Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kijamii. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kijamii. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 16 Julai 2014

MAISHA NI SAFARI NDEFU, HAKUNA KUKATA TAMAA, KUWA MVUMILIVU SONGA MBELE

Ni mwaka sasa toka nimemaliza shahada yangu ya kwanza ya Uchumi kilimo na Biashara. Shukrani kwa mama yangu Bi Swalati A. Ndimbo kwa  jitihada zake kubwa kwangu kuhakikisha nasoma. Nakumbuka mama yangu alilazimika kuuza kuni wakati huo ili nipate hela ya madaftari. Namshukuru pia Mjomba 'angu Marehemu Balihua A. Ndimbo, kwa kunisomesha toka kidato cha kwanza hadi cha Sita na kunipa upendo wa hali ya juu. Msingi niliojengewa umekuwa Imara kuendeleza  jengo  ambalo kwa sasa, lilipofikia, limeanza kupendwa na hivyo kutumiwa na watu , naamini muda si mrefu jengo hilo litaimarika zaidi na kuwa zuri lenye mvuto maradufu  . Pia nimshukuru Baba 'angu Mzee Titus F. Ng'oma kwa mchango wake kama Baba. Namshukuru Babu yangu mzee Mwenyekheri M. Ndimbo na Mkewa Bi Brenda M. Ndimbo kwa kupita mikononi mwao. Dr Gabagambi, mwalimu wangu wa somo la Utafiti pamoja na Dr. Mkandara mwalimu wangu mlezi wa taaluma, kwa pamoja nawashukuru sana  kwa mchango wao kwangu. Mwisho  nawashukuru Maschool mates wangu wote, nitamtaja mmoja moja kwa niaba kuonyesha shukrani zangu, Primary School, Athuman Kayumba, na Yasini Komba (Shule ya msingi Namtumbo na Shule ya Msingi Mgombasi), O- level (Minaki secondari), Shaibu Rajabu, A- level (Umbwe Secondari) Justin Sanya, Certificate in Animal health and Production, Shaibu Ndimbo na Emanuel Maimbi) chuo cha mifugo Madaba na Morogoro), Diploma in Animal Health(chuo cha mifugo Morogoro), Editha Matembe, Bsc. Agricultural Economics and Agribuiness (SUA), Makando Weight G Force (Sufian Makando), Na kwa upande wa kazini namshukuru Mkurugenzi wangu Bwana Johaness B. Kamonga, Mkurugenzi mtendaji wa Matembwe Village Co Ltd, Njombe, Dr. George J. Mkoma, Mkurugenzi wa Kampuni ya Hisa Micro finance and Community Development, Dr. Boniface Tibaijuka, Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma pamoja na Mama Daina Mnywanga  Mkuu wa Idara ya Kilimo na Umwagiliaji Halimashauri ya wilaya ya Mvomero. Mwisho aliye juu ya wote ni allah aliyenijalia kufika hapa nilipofika. Alhamdulillah!


Allah Is Great

Ijumaa, 30 Mei 2014

KAMERA YETU YAKUTANA ANA KWA ANA NA WADAU HAWA MJINI DODOMA

Kamera yetu ilikutana na  hawa waheshimiwa. Kutoka kushoto ni Rehema Ndimbo,  Haidari Ndimbo katikati na Aman Ng'oma kulia wakiwa Maeneo ya Nyerere square Dodoma.




























Kicheko kikiwa kimekolea kabisa, aliyevaa tshirt Nyekundu ni Juma Ndimbo mwanafunzi wa U-dom mwaka wa tatu.

Ijumaa, 15 Novemba 2013

MAMBO YAMEIVA SASA, TANGAZO LA GRADUATION YA CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE SUA


 SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE

ANNOUNCEMENT

TWENTY NINETH GRADUATION,PRIZE AWARDING CEREMONIES AND CONVOCATION MEETING.

A. GRADUATION CEREMONY:
Graduands and Members of the General Public are hereby informed that the 29th SUA Graduation Ceremony will be held on Friday 29th November, 2013 at Solomon Mahlangu Campus (SMC), “Nelson Mandela Freedom Square”, Mazimbu in Morogoro,
starting at 11:00 hrs. The Chancellor of SUA Hon. Al Noor Kassum will confer degrees and non-degree awards to the 2012/2013 academic year graduands

B. HIRE AND RETURN OF GOWNS:
Also, graduands be informed that hiring fee for a graduation gown is Tshs 30,000/= (non-refundable) and this fee is payable through SUA CRDB Bank Account Number 01J1076769836. Graduands should note that deadline for returning all the hired gowns
to the University shall be Monday the 2nd December 2013, from 8.00 to 18.00 hrs and Tshs 20,000/= per day shall be charged as a penalty for each gown to be returned thereafter.

C. COLLECTION OF GRADUATION GOWNS AND PARTICIPATION IN
REHEARSAL:
Graduation Gowns will be collected by graduands on Wednesday 27thNovember, 2013and Thursday 28nd November, 2013 between 8:00 and 17:00 hrs. Participation in rehearsal for graduands is mandatory and it will be held on the graduation ceremony day
(29th November, 2013) from 08:00 to 9.00 hrs, at the “Nelson Mandela Freedom Square”, SMC Campus. Graduands who will not take part in the rehearsal shall not be allowed to participate at the ceremony, regardless of their presence. Likewise, graduands who have not settled their outstanding fees and other related costs
are being encouraged to settle the debts immediately, through the Account number indicated in item “B” of this announcement. Otherwise, they will not be allowed to graduate before doing so.

D. PRIZE AWARDING CEREMONY:
Continuing students and graduands are also informed that Prize Awarding Ceremony for
those who excelled in various subjects will be held on Thursday 28
th
November, 2013 at
the Council Chamber, Main Campus, from 8:30 to 10.30 hrs. Names of prize awardees will be announced during the second graduation ceremony announcement.

E. CONVOCATION MEETING:
SUA Convocation Members are notified that the Annual General Meeting of the SUA Convocation will be held on Thursday 28nd
November, 2013 at the “Multipurpose Hall,” Main Campus, from 11:00 to 13.00 hrs, immediately after the prize awarding ceremony.

YOU ARE ALL WELCOME

Issued by:-
Office of the Deputy Vice Chancellor (Academic),
Sokoine University of Agriculture,
P.O. Box 3000,
Morogoro
Tel. 023 2604652
Fax: 023 2604652
E-mail dvc@suanet.ac.tz

WAPIGANAJI HAO TOKA 2010 HADI 2013 WALIPOFANIKIWA KUONDOKA KILA MMOJA NA SHAHADA YAKE YA KWANZA YA SAYANSI YA UCHUMI KILIMO NA BIASHARA YA CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE SUA, HONGERENI SASA

Alhamisi, 14 Novemba 2013

NAWAPONGEZA WANAFUNZI WOTE WA CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE SUA KWA KUMALIZA CHUO

Rafiki zangu wote, wanafunzi wenzangu,
Niwajibu wangu kuwashukuruni nyote, kwa ushirikiano ambao mumeuonyesha kwangu. Mafanikio yangu yametokana na michango yenu. Tumetoka mbali na tumepitia misukosuko mingi lakini hatimaye tumemaliza. Hatunabudi kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutufikisha hapa tulipofika. Safari yetu ilianza mwaka 2010, ni safari iliyokuwa chungu sana kwa kuwapoteza baadhi ya ndugu zetu, rafiki zetu na watanzania  wenzetu ambao kwa namna moja ama nyingine walitamani tungemaliza wote mwaka huu, lakini haikuwa mipango ya mungu.
Kila jambo linapotokea lina sababu zake. Tunapaswa kumshukuru mungu kwa mazuri na mabaya tunayoyapata. Hii yote ni mitihani ambayo mungu ametupatia sisi wanaadamu. Ni mitihani ambayo binaadamu inapokupata yakupasa kutulia na kumwomba mungu akurahisishie katika kuitatua bila kuleta athari.
Niwapongeze wote mliofanikiwa kufaulu vyema mitihani yenu, mungu awatimizie ndoto zenu, na mujitahidi kuitumia elimu yenu kuwasaidia watanzania wenzenu wengi ambao hawakubahatika kupata elimu ya chuo kikuu kama ambavyo ninyi mmeipata. Popote mtakapokuwa chapeni kazi kwa bidii ili uwepo wenu uonekane.
Lakini pia si lazima  kuhangaika kutafuta kazi, mnaweza mkawa nyinyi wenyewe chanzo cha kazi kwa wantanzania wenzenu. Mnapaswa kufikiri kijasiriamali hatimaye muweze kuishi katika maisha bora.
Nirudie kuwapa pole ndugu zangu wote ambao matokeo hayakuwa mazuri katika mitihani yenu, naomba mtambue kuwa hii ni mtihani tu ambao mungu humpatia mja wake kama njia ya kumpima namna atavyoupokea mtihani huo, kama  atashukuru ama atakufuru, tusiwe miongoni mwa wale watakokufuru, kwani mpaka hapa tulipofikia sehemu njingi sana tulifurahi, chukulia mfano, ulipomaliza form iv ulifaulu ukafurahi, form vi pia nk. Huu ni mtihani mdogo sana, ni muhimu kumwomba mungu aweze kukuvusha kwenye haya mapito. Ni matumaini yangu kuwa mtafanya vyema mtakaporudia.
Mwisho kabisa, naomba nitumie fursa hii  kuwaomba msamaha kwa yeyote  ambaye kwa namna moja ama nyingine nilimkwaza, mimi ni binaadamu kama walivyobinaadamu wengine na sifa ya binaadamu ni mapungufu. Safari ya miaka mitatu ni mingi sana tutakiane kheri katika maisha.
 Nawatakia maafali njema kwa watakaohudhuria.
Asanteni.
Aman Ng'oma


KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD