Najaribu kuwaza kwa herufi kubwa. Nchi yetu ya Tanzania ni kubwa sana. Kwa ukubwa wake simaanishi kuwa igawanywe na kuwa nchi mbili kama ilivyo kwa nchi ya Sudan ilivyotengeneza nchi mbili , Sudan Kusini kwa Bwana Salva kir na Sudani ya Kaskazini kwa Bwana Omary Al bashir. Ninachowaza ni ule umbali wa kutoka pande moja ya nchi hadi nyingine kwa mfano kutoka Dsm hadi Mwanza, Sumbawanga hadi Dsm au Bukoba hadi Dsm au Kigoma hadi Dsm. Vilevile natazama tena umbali kutoka Mbeya hadi Mwanza, au Mbeya hadi Arusha ama kutoka Songea hadi Arusha. Ukiangalia route zote hizo ni ndefu. Unahitaji siku moja hadi mbili kufika mahali husika.
Barabara zinazounganisha nchi kwa asilimia kubwa ni barabara zuri na zenye kupitika kwa takribani mwaka mzima. Ni barabara zenye kiwango cha lami kwa asilimia kubwa. Biashara zinafanyika vizuri baina eneo moja la nchi na jingine. Tatizo langu ni muda ambao tunautumia kusafiri kwa njia ya basi kutoka eneo moja hadi jingine. Bila shaka kila mtu atakubaliana na mimi kuwa
tunapoteza muda nwingi sana kwenye safari. Kwa mfano mtu anayesafiri toka Songea hadi Dodoma anatumia takribani saa kumi na tatu. Toka saa kumi na mbili asubuhi hadi saa moja jioni. Mtu anakuwa amekaa tu bure bila kufanya kazi yoyote. Ni mwendo wa kutazama mbuga mbalimbali, milima, Mabonde, mito na Mabwawa. Hali hii inakwenda sambamba na abiria wengine wanaotoka mikoa mbalimbali.
Kazi kubwa inakuwa ni kupiga usingizi mwanzo wa safari hadi mwisho. Ama sivyo labda upate mtu ambaye utaweza kupiga nae stori kadhaa wa kadhaa kubadilishana nae mawazo ili kuondoa uchovu wa safari, Lasivyo utaishia kukaa tu kwenye basi na kumtazama dereva akifanya yake.
Tanzania kuna mabasi zaidi ya 400 yanayotoka kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo kuelekea mikoa mbalimbali na nje ya mipaka yetu na kuingia Ubungo. Kila basi tuseme labda lina uwezo wa kubeba abiria 55 kwa wastani. Idadi hiyo ya abilia ukizidisha na idadi ya mabasi 400 unapata abilia 22, 000 . Abilia hao watapoteza takribani siku moja hadi mbili kutegemeana na umbali, wote hawa hawazalishi. Je ni hasara kiasi gani kama taifa linapata kwa watu hao ambao ni nguvu kazi kwa kutoshiriki kwao katika shughuli za uzalishaji? Hapa tunawaondoa abilia wote wanaosafiri kibiashara ambao idadi yao ni ndogo kwa kuwa wafanyabiashara wengi wanapenda kubana matumizi na hivyo hupanda malori.
Siku moja nilijaribu kuwaza hivi haiwezekani au hakuna matajiri katika biashara ya usafirishaji wa abilia wakaoda mabasi yenye meza na sehemu ya umeme ambapo mtu ataweza kuweka computor yake kama ni mwanafunzi akapata fursa ya kusoma njia nzima badala ya kukaa tu kama mzigo, au kwa waandishi wa habari, vitabu au walimu wakaweza kuanda kazi zao huku wakiwa safarini? Kwa hali ilivyo sasa ukiwa mwanafunzi au katika kada ya ualimu au habari huwezi kufanya kazi yoyote ukiwa safirini. Muda wote utapotea bure bila kufaya shughuli ya uzalishaji mali. Kwa nini serikali isiharakishe mchakato wa kujenga njia za treni za umeme ili zipunguze mwendo tunaoutumia tukiwa safarini?
Naamini akitokea mfanyabiashara wa abilia akaliona hili na akaitumia kama fursa itamtoa. Hata akiamua nauli iongezwa bado watu watapanda tu kwa kuwa watu wanangalia faida inayopatikana ndani yake.
Aman Ng'oma
Mkurugenzi Mtendaji
Kinasoru East Africa Tanzania Ltd
0767989713
Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni