Alhamisi, 26 Juni 2014

NI LANDMARK HOTEL


Kumekuchaaa Dar es salaam. Ni tarehe 20/09/2014 ndani ya Landmark Hotel, ni semina ya aina yake kuwahi kufanyika. Nitakuwemo katika wale watakao toa mada siku hiyo. Ni fursa pekee kwa wale  wanaofuga na wanaohitaji kuanza kufuga nk. Karibu tukutane tuonyeshane utajiri uliojificha katika ufugaji wa kuku, hakuna haja ya kulalamika. Anza sasa kufuga kuku unufaike Kiuchumi. 


Ni semina ya aina yake kwasababu mambo mengi yatahusika siku hiyo kama ambavyo yamebainishwa kwenye hilo tangazo hapo juu.



Siyo siku ya kukosa siku hiyo. Ni fursa pekee kwa wafugaji  na wadau wa kuku Dar es salaam na maeneo jirani. 

Karibu nyote.




Jumatano, 18 Juni 2014

UFUGAJI WA KUKU NDIO MPANGO MZIMA, HARAKA UNATAJIRISHA

Vifaranga wakiwa bandani. Ndivyo inavyotakiwa waonekane wasiwe wamebanana  au kujikusanya sehemu moja.
 Hapa wamekuwa kidogo ni hatua kwa hatua.
 Hiki ndicho kiwanda cha kutengeneza chakula cha kuku.
 Kazi inaendelea chakula kinatengenezwa na kuchanganywa vyema kiwandani.
Hapa afisa akiwa kazini anawajibiki. Ni Matembwe village company Ltd, Njombe
 Kazi inaendelea hakuna kulala mpaka kuku wapate chakula.
 Hapa vifaranga ndio kwanza wamezaliwa tayari kwa kuwafanyia sexing kuwatenganisha vidume na vijike ili wapelekewe wateja.
Vifaranga bora kabisa Kutoka Matembwe Njombe.


Sexing Inaendelea hapa. Sexing inayofanyika ni ile ya kutumia mabawa

Kazi ni kazi hakuna kulala. Sexing inaendelea.
Afisa akifanya Post mortem ya kuku aliyekufa masaa kama matano hivi toka aaze kuonyesha dalili ya ugonjwa ,   baada ya Post mortem alionekana ana msumali kwenye filigisi au gizzard
Hapa chakula kiko tayari kwa kusambazwa madukani kwa ajili ya kuuzwa na kingine kubakizwa tayari kwa kulishwa kuku wa Kampuni.

TANGAZO LA SEMINA YA WADAU WA TASNIA YA KUKU WA DAR-ES- SALAAM


Habarini wadau,


Still niko humu uwanjani.

Leo nina habari njema kwa waazi wa Dar es salaam. Kuna semina kabambe inaratibiwa  soon nitawapa habari kamili. Mimi pia nitakuwa mjengoni katika wale watakao wasilisha maada siku hiyo. Kaani mkao wa kula ni semina ya siku moja kiingilio ni tsh 20000/=

Kama kweli  wewe ni mfugaji ama unakusudia kuanza ufugaji basi tafadhali usikose siku hiyo. Ukikosa utakuwa umepitwa na mengi. 

Wadau mbalimbali wa kuku watakuwepo siku hiyo, mabenki yanayotoa mikopo kwa wafugaji, wafugaji wakubwa wa kuku waliofanikiwa katika ufugaji wao watatoa ushuhuda  siku hiyo, wanunuzi wa mazao ya kuku, watu wa mahoteli mbalimbali, supermarkets,nk madaktari na watu waliobobezi  katika tasnia ya kuku nk. Watakuwepo pia wazalishaji wa vifaranga, watengenezaji wa vyakula mbalimbali vya kuku, watengenezaji wa Incubators wa ndani ya nchi na wawakilishi wa watengenezaji wa mashine za nje.

Kila kitu utakachohitaji kukifahamu siku hiyo utafahamu. Je wajua ukitaka kuanzisha hatchery hatua gani muhimu za kufuata, nini kinahitajika na wapi uanzie, siku hiyo ni siku muafaka.

Mambo yakikaa sawa tutawajulisha,lini na ukumbi gani semina hiyo itafanyika. Kwa wale watakaohitaji basi tuwasiliane kupitia namba zangu 0767989713, 0715989713 na 0786989713

Kwa pamoja tunaweza kuutokomeza umasikini.

Jumatatu, 9 Juni 2014

UZALENDO NA NIDHAMU KATIKA MATUMIZI YA RASILIMALI ZA UMMA

Kwanini Tanzania masikini. Mimi nadhani viongozi wetu tuliowachagua hawawajibiki vyakutosha kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu. Wanapenda kuishi maisha ya anasa kana kwamba Tanzania na Watanzania ni Matajiri. 

Wanasiasa pia wanalifilisi taifa hili. Ebu fikiria kuna ulazima gani wa mbunge mmoja kulipwa tsh 300000/= kwa siku ili hali nchi yetu ni masikini. Kuna ulazima gani wa kununua magari ya kifahari ya shilingi milioni 200 ili hali watanzania wezetu wanakufa kwa njaa, wanafunzi hawana madawati ya kukalia, walimu wanalalamika maslahi madogo, madaktari nao pia.

Ningekuwa Rais ningeagiza viongozi wote wa serikali watumie tax gari zinazoendana na uwezo wetu. Wabunge wa bunge la katiba na bunge la bajeti ningewalipa tsh elfu 85 tu kwa siku kama wafanyakazi wengine wanapoenda kufanya kazi nje ya mkoa wake.

Ili tuendelee lazima tukubali kuishi kwa ubahiri na mikati mikubwa ya kuhakikisha kuwa Tanzania na Watanzania tunawakomboa kutoka kwenye lindi la umasikini.

Tujenge miundo mbinu itakayo rahisisha kuchumi wetu upae.

Hakuna faida ya kwenda kuficha nje mabilioni ya pesa ili hali watanzania wenzako wanakufa njaa hapa nchini kwako.

Tujifunze kuhurumiana. Kwa pamoja tunaweza kutokomeza lindi la umaskini katika nchi yetu 

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD