"Askari
wa kikoloni", akipewa adhabu ya push up baada ya kuboronga wakati wa
gwaride. Hili lilikuwa igizo lililoendeshwa na askari polisi wakati wa
maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa
michezo Aman mjini Unguja Jumapili Januari 12, 2014.
Kamanda
wa kikosi cha askari KAR, akiongoza wenzake kwenye onyesho la kuiga
lililoendeshwa na askari polisi kuonyesha jinsi jeshi la kikoloni
lilivyokuwa likifanya mambo yake.
Rais
wa Zanzibar, Dkt Ali Mohammed Sheni, akikagua vikosi vya ulinzi kwenye
kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye
uwanja wa michezo Aman mjini Zanzibar Jumapili Januari 12, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni
Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea
miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo
mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote
kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12,
mwaka 1964.
Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na
mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume
yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na
kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine
kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar
yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar –
miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.
Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa
kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50
ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi
kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea
miaka 50 ya Mapinduzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho,
Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public
Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu
ya Zanzibar.
Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo
mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote
kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12,
mwaka 1964.
Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na
mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume
yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na
kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine
kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar
yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar –
miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.
Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa
kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50
ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Shein alitangaza mapumziko
hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan
mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.
Rais
wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Sheni, akimvisha nishani mtangulizi
wake, rais Aman Abeid Karume, ikiwa ni sehemu ya sherehe za Mapinduzi ya
Zanzibar zilizofikia kilele chake Jumapili Januari 12, 2014 kwenye
uwanja wa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni