Alhamisi, 28 Aprili 2016

UFUGAJI WA KIBIASHARA


Kwa kawaida incubator inayochukua mayai 5500, full capacity yake ni mayai 16500. Mashine kama hiyo hupaswi kujaza mayai yote kwa kuwa mfumo wa mashine za kutotolea vifaranga unavyotengenezwa si kwa ajili ya kujaza mayai at its full capacity. Kwanini, kwa sababu ukijaza mayai kadiri ya uwezo wa mashine, maana yake ni kuwa utatakiwa ukaa siku 21 za kusubiri mayai uliyoyaingiza katika mashine hiyo hadi yatotolewe.
Na kwa kawaida mayai yanayofaa kutotoleshwa yanapaswa yasizidi siku kumi toka mayai hayo yatagwe lakini inafaa zaidi yawe yaliyotagwa ndani ya siku saba na siku ya nane yaingizwe katika mashine kwa ajili ya kuanza kuatamishwa. Mayai yaliyokusanywa ndani ya siku saba na siku ya nane yakaingizwa katika mashine yanakuwa na ufanisi mkubwa katika kutotolewa. Kwahiyo kama ukisema ujaze mayai mashine yako yote maana yake ni kwamba utapoteza mayai yatakayotagwa kabla ya siku 21 wakati ukisubiri mayai ya mwanzo yaweze kutotolewa.
Kwa msingi huo machine nyingi zimetengezwa katika mfumo ambao, kama uwezo wa mashine ni kuingiza mayai 3186 hatcher yake itaingiza mayai 1062. Hii inakufanya kila wiki uwe unaingiza mayai. Na kama kila wiki utakuwa ukiingiza mayai maana yake kuwa kila wiki utakuwa ukizalisha vifaranga. Mfumo huu hauruhusu kupoteza mayai, mayai yote yatakayokuwa yakitagwa yataingizwa katika mashine.
Mayai ya kuatamishwa hukaa siku 21 toka siku ya kwanza kuatamishwa hadi kupata vifaranga.
Kinasoru East Africa (T) Ltd

Ijumaa, 22 Aprili 2016

BIASHARA YA UTOTORESHAJI WA VIFARANGA WALIOBORESHWA AU WA ASILI INALIPA, JARIBU

Kampuni yetu ya KINASORU EAST AFRICA (T) LTD iliitwa kwa ajili ya kumshauri mheshimiwa mmoja ambaye alikuwa na wazo la kufuga kuku wa asili walioboreshwa kama sehemu ya kazi yake ya ziada. Alitaka apate mwongozo wa kitaalam namna gani anaweza kutengeneza pesa kupitia ufugaji wa kuku hao.
Kitu cha kwanza tulimuuliza, anashilingi ngapi kama mtaji alioandaa kwa ajili ya mradi wake. Mheshiwa akasema ana Milioni 50. Tukamwambia tunatambua unapenda sana kufuga lakini kwasababu umetuita, tunaomba tukushauri. Badala ya kufuga anzisha mradi wa utotoleshaji wa vifaranga walioboreshwa. Badala ya kufikiria kuuza kuku chotara kama wa nyama baada ya miezi 3 au 4 au mayai mara baada ya kuanza kutaga, utakuwa ukiuza vifaranga.
Akauliza kwa hiyo itabidi nianze kufuga kuku hao kama wazazi ili wanipatie mayai nitakayotumia kwa ajili ya kuatamisha ili kuzalisha vifaranga hao kisha niwauze?
Kampuni yetu ikamwambia hapana. Utotoleshaji wa vifaranga na ufugaji wa kuku wa asili walioboreshwa ni vitu viwili tofauti. Ni miradi miwili inayojitegemea. Tukamwambia, Ukitaka ufanikiwe katika mradi wako kwanza shika mradi mmoja ili umudu kuusimamia vyema.
Wapi nitayapata mayai bora yenye mbegu ya kuweza kuendesha mradi huo. Tukamwambia kampuni yetu ina wafugaji wa kutosha wa kuku wa asili walioboreshwa ambao tunawaita kama outgrowers. Tunawauzia vifaranga kisha tunawasaidia kwenye huduma za ugani pale kuku wanapokuwa wanaumwa au chakula pale wanapokosa pesa. Wafugaji wakituita tunaitika haraka kutoa msaada wetu wa kila hali na kuku wakianza kutaga wanatuletea mayai hayo ofisini kwetu na sisi tuwauzia wateja wetu wanaozalisha vifaranga . Kwa mantiki hiyo tukamwambia mayai kwa ajili ya mradi wake wa utotoleshaji wa vifaranga kampuni yetu itamuuzia.
Kampuni yetu inauza tray moja la mayai ya kuku wa asili walioboreshwa kwa shilingi 17,000. Ni mayai ya uhakika yanayotoka kwenye vyanzo salama.
Tukamwelekeza anunue mashine mbili moja hatcher na nyingine ni setter zenye uwezo wa kuingiza mayai 5500 kwa wiki. Bei za mashine hizo zote mbili ni shilingi milioni 25.
Kwa kawaida mashine ya kutotolea vifaranga ina sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni ile sehemu ya kuatamishia mayai na sehemu hiyo tunaiita setter na sehemu ya pili ni ile ya kutotoleshea vifaranga tunaiita hatcher. Kuna mashine zingine Setter na hatcher zote ziko kwenye mashine moja ambapo setter inakuwa juu na hatcher inakuwa chini na wakati nyingine huwa kwenye mashine 2 tofauti kama tulivyokwisha kubainisha hapo awali.
Uwezo wa utotoaji wa mashine hizo ni asiliamia 96. Maana yake ni kwamba kama kila wiki mayai 5500 yatakuwa yanaingizwa katika mashine na mayai yakawa mazuri kwa maana yametoka kwenye kuku wazazi waliotuzwa vyema, maana yake ni kuwa katika mayai 5500 yatakayoingizwa katika mashine, mayai 5280 yataanguliwa na kutoa vifaranga.
Kwa sababu wewe unakuwa mzalishaji, basi utauza kila kifaranga mmoja kwa shilingi 1700 kwa maagent au wafugaji binafsi wanaokuja shambani kununua au kufuata vifaranga hao. Na maagent, wao watapanga bei zao ili nao wapate faida.
Wewe mzalishaji umezalisha na kila kifaranga ukakiuza kwa shilingi 1700, kwa vifaranga 5280 maana yake utaingiza tsh 8,976,000/= kwa wiki na kwa mwezi utakuwa na shilingi 35,904,000. Kama wiki moja mashine inaingiza mayai 5500, kwa mwezi mzima utahitaji mayai tray 22000 sawa na tray 733 kila tray ni tsh 17,000/= ukizidisha hapo utapata tsh 12,461,000 kama gharama za ununuzi wa mayai ya mbegu ya kuku asili walioboreshwa. Mshahara wako kwa mwezi tsh 1,200,000/=, Mshahara wa hatchery attendant 700,000/=, gharama ya umeme kwa mwezi ni tsh 500,000/=, Maji tsh 150,000/= usafari tsh 400,000/=. Jumla ya gharama zote kwa mwezi itakuwaa tsh 15,411,000/=. Ukichukua mauzo yote ukatoa gharama utajikuta unabaki na tsh 20,493,000/= kama faida sawa na tsh 5,123,250 kwa wiki.
Baada ya kumpigia hesabu hizo alikubaliana na wazo letu na akanunua mashine na kuanza rasmi mradi wake wa utotoleshaji wa vifaranga.
Sasa hivi anaiona faida ya kuzalisha vifaranga na sisi tumebaki kama watoaji wa mayai ya kuku wa asili walioboreshwa kwa ajili ya Biashara yake. Kwa kushika kazi moja unapunguza maumivu ya kichwa kuwahangaikia kuku mara waumwe mara utagaji usiwe mzuri kutokana na matunzo na mambo mengine.
NB: Mashine za kutotolea vifaranga zinaitwa Incubators.
Kwa mahitaji ya mayai ya kuku asili walioboreshwe na ushauri wa miradi ya ufugaji, Biashara, Masoko na Mitaji usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0767989713, 0786989713 na 0715989713.
KINASORU EAST AFRICA (T) LTD

Ijumaa, 18 Desemba 2015

UFUGAJI WA KIBIASHARA WA KUKU

Kuku anayetaga mmoja kwa siku anakula wastani wa gram 123. Kwahiyo kwa mfano ukiwa na kuku 1000 kwa siku utahitaji kilo 123 ambazo ni karibia sawa na mifuko 2.5 ambapo kila mfuko mmoja ukiwa na Kilo 50. Na kama utakuwa na kuku 100 watahitaji kilo 12.3 kwa siku.

Wastani kilo moja kwa sasa kwa chakula kile Super ambacho kinauzwa tsh 55,000/= kwa mfuko ni tsh 1100 kwa kilo moja kwahiyo kwa kuku 1000 ambao wanakula kilo 123 kwa siku utahitaji sh 135,300 kwa siku. Kwa hiyo ili uweze kupata faida inatakiwa kuku wako utagaji uanzie 60% ambapo utakuwa na uwezo wa kutengeneza faida ya kama Tsh 34,700/= kwa siku. Kama utagaji utakuwa zaidi ya 80% faida itakuwa kubwa zaidi. Bei ya mayai kwa sasa hivi kwa jumla ni kati ya Tshs 8,500/= na 9000/= kwa tray.

Kuku kukosa madini ya chuma Calcium huwafanya waanzishe tabia mbaya ya kudonoana wao kwa wao na mwingine kula mayai yao. Lakini sababu nyingine za kudonoana ni pamoja na mrundikano wa kuku katika nafasi ndogo ya banda, vilevile mwanga mkali, upungufu wa madini kama hayo ya chuma,na pia kukosekana kwa mabox ya kutagia ambako hufanya kuku watage chini na kusababisha wenzao wawadonee pale wanapotaga.

Nini kifanyike, hakikisha kuku wanakaa kwa nafasi iliyoshauriwa kitaalam, pia wawekewe bembea zitakazikuwa zikiwashughulisha na michezi, pia wakati wa mchana wawekewe mboga mboga za majani mfano mchicha, chinese au majani yoyote yayopendelewa na kuku hao kuyatumia mfano Lusina nk. Vile vile chakula kiwe na chokaa pamoja na dcp ya kutosha. Lakini njia zote hizo zikishindikana basi kuku wakatwe midomo mara moja. Na mdomo tunaokata ni ule wa juu kwababu ndiyo unaotumkika kwa ajili kudonolea wenzake. Mdomo wa chini hutumika kwa ajili ya kulia chakula hivyo ukikata yote miwili utamuathiri katika ulaji wake kitu ambacho kitampa mshituko na kama ni watakaji watashusha ghafla utagaji wao.

YOUTUBE ON UFUGAJI WA BIASHARA

 Here are youtube clips explaining in Kiswahili  about Ufugaji wa Kibiashara meaning keeping livestock commercially. The aim of this clips is just to provide skills and Practices management  on how to keep livestock particularly poultry on commercial basis.
https://www.youtube.com/watch?v=mOD0L0TzwyY

Jumatano, 16 Desemba 2015

GOOD POULTRY HOUSES DISIGNED

The farmer needs poultry shed that could enable him/her raising smoothly the poultry. The better poultry houses lead to Good performance of the poultry flock. The preferable houses should be constructed by following clearly the guidance from the poultry specialist since the structures differs from one are to another.

The poultry structure from hot environment like all coastal Regions like Dar es salaam, Tanga, Pwani, Lindi and Mtwara must be raised its wall only three course from the foundation then followed by openness/ window  covered by poultry wires. These kinds of houses allow good circulation of ventilation which make poultry live healthily.

                                                                                        
But in cold weather areas like Njombe, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro and Arusha the poultry house should be raised seven course from the foundation of the before put the window covered by poultry wire.



Ijumaa, 13 Februari 2015

MABANDA MBALIMBALI YA KUKU

Ufugaji wa kuku unahitaji mabanda bora. Mabanda bora ni yale yaliyojengwa kwa vipimo sahihi na kufuata mwongozo wa mtaalam wa mifugo. Yanatakiwa yawe yanaruhusu hewa ya kutosha kupita. Vile vile yawe na kimo cha mita 



Alhamisi, 5 Februari 2015

TUNAUZA KUKU WA NYAMA WA KIENYEJI KWA BEI NAFUU KABISA

Kwa watu wenye Hotel, Cafteria, Supermarket, shughuli za kijamii mfano Harusi, Misiba, Vipaimara, Maulidi, Chrismass, Idd nk, hii ni habari njema kwenu. Tunauza kuku kwa Idadi yoyote unayoitaka. Karibu bei zetu zinaanzia Tsh elfu 9, 10 na 11 kwa bei za jumla


Soma zaidi........

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD