Alhamisi, 14 Novemba 2013

NAWAPONGEZA WANAFUNZI WOTE WA CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE SUA KWA KUMALIZA CHUO

Rafiki zangu wote, wanafunzi wenzangu,
Niwajibu wangu kuwashukuruni nyote, kwa ushirikiano ambao mumeuonyesha kwangu. Mafanikio yangu yametokana na michango yenu. Tumetoka mbali na tumepitia misukosuko mingi lakini hatimaye tumemaliza. Hatunabudi kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutufikisha hapa tulipofika. Safari yetu ilianza mwaka 2010, ni safari iliyokuwa chungu sana kwa kuwapoteza baadhi ya ndugu zetu, rafiki zetu na watanzania  wenzetu ambao kwa namna moja ama nyingine walitamani tungemaliza wote mwaka huu, lakini haikuwa mipango ya mungu.
Kila jambo linapotokea lina sababu zake. Tunapaswa kumshukuru mungu kwa mazuri na mabaya tunayoyapata. Hii yote ni mitihani ambayo mungu ametupatia sisi wanaadamu. Ni mitihani ambayo binaadamu inapokupata yakupasa kutulia na kumwomba mungu akurahisishie katika kuitatua bila kuleta athari.
Niwapongeze wote mliofanikiwa kufaulu vyema mitihani yenu, mungu awatimizie ndoto zenu, na mujitahidi kuitumia elimu yenu kuwasaidia watanzania wenzenu wengi ambao hawakubahatika kupata elimu ya chuo kikuu kama ambavyo ninyi mmeipata. Popote mtakapokuwa chapeni kazi kwa bidii ili uwepo wenu uonekane.
Lakini pia si lazima  kuhangaika kutafuta kazi, mnaweza mkawa nyinyi wenyewe chanzo cha kazi kwa wantanzania wenzenu. Mnapaswa kufikiri kijasiriamali hatimaye muweze kuishi katika maisha bora.
Nirudie kuwapa pole ndugu zangu wote ambao matokeo hayakuwa mazuri katika mitihani yenu, naomba mtambue kuwa hii ni mtihani tu ambao mungu humpatia mja wake kama njia ya kumpima namna atavyoupokea mtihani huo, kama  atashukuru ama atakufuru, tusiwe miongoni mwa wale watakokufuru, kwani mpaka hapa tulipofikia sehemu njingi sana tulifurahi, chukulia mfano, ulipomaliza form iv ulifaulu ukafurahi, form vi pia nk. Huu ni mtihani mdogo sana, ni muhimu kumwomba mungu aweze kukuvusha kwenye haya mapito. Ni matumaini yangu kuwa mtafanya vyema mtakaporudia.
Mwisho kabisa, naomba nitumie fursa hii  kuwaomba msamaha kwa yeyote  ambaye kwa namna moja ama nyingine nilimkwaza, mimi ni binaadamu kama walivyobinaadamu wengine na sifa ya binaadamu ni mapungufu. Safari ya miaka mitatu ni mingi sana tutakiane kheri katika maisha.
 Nawatakia maafali njema kwa watakaohudhuria.
Asanteni.
Aman Ng'oma


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD