Jumapili, 29 Desemba 2013

MTOTO WA MIAKA 11 ANUSURIKA KUUAWA NA MAMBA.

Baba wa familia moja huko nchini Zimbabwe alijikuta akijitosa mtoni  kupambana na Mamba ili kuokoa maisha ya mwanae mwenye umri wa miaka 11 ambae alikamatwa na mamba wakati wanavuka mto Nyaitengwa.
Baba huyo ambae anajulikana kama Mr Tafadzwa Kachere na mwanae Tapiwa walijeruhiwa vibaya na mamba huyo hapo jana na kupelekea wao kulazwa katika hospitali ya Chitungwiza.
Tapiwa alijeruhiwa kiasi cha mguu wake wa kushoto kukatwa, wakati mkono wa kushoto wa Baba yake uliumizwa vibaya, Mr Kachere alisema kuwa mamba huyo aliwashambulia wakati  watoka katika bustani yake kuelekea nyumbani, Mzee huyo aliendelea kusema kuwa walipokuwa wanavuka mto huo kijana wake akiwa nyuma alisikia mwanae akipiga mayowe ya kuomba msaada na ndipo alipoamua kwenda na kupambana na mamba huyo ili aweze kumuokoa mwanae aliyekua anaangaika baada ya kung'atwa mguu wake.

Mzee huyo aliendelea kusema " niliangaika kufungua mdomo wa mamba huyo kwamikono yangu lakini ilishindikana, pamoja na kumchoma choma na mianzi mdomoni lakin ilikuwa ni ngumu mno kumwachia mwanangu na ndipo nilipomchoma mamba huyo na mwanzi machoni nikiwa nimekaa mgongoni mwake na kumwachia mwanangu na yeye kuangaika katika maji na mimi nikambeba mwanagu mgongoni taratibu tukajikokota kutoka nje ya mto.
Baada ya shambulio hilo tulipata msaada wa kwanza katika hospitali ya Nyadire kabla ya kupelekwa hospitali ya kati 'Chitungwiza"SOMA ZAIDI
Mr Kachere ametoa wito wa msaada wa kununua mguu wa bandia kwa ajili ya mwanae. Kachere alisema "Naomba msaada kwa yeyote mwenye uwezo ili ninunue mguu wa mwanangu kwani yeye bado anahitaji kwenda shule na hadi sasa yeye anaamini kuwa mguu wake utarudi.

Si uongo yeye anaamini kuwa mguu wake umeondolewa kwa madhumuni ya matibabu na sijui ni jinsi gani nitamfikishia taarifa ya mguu wake, alimalizia kusema Baba huyo kwa uchungu na kulia.

Hii ni kwababa mwenye upendo wa dhati kufa kwaajili ya mwane  Je ingekuwa wewe ungefanyaje....?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD