BWANA UWEZO NYATIGE, ANAULIZA
"Habari za majukumu.
Nimesoma ushauri wenu juu ya ufugaji mtandaoni mbarikiwe kwa hilo.
Nimevutiwa na mradi wa utotoleshaji wa vifaranga. nina changamoto moja sijui mtanisaidiaje.
Nimesoma ushauri wenu juu ya ufugaji mtandaoni mbarikiwe kwa hilo.
Nimevutiwa na mradi wa utotoleshaji wa vifaranga. nina changamoto moja sijui mtanisaidiaje.
Mimi ni mkazi wa Dar es salaam wakati nyie mko Dododma.
1. Je mna watu wenye mayai hayo hapa Dar es salaam ili nikianza mradi niwe na uhakika wa mayai hayo bora ya kuku wa kienyeji walioboreshwa?
2. Je nitakapototolesha mayai hayo, vifaranga ni lazima nivilete Dodoma ili kuwauzia hao Ma Agent au mnao pia Dar wanaochukua vifaranga kwa uhakika?
Nina nia ya kujikomboa kiuchumi. naomba unisaidie hayo ili niweze kufanya maamuzi ikiwa pamoja na kujipanga kuja Dododoma kwa ajili ya Semina maalum juu ya hilo kabla sijaanza mradi.
Nashukuru kwa ushirikiano wako.
Ahsante".
Nashukuru kwa ushirikiano wako.
Ahsante".
MAJIBU KUTOKA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD
Bwana Uwezo Nyatige,
Awali ya yote nikushukuru kwa baraka zako kwetu lakini pili nikupongeze kwa kuwa mfuatiliaji wa mada zetu za ufugaji kupitia mitandao. Nakuhaidi kuendelea kutoa mafunzo kama hayo katika mitandao mbalimbali ya kijamii ili yaweze kuwa msaada na mwongozo kwako na kwa watu wengine pia katika uendeshaji wa miradi ya ufugaji kibiashara. Utakapoona wakati mwingine tuko kimya kwa muda isikupe hofu sisi tupo, ni kutingwa tu kidogo na majukumu ya hapa na pale lakini napenda nikuhakikishie kuwa Kinasoru East Africa Tanzania Ltd daima iko pamoja na wakulima na wafugaji kwa ujumla wake.
Naomba nianze kukujibu kwa kukuondoa shaka kuhusu umbali uliyopo baina yetu kwa maana Dodoma na DSM. Kimsingi umbali huo siyo kikwazo kitakachokufanya ushindwe kuanzisha mradi wako. Kampuni yetu inawataalamu waliyobobea katika fani hiyo na kwamba wataweza kukushauri kwa njia mbalimbali ikiwemo njia ya simu na kukutembelea huko Dar es salaam kwa mwaliko wako na baada ya kukushauri tutakupatia vitabu vya mwongozo vitakavyokusaidia kukuongoza. Vile vile Dar es saalam ni miongoni mwa mikoa iliyo na wateja wetu wengi kabisa na wote tunawashauri kwa njia ya simu na inapopatikana safari ya kuja huko tunaitumia fursa hiyo pia kuwatembelea na wateja wetu wengine. Mradi kama huo unaoutaka kuufanya tumeweza kuwaanzishia weteja wetu wengine kadhaa kuwataja japo wachache mmoja yupo Morogoro na Mwingine yuko Mwanza maeneo ya Nyasaka na wote hatchery zao zinafanyakazi vizuri sana. Ukiangalia Mwanza ni mbali kuliko Dsm lakini tumeweza kumwongoza hadi sasa na maendeleo yake ni mazuri.
Kinasoru East Africa Tanzania LTD haina vyanzo vya uhakika vya kukusanya mayai mazuri yanayofaa kwa shughuli ya utotoleshaji kwa mkoa wa Dar es salaam. Mfumo wetu wa kupata mayai ni kwa kuwatumia wafugaji tuliyowapa elimu maalum ya ufugaji wa kuku wazazi wenye kutaga mayai yanayofaa kuatamishwa na hatimae kutotolewa vifaranga. Wafugaji hawa tunawaita outgrowers. Tumewafundisha sifa za mayai yanayotakiwa kutotoleshwa yanatakiwa yaweje na namna gani yataweza kutuzwa. Pia wafugaji hao tunawafuatilia hatua kwa hautua kuona kama kweli wanazingatia mafunzo tuliyowapatia. Kwa sasa tuna outgrowers Morogoro mjini, Dakawa na Dodoma mjini. Na mtu yoyote anayehitaji mayai kutoka sehemu yoyote ya nchi yetu , tutamtumia kutoka Dodoma kwani Dodoma ndiyo kituo kikuu cha kukusanya mayai na kuyatuma kwa wateja wetu mbalimbali. Kwasababu mayai yetu yanatoka kwa wafugaji wetu mablimbali, na ili kudhibiti ubora wake kila mfugaji tumempatia namba na kwamba namba hiyo tunakuwa tumeiandika katika kila yai lililoletwa na mfugaji husika. Na ikitokea mayai hayajatotolewa na ikathibitika kuwa kutototolewa huko kwa mayai kunatokana na mayai yetu basi tunachukua jukumu la kumfidia mteja wetu, tunachofanya ni kukuuliza tu ni mayai namba ngapi au yenye alama gani ambayo hayakuweza kutotolewa ili tuweze kumtafuta mhusika wa mayai hayo. Kupitia namba hizo tutambaini mfugaji mwenye hayo mayai na hatimaye mfugaji huyo atalazimika kufidia mayai mengine kinyume cha hapo tutamwondoa katika mfumo wetu wa masoko. Wafugaji waaminifu peke yao ndiyo tunaowahitaji. Tunashukuru kupitia mfumo huu wafugaji wetu wamekuwa waelewa na waaminifu sana. Mayai wanayotuletea yamekuwa yakikidhi haja yetu. Wateja wetu wanaoagiza mayai hayo wamekuwa wakiyafurahia kwa namna yanavyototolewa vizuri lakini vilevile ule mfumo wetu wa kufidia tunaoutumia pale inapotokea mayai yameleta shida.
Utakapo totolesha mayai hayo vifaranga siyo lazima utulete Dodoma. Kazi ya Kinasoru East Africa Tanzania Ltd ni kuwaunganisha wafugaji na wateja au watotoleshaji na wateja. Tunachokifanya sisi ni kukutafutia soko la karibu yako hukohuko Dsm na ikishindikana tutakutafutia masoko katika mikoa ya jirani na mkoa wako. Lakini vilevile unapaswa kutambua kuwa Kinasoru East Africa Tanzania Ltd inakupa uhuru wewe mfugaji wa kuchagua kama ikitokea umepata soko lako la uhakika uweze kuuza bila sisi kukuingilia. Hivi ndivyo tunavyofanya kazi zetu. Siku zote lengo letu ni kumwona mkulima na mfugaji anafanya shughuli zake kibiashara ili tija ya kazi yake iweze kuonekana. Na kama kote huko itashindikana basi tutakutafutia soko Dodoma kwa wafugaji wetu na maeneo mengine ya nchi na hapa sisi tutaongeza asilimia kidogo ya gharama kutoka kwenye bei yako ili nasi tuonekana kuna shughuli tunaifanya na ndipo hapo tunapogeuka na kuwa wakala wako. Lengo letu ni kuwa hatutaki mfugaji ahangaike mwenyewe kutafuta masoko mara uzalishaji unapoanza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni