Jumapili, 28 Septemba 2014

TAREHE MPYA YA SEMINA YA UFUGAJI BORA WA KUKU SONGEA NA DAR ES SALAAM


Kutokana na sebabu zilizo nje ya uwezo wetu, ile Semina ya ufugaji bora wa kuku sasa kufanyika tarehe 01/11/2014 badala ya kuhairishwa tarehe 27/09/2014, tunaomba radhi kwa usumbu uliojitokeza.


Kwa taarifa kamali pitia tangazo hilo hapo chini au piga 0767989713/0715989713 au kwa mratibu wa semina hiyo kwa namba 0655663900


Click image for larger version. 

Name: IMG-20140926-WA0000.jpg 
Views: 0 
Size: 242.1 KB 
ID: 188785

Tarehe 11/10/2014, kutakuwa na semina kama hiyo Songea katika ukumbi wa Familia Takatifu Bombambili, tiketi zinapatikana kwa bwana Siphael Mgeni, wakala maarufu wa kusambaza vifaranga wa kuku mkoani Ruvuma anapatikana mtaa wa Zanzibar jengo la CCM, au waweza mpigia kwa simu namba 0717705614 au 0684812938.

Kwa ufugaji wenye tija, unakaribishwa katika semina
Tangozo hilo hapo chini ni kwa ajili ya semina ya Songea. Hii ni fursa pekee wala si ya kuikosa, njoo kama una jambo lolote linakutakutatiza katika ufugaji wa kuku utapata ufumbuzi siku hiyo, kwa hakika tumejipanga kuwahudumia watanzania.

Click image for larger version. 

Name: SONGEA.jpg 
Views: 0 
Size: 228.2 KB 
ID: 188789





Jumamosi, 27 Septemba 2014

KALI YA MWAKA, MTENDAJI NAMTUMBO AKUTANA ANA KWA ANA NA JENEZA MLANGONI KWAKE, AFUNGA MLANGO NA KURUDI NDANI HUKU AKILIA MACHOZI KAMA MTU ALIYEFIWA

Ni katika hali isiyo ya kawaida, mtendaji wa kata ya Kitanda wilayani Namtumbo Bwana Fidea Mbawala amekuta jeneza likiwa limefunikwa vizuri kana kwamba kuna maiti ambayo inahitajika kwenda kuzikwa hivi punde. Tukio hilo limetokea katika kijiji cha kitanda ambapo watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo walimwekea jeneza hilo mlangoni kwake kwa sababu ambazo bado hazijaweza kufahamika.

Taarifa zaidi zinadai kuwa mtendaji huyo alipoamka asubuhi na kutoka nje ndipo alipokutana na jeneza hilo mlangoni  baada ya kufungua mlango mkubwa wa nje. Bwana Mbawala alipoona jeneza hilo alishituka huku akioneka mwenye huzuni iliyoambata na uwoga.

Bwana mbawala hakuweza tena kutoka nje, ilibidi afunge mlango na kuingia tena ndani huku akiwa analia kwa simanzi kama mtu aliyefiwa. Ilibidi apige simu polisi kwa ajili ya kutoa taarifa.

Tukio hilo limevuta hisia watu wengi kwani halijawahi kutokea kijijini hapo. Baada ya watu kuwasili walimtoa mlango wa pili huku ule mlango wenye jeneza ukibaki umefungwa na jeneza kuendelea kubaki kama lilivyo pale mlangoni huku umati mkubwa wa watu ukiwa umejaa nyumbani kwa mtendaji huyo.

Awali mkuu wa wilaya ya Namtumbo aliagiza watendaji wakusanye michango kwa wananchi kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari ya kata ya Kitanda ijulikanayo kwa jina la Mkomanile, na akamwagiza dawani wa kati hiyo Bwana Titus Fedinand Ng'oma na  Mtendaji wake  bwana  Mbawala wahamasishe watu katika utoaji wa michango hiyo na kwamba yeyote asiyetoa michango hiyo akamapatwe mara moja.

Uhamasishaji ulifanyika lakini mwitikio ulikuwa mdogo na mtendaji hakuweza kuwakamata watu walioshindwa kutoa michango hiyo.

Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ya Namtumbo alimwagiza diwani wa kata hiyo Bwana Ng'oma  pamoja mtendaji wake bwana Mbawala wakamatwe na wapelekwe polisi kwa kupuuza agizo lake. Mnamo  tarehe 24/09/201, diwani na mtendaji walikamatwa na kufikishwa polisi. Baada ya maelezo diwani aliachichiwa akiambiwa arudi siku ya pili kwa mahojiano zaidi huku mtendaji wa kata akiendelea kushikiliwa na polisi ingawa badae waliachiwa na kutakiwa kwenda kukusanya michango hiyo na kwamba atakaye kataa akamatwe mara moja. Baada ya kuwatangazia wanachi walipe michango hiyo na kwamba asiyelipa atakamatwa na kufikishwa mahakamani, ndipo mtendaji akakumbana na zahama hili.

Wadadisi wanalihusisha tukio hilo na michango iyoendelea kukusanywa na kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari ya kata ya kitanda ya Mkomanile, na kwa kufanya hivyo ni kujaribu kumtisha mtendaji huyo ili aogope kuwachangisha pesa wananchi hao.      

Jumapili, 7 Septemba 2014

WILL THE BAVAR 373 BRING THE END OF THE AMERICAN EMPIRES?

As short-lived as it may prove to be, the American empire could well meet its match in Iran and by way of that country’s air defences.
Iran’s own advanced long-range air defence system is still under development but if it’s all it’s claimed to be it could ultimately prove to be the weapon that spells the end of America’s imperial designs.
Work on the Bavar 373 (Belief 373) began when problems arose with the delivery of Russia’s S-300 system. Although the S-300 deal was originally signed in 2007, Russia failed to deliver the system and finally cancelled the sale in 2010, following pressure from the U.S. and Israel.

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD