Mh.Zitto Kabwe leo ameandika historia kwenye aridhi ya
Kigoma baada ya kupata Mapokezi ambayo wenyeji/wazawa wanadai labda
Nyerere ndio aliyapata mapokezi haya.
Mh.Zitto amerejea leo Kigoma kuzungumza na wananchi wake,wananchi wote
wa Kigoma namna mwenendo wa siasa ndani ya CHADEMA unavyorudisha
utafutaji wa Demokrasia makini ndani ya Nchi hii,Pia namna wanachadema
wenzake wanavyopigilia misumali kwenye mwili wake ilikukwamisha jitihada
zake za kupambana na mafisadi,Kupambana na ujenzi wa Taifa letu.
Mh.Zitto Kabwe amaetua Kigoma mnamo saa 3 na Nusu Asubuhi ambapo
alikutana na Maelfu ya wananchi wakiwa Nje ya uwanja wa Ndege tayari kwa
kumpokea.
Maandamano ya Amani yaliyojumuisha maelfu ya Wanakigoma,kukiwa na
pikipiki zaidi ya 240 na magari ya Watu Binafsi wenye mapenzi ya dhati
kwa zitto zaidi ya 80 yalianza safari ya kutoa Airport kupitia Ofisi za
Mkoa za CHADEMA na hatimaye safari ya kuelekea Kigoma Kaskazini kijiji
cha Mwandinga alipozaliwa Zitto Kabwe kwaajili ya Mkutano wa Hadhara
kuzungumza na wananchi wake.
Maandamano hayo ya Amani/msafara uliochukua zaidi ya masaa 3 kwa
kutembea zaidi ya Kilomita 15 kwa mwendo wa polepole hatimaye ukafika
Mwandinga.
Kwwenye Mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya Wananchi wakitokea
pande zote za Kigoma,Zitto alijikita kwenye mambo Makuu Matatu,Kwanza
kueleza kwanini ameamua kurejea Nyumbani (Kuzungumza na waliompatia
Ubunge),Pili kuzungumzia hali ya Kisasa anayopitia kwa sasa ambapo
amekili yeye bado ni mwanachadema Mtiifu sana,Na anaamini Rufaa yake kwa
Kamati kuu chombo cha juu kabisa cha maamuzi ndani ya chama kitamtendea
haki,kwa sababu tuhuma zote dhidi yake sizakweli,Pia zimelenga
kummaliza kisiasa yeye na wale wanaounga Demokrasia ya kweli ndani ya
CHADEMA.
Zitto anasema atapambana kuhakikisha anapata haki yake,na atakuwa wa Mwisho kuondoka CHADEMA tena kwa hiali yake.
Mwisho kabisa Mh.Zitto amewaahidi wanakigoma kuwa hatafanya maamuzi
yoyote kabla hajarudi tena Nyumbani na kushauriana na wananchi wake.
Amesisitiza kuwa Kigoma ya Leo hii ambayo kila mmoja kwa nafasi yake
anajisifia kuitwa mzawa wa kigoma ni moja ya jitihada zake,Pia yeye
hayupo kwa Msalahi ya CHADEMA tu,Hoja ya Buzwagi ilikuwa ya Kitaifa,Hoja
ya kumuwajibisha waziri Mkuu ilikuwa ya Kitaifa,Lakini hata hii hoja ya
PAC ya kukagua mahesabu ya Vyama vya siasa ni ya Kitaifa,Hivyo hayupo
tayari kuwamnafiki kwa kuitetea CHADEMA kukaguliwa eti kwa sababu yeye
ni Kiongozi ndani ya CHAMA.
Mkutano Umemalizika Salama kabisa,Wananchi wameridhika zaidi na kwa shangwe kwa pamoja wanasema"ZITTO KWANZA,CHADEMA BAADAE"
Picha zaidi hizi hapa chini
Hakuna kurudi nyuma hadi kieleweke
Vijanaaaaaaaaaaa"nguvu ya Mabadiriko"
Msafara unaendelea ukitokea Ofisi za CHADEMA MKOA hapa Kigoma kuelekea Mwandinga kijijini alikzaliwa Zitto kabwe
Siasa ni Vijana na hii ndio Nguvu ya Umma ilivyojitokeza kumpokea ZItto kabwe hii leo hapa Kigoma
Vijana wakiwa wamehamasika vya kutosha sana,hapa wanaimba "Kitimtimu utakiona leo,Kwenye nyumba ya Zitto..Slaa umeingiaje"?
Kwa namna msafara ulivyokuwa mkubwa ilimlazimu kila aliyenyumbani kwake
kukikimbilia barabarani angalau kupungia mkono kwa Mh.Zitto Kabwe
Ulinzi wa wananchi wenyewe umeimarishwa sana,Vijana wamamrinda Mbunge
wao.Kubwa zaidi hakuna askari kwenye msafara huu ni wananchi
wanajiongoza na wapo salama
Zitto Kabwe"Nimerudi nyumbani,Nawasshukuru kwa mapokezi mazuri haya ya Kihistoria hapa Kigoma,Nimerudi Shujaa wenu
Zitto"Asanteni sana,nawapenda sanaa"
Alipokuwa anakaribia kuingia Mwandinga Mh.Zitto kabwe alilazimika kuteremka na kuanza kutembea kuelekea kwenye Mkutano
Msafara bado unaendelea,Wananchi wanasema hakuna kurudi Nyuma mpaka kieleweke
Ni maelfu ya WANANCHI ambao wanatembea kuelekea Mwandinga umbali wa
zaidi ya kilomita 15 kwa miguu huku wakiwa na furaha sana ya kukutana na
Mbunge wao
Msafara wa magari zaidi ya 100 ukitokea Airpot kumpokea Mh.Zitto kabwe
kuelekea Mwandinga,Hapa Shughuli za maendeleo zimesismama kwa muda
wananchi wamejumuika kumsindikiza Zitto Mwandinga kuzumngumza na
wanakigoma
Ni nyomi ambayo haijawahi kutokea hapa Kigoma
Zitto Kabwe anasema"Nimerudi Nyumbani kuzungumza na nyini kaka,dada,baba
na Mama zangu kuhusu maisha yangu ya Kisiasa,Nimerudi Nyumbani
kwasababu ndipo nilipokulia na kuanza maisha,Pia nyie ndio mlionifikisha
hapa".
Picha inajieleza namna wananchi walivyomiminika Mwandinga kumsikiliza Mtoto wao Zitto Kabwe
Huu ni Upande mmoja wa Sehemu ya Mkutano wananchi wakiwa makini
kusikiliza kile Mh.Zitto anaongea kuhusu mwenendo wa Siasa za CHADEMA na
namna atakavyokuwa wamwisho kuondoka CHADEMA kwa hiari yake.
Msafara ukiendelea zaidi ya Kilomita 15 kutoa Airport Kuelekea Mwandinga
Nyumbani alikozaliwa Zitto Kabwe,Wananchi wamejitokeza kwa wingi sana
haijawahi kutokea.
\
Mh.Zitto Kabwe akaihutubia Maelfu ya Wananchi katika viwanja vya
Mandinga,Kubwa amesisitiza ataendelea kudai Demokrasia ya Kweli ndani ya
CHADEMA na inamuuma sana kuona wanaompiga Mishale ni Wanachadema
wenzake.
Maelfu ya Wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano wa Mh.Zitto kabwe hapa
Mwandinga Kijijini kwake alikozaliwa Mkoani Kigoma,Bango linasomeka
"ZITTO KAMA MANDELA KASORO JELA"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni