MBOWE ATIA NENO KAULI YA ZITTO ASEMA KUPEWA PESA NA KIKWETE AU CCM SIYO TATIZO LAKINI UNAPEWA PESA KWA SABABU ZIPI,NA KWA MALENGO GANI
Akizungumza na mwandishi wetu Mbowe alisema ni utoto kukwepa kujibu
hoja kwa kuanzisha tuhuma dhidi ya mtu mwingine ambazo si za kweli.
“Mimi nimekuwa nikisimamia ukweli, mtu anapotuhumiwa ni lazima ajibu
tuhuma hizo. Ni utoto kuacha kujibu tuhuma na kuzusha tuhuma nyingine.
Anapaswa kufanya utetezi wa tuhuma zinazoelekezwa kwake.
“Mimi ni mbunge, bungeni nimekuwa nikichangia watu mbalimbali mimi kama
Freeman, si ajabu watu wengine kunichangia. Hapa jambo la msingi ni
kwamba unapewa pesa kwa sababu gani, kwa nia ipi? Kupewa pesa na Kikwete
au CCM si tatizo lakini unapewa pesa kwa sababu zipi, kwa malengo
gani?” alihoji Mbowe.
Duh kumbe watu wanachukua chapaa!!!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni