaji na udhifadhi bora wa Samaki na mazao ya uvuvi, Biashara na Masoko ya Samaki pamoja na Ufugaji wa Samaki na viumbe wengine wa majini.

 Kutoa leseni za uvuvi.

 Kuendesha mafunzo ya taaluma ya uvuvi.

 Kusimamia na kutekeleza Sheria za Uvuvi (k.m. kuzuia uvuvi haramu).

 Kusimamia ukusanyaji wa takwimu za uvuvi pamoja na maduhuli.

 Kuratibu shughuli za utafiti wa uvuvi.

 Kutoa ushauri na Mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali ya uvuvi.

 Kukagua ubora wa Samaki na mazao ya uvuvi na kuweka viwango vya Kitaifa.


1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (Bachelor Degree) katika fani za Sayansi ya Uvuvi (Fisheries Science/Management, Zoology, Microbiology, Marine Biology, Food Science and Aquaculture).


1.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.

2.0 MVUVI MSAIDIZI DARAJA LA II (FISHERIES ASSISTANT II) – NAFASI 18

2.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kutengeneza, Kushona, Kutunza na Kukarabati zana za uvuvi.
 Kutunza na kuangalia mabwawa ya samaki.
 Kutega mitego Ziwani au Baharini.
 Kutengeneza nyavu ndogo ndogo.
 Kuwapa chakula samaki katika mabwawa.
 Kuvua samaki katika mabwawa.
 Kutoa ushauri kwa wavuvi kuhusu mbinu mbalimbali za uvuvi.
 Kukusanya takwimu za uvuvi kutoka kwenye vituo vya kupokelea samaki.
 Kutoa ushauri juu ya uhifadhi wa samaki na mbinu za usambazaji na uuzaji wa mazao yatokanayo na samaki.
 Kuwaelimisha wananchi juu ya ufugaji wa samaki na mambo muhimu ya kuzingatia.

2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye stashahada (Diploma) ya Uvuvi au Uhifadhi wa Samaki na Masoko (Fish Processing & Marketing) kutoka vyuo vya uvuvi vya Mbegani, Kunduchi au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

7
2.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi
3.0 AFISA MIFUGO MSAIDIZI DARAJA LA II (LIVESTOCK FIELD OFFICER II) – NAFASI 473

3.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Atafanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa wafugaji wa eneo lake.
 Kwa kushirikiana na wakaguzi wa afya, atakagua nyama na usafi wa machinjio mara kwa mara.
 Atakusanya takwimu za nyama na mazao yatokanayo na mifugo k.m ngozi na kuandika ripoti.
 Atatibui magonjwa ya mifigo chini ya usimamizi wa Daktari wa mifugo na kushauri wafugaji jinsi ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa.
 Atatembelea wafugaji mara Kwa mara na kuwapa ushauri fasaha wa kitaalam katika eneo Lake Kazi.
 Atakusanya takwimu zote za maendeleo ya mifugo katika eneo lake .
 Atashauri na kusimamia ujenzi wa majosho, machinjio, vibanio na miundo mbinu inayohusiana na ufugaji bora.
 Atahusika na uhamilishaji (Artificail Insemination) na uzalishaji (breeding) wa mifugo kwa ujumla.
 Atashauri wafugaji kuhusu mbinu bora za kuzalisha maziwa na utunzaji wa ndama.
 Atafanya kazi nyingine za fani yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.

3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha VI waliofuzu mafunzo ya Stashahada (Diploma) ya mifugo kutoka chuo cha Kilimo na Mifugo (MATI au LITI) au chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali.


3.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi

4.0 AFISA MIFUGO DARAJA LA II (LIVESTOCK OFFICER II) – NAFASI 107
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Atabuni mipango ya uzalishaji mifugo wilayani.
 Ataratibu uzalishaji wa mifugo katika mashamba makubwa ya mifugo.
8
 Atasaidia kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani.
 Ataratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataam wa mifugo na wafugaji.
 Atafanya mapitio na marekebisho ya miundo ya masoko ya mifugo wilayani kwake na mkoani.
 Atabuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani.
 Atafanya soroveya ya rasilimali (resource survey) kama vile mifugo, vyakula vya mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi.
 Ataendesha mafunzo kwa Mawakala, wauzaji na wataalam juu ya njia salama katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo.
 Atatafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali
 Atafanya utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya.
 Atashiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa malisho.
 Ataandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo.
 Atafuatilia, kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.
 Atafanya kazi nyingine zinazohusiana na fani yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya sayansi ya Mifugo (Animal Science) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali au sifa inayolingana nayo.

4.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi


5.0 MTEKNOLIJIA WA SAMAKI DARAJA LA II (FISH TECHNOLOGISTS II) – NAFASI 4
5.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kutoa ushauri juu ya utayarishaji, utengenezaji, ukaushaji na uhifadhi wa samaki na mazao yatokanayo na uvuvi.
 Kusimamia kushauri juu ya kanuni za uthibiti ubora wa Samaki na mazao yake
 Kutoa ushauri juu ya matumizi mbalimbali ya samaki kama chakula bora katika Viwanda na maeneo mengine.
 Kudhibiti ubora wa samaki katika mialo.
 Kudhibiti usafi katika maeneo ya kupokelea samaki.
 Kukagua nyaraka mbalimbali zinazotakiwa kutunzwa melini na viwandani.

5.2 SIFA ZA MWOMBAJI

9

 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Sayansi ya Chakula (Food Science and Nutrition, Food Technology, Microbiology) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

5.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi

6.0 DAKTARI WA MIFUGO DARAJA LA II (VETERINARY OFFICERS) – NAFASI 19

6.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kutoa huduma za afya ya mifugo
 Kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika eneo au sehemu alipo.
 Kutayarisha na kusimamia mipango ya kuzuia, kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya mifugo katika eneo lake.
 Kushiriki katika uchunguzi wa magonjwa ya wanyama pori katika eneo lake.

6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Tiba ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali na wawe wamesajiliwa na Bodi ya Madaktari wa Mifugo nchini.

6.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi

7.0 AFISA UTAFITI MIFUGO DARAJA LA II (LIVESTOCK RESEARCH OFFICER II) – NAFASI 9

7.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kujifunza kumudu mbinu na taratibu za utafiti wa mifugo/ndorobo
 Kufanya utafiti chini ya usimamizi wa Afisa Utafiti Mwandamizi.
 Kuandika na Kuweka kumbukumbu za utafiti.
 Kusaidia kuendesha semina na maonyesho ya ufugaji bora.
 Kuandaa mapendekezo ya utafiti (Research Proposals) kwa kushirikiana na Afisa Utafiti Mifugo anayesimamia.
 Kufanya kazi zozote kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

7.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Sayansi ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

7.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi

10

8.0 DAKTARI UTAFITI MIFUGO DARAJA LA II (VETERINARY RESEARCH OFFICER II) – NAFASI 5
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kujifunza na kumudu mbinu na taratibu za utafiti wa afya na maradhi ya mifugo
 Kuweka kumbukumbu za utafiti
 Kusaidia kuendesha semina na maonyesho ya ufugaji bora.
 Kuandaa mapendekezo ya utafiti (“research proposal”) kwa kushirikiana na Daktari Utafiti Mifugo anayemsimamia.
 Kufanya utafiti chini ya usimamizi wa Daktari Utafiti Mwandamizi
 Kukusanya na kuchambua takwimu za utafiti unaoendelea.
 Kuchapisha taarifa na makala za utafiti
 Kuendesha semina na maonyesho ya ufugaji bora.

8.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (bachelor degree) katika fani ya Sayansi ya Tiba ya Mifugo (“Veterinary Science) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Wawe wamesajiliwa na Bodi ya Madaktari wa Mifugo nchini.

8.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi

9.0 FUNDI SANIFU MAABARA MIFUGO DARAJA LA II (VETERINARY LABORATORY TECHNICIAN II) – NAFASI 6
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kwa kushirikiana na Afisa Mifugo Msaidizi, atafanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika eneo lake.
 Atakusanya sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa maabara.
 Kuwasaidia wataalam kuanda vifaa vya uchunguzi
 Kutunza Usafi wa Maabara na vyombo vilivyomo.
 Kutunza takwimu za uchunguzi
 Atafanya kazi zingine zozote kama atavyopangiwa na mkubwa wake wa kazi

9.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha sita (VI) waliofuzu mafunzo ya miaka miwili (2) ya Stashahada katika fani ya Fundi Sanifu Maabara (Mifugo) kutoka Chuo cha Mifugo (LITI), au chuo kingine kinachotambiliwa na serikali.

9.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi

11


10.0 MKUFUNZI MIFUGO DARAJA II (LIVESTOCK TUTOR II) – NAFASI 5
10.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kutafsiri mihutasari ya mafunzo kwenye masomo.
 Kuandaa mtiririko wa kila somo (Lesson Plan) kwa upande wa nadharia na vitendo.
 Kufundisha kozi za stashahada na astashahada kwa upande wa nadharia na vitendo.
 Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
 Kupima maendelo ya wanachuo kwa kushirikiana na maofisa mifugo wa wilaya, viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo.
 Kufanya kazinyingine zozote za fani yake atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.

10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Sayansi ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

10.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi


11.0 MKUFUNZI WA MIFUGO MSAIDIZI (ASSISTANT LIVESTOCK TUTOR) – NAFASI 3
11.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kuandaa mtiririko (Lesson Plan) wa masomo
 Kufundisha kozi ya astashahada ya mifugo na wafugaji.
 Kusimamia masomo ya vitendo chini ya usimamizi wa Mkufunzi Mkuu wa somo
 Kuandaa na kupanga vifaa kwa ajili ya somo la vitendo
 Kuwapima wanachuo wakati wa mazoezi ya somo la vitendo
 Anaweza kuteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo (dairy, poultry, maabara, museum, nk).
 Kufanya kazi nyingine kadri atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.

11.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita (VI) waliofuzu mafunzo ya Stashahada ya mifugo kutoka MATI/LITI au chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali.

11.3 MSHAHARA

12

 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi

12.0 DAKTARU MIFUGO MKUFUNZI DARAJA LA II (VETERINARY TUTOR II) – NAFASI 1

12.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kutafsiri mihutasari ya mafunzo kwenye masomo
 Kuandaa mtiririko wa kila somo (lesson plan) kwa upande wa nadharia na vitendo
 Kufundisha kozi za stashahada na astashahada kwa upande wa nadharia na vitendo.
 Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na madaktari /maofisa mifugo wa wilaya, wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practicals).

 Kufanya kazi nyingine zozote kadri atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.

12.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Tiba ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Wawe wamesajiliwa na Bodi ya Madaktari Tanzania.

12.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi

13.0 MTEKINOLOJIA WA SAMAKI MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT FISH TECHNOLOGIST II) – NAFASI 6

13.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kutengeneza na kuhifadhi samaki

13.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita waliofuzu mafunzo ya miaka miwili ya uhifadhi na biashara ya samaki (Fish Processing and Marketing) kutoka chuo cha maendeleo ya uvuvi Mbegani au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

13.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B kwa mwezi

14.0 MUUNDA BOTI DARAJA II (BOAT BUILDER II) – NAFASI 2

14.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kusaidia kuunda boti za uvuvi

 Kuwashauri wavuvi juu ya utunzaji na matumizi ya boti

13

 Kufanya matengenezo ya boti.

 Kusaidia kutafsiri/kusoma michoro ya kiufundi ya boti.

 Kuandaa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa boti.


14.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye stashahada ya Uundaji boti kutoka chuo cha Mbegani au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.


14.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi


15.0 DEREVA WA VIVUKO DARAJA LA II (FERRY / BOAT OPERATOR) – NAFASI 1

15.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kufunga na kufungua kamba za kivuko.

 Kuchunga usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya kivuko.

 Kupanga abiria au magari kwenye kivuko.

 Kuendesha na kuongoza kivuko.

 Kutunza daftari za safari ya kivuko.

 Kuhakikisha kwamba injini za kivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi.

 Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi.



15.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa waliohitimu Mtihani wa Kidato cha IV, wenye Ujuzi wa kuendesha na kutunza Mashua/Kivuko uliothibitishwa na Chuo cha Dar es Salaam Marine Institute au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda usiopungua miaka miwili; na waliofuzu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha majini, kuogelea na kupanga watu na magari kwenye mashua/vivuko.


15.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.


16.0 MSAIDIZI MIFUGO (LIVESTOCK FIELD ASSISTANTS) – NAFASI 209

16.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kutoa huduma za ugani katika uendelezaji mifugo na mazao yake,

 Kutibu mifugo na kutoa taarifa za magonjwa, tiba na chakula,

 Kusimamia utendaji kazi wa wahudumu mifugo,

 Kutunza takwimu na taarifa mbalimbali za mifugo,

14



 Kukaguo ubora wa mazao ya mifugo,

 Kusimamia ustawi wa wanyama,

 Kufanya kaza nyingine atakazo pangiwa na msimamizi wake wa kazi zinazohusiana na fani yake.


16.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV ambao wamepata mafunzo ya mifugo ya muda wa miaka miwili na kutunukiwa Astashahada (certificate) ya uzalishaji na afya ya mifugo kutoka vyuo vya mafunzo ya mifugo. (Livestock Training Institute – LITI) au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

16.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B Kwa mwezi.


17.0 AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGRO – OFFICERS) – NAFASI 200

17.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kuthibiti visumbufu vya mazao na mimea,

 Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi,

 Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi,

 Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo,

 Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana,

 Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara,

 Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji,

 Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau,

 Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao,

 Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao mengine,

 Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora,

 Kuandaa, kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora,

 Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,

 Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya kupitishwa,

 Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo,

 Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani,

 Kufanya utafiti mdogo mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya kilimo cha umwagiliaji,

 Kufanya utafiti wa udongo,

 Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulima/wamwagiliaji,

 Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti,

 Kuendesha/kusimamaia vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.

15


17.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya kilimo au shahada ya sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.


17.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D Kwa mwezi.


18.0 AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS) – NAFASI (1098)

18.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio,

 Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio,

 Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora,

 Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti,

 Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo, matumizi ya mbolea na madawa, pembejeo za kilimo,

 Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei kwa wiki mwezi, robo na mwaka ngazi ya halmashauri,

 Kukusanya takwimu za mvua,

 Kushiriki katika savei za kilimo,

 Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu matatizo na teknolojia sahihi za kutumia,

 Kupanga mipango ya uzalishaji,

 Kupima uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi,

 Kutathmini na kusavei maeneo ya vyanzo vya maji kwa ajili ya kuhifadhi,

 Kutunza miti mizazi,

 Kuwatambua wasambazaji wa pembejeo,

 Kutoa mafunzo ya lishe kwa wakulima,

 Kufanya vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu,

 Kusimamia taratibu za ukaguzi,

 Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea,

 Kusimamia shughuli za kila siku za majaribio ya kilimo,

 Kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji,

 Kutoa ushauri wa kilimo mseto,

 Kuandaa sheria ndogo za hifadhi ya mazingira na

 Kutoa taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo.


18.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Sita (VI) wenye stashahada (Diploma) ya kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

16


18.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B Kwa mwezi.

19.0 MHANDISI KILIMO DARAJA LA II (AGRO – ENGINEERS) – NAFASI 82

19.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo,

 Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana,

 Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za umwagiliaji,

 Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji,

 Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafunindisha wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji,

 Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji,

 Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji,

 Kuandaa mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za za kilimo,

 Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta,

 Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora na

 Kushughulikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji ipasavyo.


19.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo cha umwagiliaji na cha zana kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.

19.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS E Kwa mwezi.


20.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II – NAFASI 74

20.1 MAJUKUMU YA KAZI


Fani ya Kilimo

 Kutoa ushauri kwa wakulima kuhusu matumizi bora ya zana za kilimo kwa vitendo,

 Kuwafundisha wakulima kutengeneza na kufanya matengenezo ya zana za kilimo,

 Kuendeleza kilimo cha zana,

 Kukusanya na kutunza takwimu za zana za kilimo,

 Kukusanya na kutunza takwimu za kilimo cha umwagiliaji,

 Kusaidia katika ujenzi wa mifereji ya umwagiliaji,

 Kushiriki katika savei kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji,

 Kushiriki katika ujenzi wa malambo madogo.


Fani ya Maabara 17


 Kufanya mchanganuo (analysis) kikemikali ili kuthibitisha/kutathmini udongo, mimea na mbolea na vielelezo (samples) vinavyohusika kwenye maabara.

 Kutunza vyombo vya maabara,

 Kutunza kumbukumbu za maabara,

 Kutambua, kuthibitisha na kuweka kumbukumbu za takwimu za vidudu mbalimbali vinavyosababisha magonjwa ya mimea,

 Kusaidia kaza za watafiti,

 Kwenda mashambani kuchukua sampuli zinazohitajika kwa uchunguzi katika maabara.


20.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Sita (VI) waliofuzu mojawapo ya mafunzo yafuatayo:

 Mafunzo ya miaka miwili (2) ya stashahada (Diploma) ya ufundi sanifu wa vyombo vya kilimo (agro-mechanics), au ufundi sanifu Umwagiliaji maji, na `Agricultural land use technician`

 Mafunzo ya miaka miwili (2) ya stashahada (Diploma) ya ufundi sanifu wa Maabara,

 Mafunzo ya Taasisi za ufundi (VETA)

 Au sifa zinazolingana na hizo kutoka kaitka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.


20.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C Kwa mwezi.


21.0 AFISA UTAFITI KILIMO DARAJA LA II (AGRICULTURAL RESEARCH OFFICER II) – NAFASI 24

21.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kusaidia kuandika na kukusanya ripoti za utafiti wa kilimo/uchumi kilimo chini ya maelekezo ya afisa utafiti mwandamizi,

 Kukusanya, kurekodi na kuchanganua takwimu za kazi za utafiti zinazoendelea,

 Kuhudhuria mikutano ya Kanda ya kuhuisha programu za utafiti,

 Kusaidia katika kuendesha semina na kuwaelekeza wakulima jinsi ya kutumia teknolojia mpya kwa kuzingatia hali ya uchumi na mazingira yao,

 Kutoa ripoti ya maendeleo ya utafiti na mapendekezo ya utafiti katika mikutano ya kanda ya kuhuisha program za utafiti,

 Kufanya shughuli za utafiti chini ya maelekezo na uangalizi wa afisa utafiti mwandamizi,

 Kuandika mapendekezo ya utafiti chini ya uongozi wa afisa utafiti mwandamizi,

 Kuandika ripoti za miradi ya utafiti kwa ajili ya kupitishwa na afisa utafiti mwandamizi,

 Kufanya majaribio ya husishi ya kilimo ma mifugo katika mashamba ya wakulima kwa kushirikiana na Maafisa Ugani na wakulima wenyewe na

 Kufanya kazi zozote kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

18


21.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Kilimo/Uchumi Kilimo/Uhandisi Kilimo, au sifa inayolingana na hizo kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.

21.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D Kwa mwezi.


22.0 MKUFUNZI WA KILIMO MSAIDIZI (AGRICULTURAL TUTOR) – NAFASI 22

22.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kuandaa mtiririko wa mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans),

 Kuandaa na kufundisha masomo ya kozi za astashahada,

 Kusimamia masomo ya vitendo vya kozi za stashahada chini ya usimamizi wa mkufunzi mkuu wa somo,

 Kuandaa na kupanga vifaa kwa ajili ya somo la vitendo kwa kozi stashahada,

 Kuwapima wanachuo wakati wa mazoezi ya somo la vitendo kwa kozi za astashahada,

 Kupima maendeleo ya wanachuo wa astashahada kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao na

 Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.


22.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha sita waliofuzu mafunzo ya Stashahada (Diploma) ya Kilimo kutoka MATI au chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali.


22.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C Kwa mwezi.


23.0 AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA III (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS) – NAFASI 362

23.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kushirikiana na wakulima kuendesha mashamba ya majaribio na mashamba darasa,

 Kutembelea wakulima/vikundi vya wakulima katika mashamba yao na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya mbinu bora na za kisasa za kilimo cha kibiashara,

 Kufundisha na kuelekeza wakulima juu ya matumizi bora ya mbolea, madawa na zana za kilimo,

 Kukusanya na kutunza takwimu za hali ya kilimo katika kijiji,

 Kubuni na kuandaa vihenge vya kisasa vya hifadhi ya mazao na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mazao,

 Kutoa taarifa juu ya dalili za kuwepo visumbufu vya mimea na mazao,

19


 Kuandaa na kutumia daftari la kilimo katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku,

 Kushiriki katika mchakato wa kuibua fursa na vikwazo vya maendeleo (Opportunities and Obstacles for Development (O & OD) na kuandaa mpango wa maendeleo ya kilimo wa kijiji (Village Agricultural Development Plan (VADP), na

 Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya kila mwezi kuiwasilisha kwa Afisa Ugani wa Kata na nakala kuiwasilisha kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji.



23.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne wenye stashahada (Diploma) ya Kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.



23.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B Kwa mwezi.



24.0 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – NAFASI 100

24.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kuendesha magari ya abiria, magari madogo na malori

 Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo,

 Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,

 Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.



24.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti cha Majaribio ya ufundi Daraja la II (Trade test II).



24.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.



25.0 MLINZI (SECURITY GUARD) – NAFASI 2.

25.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kuhakikisha kwamba mali yoyote ya ofisi inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya idhini.

 Kuhahikisha kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake.

 Kulinda usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku.

 Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi.

20





 Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo la ofisi wana idhini ya kufanya hivyo.

 Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea katika sehemu ya kazi kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika.

 Kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.



25.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne waliofuzu mafunzo ya mgambo/polisi/JKT au Mafunzo ya Zimamoto kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.



25.3 MSHAHARA



Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya mshahara TGOS.A kwa mwezi.

2.0 BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA)

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Na 27 ya mwaka 1967.

2.1 MHASIBU MKUU DARAJA II - NAFASI 1

2.1.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kuratibu kazi ya kujibu hoja za ukaguzi.

 Kuandaa hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha.

 Kuandaa na kuoanisha taarifa za mwezi za Benki.

 Kuandaa taarifa za ukaguzi wa fedha za mwaka.

 Kusimamia, kuthibitisha na kuidhinisha malipo.

 Kufanya kazi zingine kama atakavyoagizwa na msimamizi wake wa kazi.



2.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa mwenye Shahada ya Uzamili ya Uhasibu/ Biashara yenye mwelekeo wa Uhasibu kutoka Chuo/Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.

 Awe na CPA (T).

 Mwenye uwezo wa kutumia mifumo ya kompyuta ya kiuhasibu.

 Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka nane (8) mfululizo katika fani ya uhasibu.



2.1.3 MSHAHARA: PGSS 17



2.2 MSANIFU LUGHA MKUU III - NAFASI 1

2.2.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya utafiti kuhusu istilahi za masomo na kukusanya mapendekezo ya istilahi za Nyanja nyinginezo.
 Kusimamia mawasiliano baina ya Taasisi na wadau wanaohitaji huduma za kusanifu Istilahi au msamiati.
 Kusimamia kazi za utayarishaji wa tafsiri sanifu.
 Kuratibu Warsha, Semina na Mikutano ya Kamati ya Usanifishaji.

21

 Kusimamia sehemu ya Kamusi.
 Kusimamia kazi ya kukusanya na kuchambua istihali mbalimbali kwa ajili ya usanifishaji.
 Kuratibu shughuli za Usanifishaji Lugha.
 Anaweza kuteuliwa kuwa Mkuu wa Idara.
 Kufanya kazi nyingine atakayopangiwa na mkuu wake wa kazi.

2.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa mwenye Shahada ya Uzamili/Uzamivu katika masomo ya Fasihi, Lugha au Isimu ya Kiswahili
 Awe na uzoefu wa kazi katika fani hiyo usiopungua miaka minane (8).
 Awe na uwezo wa kutumia kompyuta
 Awe ameandika makala au kitabu kinachohusu fasihi au isimu ya lugha ya Kiswahili.

2.2.3 MSHAHARA: PTSS 17

3 .0 WAKALA WA VIPIMO
Wakala wa Vipimo ni Taasisi (Wakala) ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Taasisi hii iliundwa kwa mujibu wa Sheria za Serikali Sura Na. 245, mapitio ya mwaka 2002. Wakala wa Vipimo ilianzishwa rasmi tarehe 13 Mei, 2002 kwa amri ya Seriakali Na. 194 (Government Order No. 194) na kutangazwa tarehe 17 Mei, 2002. Chini ya sheria hiyo, Wakala wa Vipimo ina jukumu la kumlinda malaji Kwa kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika katika sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira

3.1 AFISA VIPIMO II – NAFASI 2

3.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kukagua, kuhakiki na kuvirekebisha vipimo vya wafanyabiashara;
 Kutunza, kuhifadhi vifaa vya kitaalam vitumikavyo katika utendaji wa kazi;
 Kutoa ushauri kuhusu masuala ya uhakiki na matumizi ya vipimo;
 Kufanya upelelezi kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Vipimo
 Kupokea na kufanyia kazi malalamiko ya wadau na waateja;
 Kufanya kazi nyingine kama atakavyopangiwa na kiongozi wake zinazohusiana
na elimu na ujuzi wa kazi

3.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza katika fani ya “Legal Metrology” au “Legal and Industrial Metrology” toka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Au

 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Uhandisi/Sayansi ambao wamepata “Crash programme” ya “Legal and Industrial Metrology” isiyopungua miezi minne (4) toka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ya Uhandisi/Sayansi ambao wamehitimu Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) katika fani ya vipimo katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

22
 Kuajiriwa wenye Stashahada ya juu katika fani ya “Legal Metrology” /Legal and “Industrial Metrology” toka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.


3.1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya mshahara (WMAS 3) kwa mwezi.


X.M.DAUDI
KATIBU-SEKRETARIETI YA AJIRA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD