Jumanne, 31 Desemba 2013

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ALIPOWAAPISHA MKUU MPYA WA POLISI NA NAIBU WAKE LEO LIVE IKULU

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki pamoja na IGP mstaafu Afande Saidi Mwema katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. PICHA NA IKULU

TUNAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA

AUSTRALIA YAWA NCHI YA KWANZA KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA 2014

Sehemu ya sherehe za mwaka mpya 2014,Sydney,Australia

Maelfu ya watu duniani wanajiandaa na sherehe za kuupokea mwaka mpya wa 2014, huku katika mji wa Sydney nchini Australia wakiwa tayari wamekwisha upokea mwaka mpya wa 2014 kuliko maeneo mengine yote duniani na sherehe za kijadi zinaendelea kwa ajili ya sherehe hizo.

Nchini Japan ambao nao tayari wamekwishaupokea mwaka huu saa mbili nyuma ya Australia, hivi sasa viongozi dini ya kijadi ya Shinto wamekusanyika katika mahekalu ya dini hiyo kwa ajili ya sherehe za mwaka mpya.
Miji mingine pia duniani inatarajia kuupokea mwaka mpya kwa sherehe kubwa ambapo katika mji wa Dubai, Falme za Kiarabu wanatarajia kuvunja rekodi kwani sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja katika mitandao ambapo pia miale ya milipuko ya fataki inatarajiwa kwenda hewani umbali wa kilomita 48.

Nchini China sherehe zikitarajiwa kufanyika katika miji yake iliyo mingi, lakini katika mji wa Wuhan wamesitisha harakati za sherehe hizo ili kuepusha uchafuzi wa mji.
Hata hivyo katika miji mingine ya nchi za Ulaya sherehe kubwa zitafanyika pia katika miji mbalimbali ikiwemo, Moscow, Paris na London.

Nchini Afrika Kusini maandalizi yamefanyika ili kuwa na tamasha la wazi maalumu kwa ajili ya kumuenzi kiongozi wa taifa hilo, Hayati Nelson Mandela aliyefariki dunia Desemba 5 mwaka 2013.

Katika mji wa New York wao wataukaribisha mwaka mpya kwa utamaduni wao wa milio ya saa kwa kuhesabu muda uliobaki pamoja na midundo ya mpira. Na katika mji wa Rio de Janeiro nchini Brazil kwa mara nyingine watu zaidi ya milioni mbili watakusanyika katika ufukwe wa Bahari wa Copa Cabana.

Katika nchi za Afrika Mashariki, maandalizi yanaendelea kwa waumini wa dini mbalimbali kwenda katika nyumba za ibada, kumshukuru Mungu kwa kuwawezesha kumaliza mwaka 2013 na kuupokea mwaka mpya wa 2014.

Source BBC

Jumatatu, 30 Desemba 2013

BREAKING NEWS! MRITHI WA NAFASI YA IGP SAID MWEMA NI ERNEST MANGU, ATAAPISHWA KESHO

Ernest Mangu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua

nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.

Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence)katika Jeshi hilo la Polisi.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).

Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

HILI BASI JIPYA LA AZAM NI KIBOKO...KILA KITI KINA TV, CHOO NDANI, FRIJI, YANI NI BALAAA

Hakuna Afrika nzima; Basi jipya la wachezaji wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam, lililowasili nchini juzi likiwa tayari kusafirishwa visiwani Zanzibar ambako timu hiyo imekwenda kushiriki Kombe la Mapinduzi. Hili ni aina ya mabasi ambayo yanatumiwa na klabu za Ulaya kama Manchester United, Bayen Munich na Barcelona ambalo kwa Afrika Azam inaweza kuwa klabu ya kwanza kulimiliki.
Kitu cha maana
Kila siti ina TV
Kuna friji

RAIS KIKWETE AKUTANA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani 24/12/2013.
 
Bwana Ban Ki Moon alimwalika Rais Kikwete ambapo viongozi hao wawili walijadili masuala mbalimbali ya kimataifa hususan masuala ya amani na ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika kudumisha amani sehemu mbalimbali Afrika na katika nchi nyingine duniani. Tanzania ina majeshi ya kulinda amani katika nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Darfur nchini Sudan na Lebanon.
 
Rais Kikwete yupo jijini New York nchini Marekani ambapo anaendelea vyema na ukaguzi wa kawaida wa afya yake.(picha na Freddy Maro)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwaajili ya kufanya mazungumzo nae.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Mazungumzo na Mwenyeji wake,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon alipomtembelea ofisi kwake jijini New York, Marekani 24/12/2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyeji wake,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon mara baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini New York, Marekani 24/12/2013.

RAIS KIKWETE, DK. SHEIN WAKABIDHIWA RASIMU YA PILI YA KATIBA LEO

 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu, Joseph Warioba, akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete, rasimu ya pili ya Katiba mpya, leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini, Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa kazi ya kukusanya maoni ya wananchi.
Jaji Warioba akikabidhi rasimu hiyo pia kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
 Rais Jakaya Kikwete akiwakabidhi Rasimu ya Katiba Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kulia), Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (katikati) na Waziri Mkuu wa zamani, Cleopa Msuya (kushoto) baada ya kukabidhiwa rasmi na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Rasimu ya Katiba Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
 Baadhi ya viongozi wa vyama wakiwa katika hafla hiyo.
 Baadhi ya viongozi wastaafu na waasisi wa Tanzania, wakiwa wameshikilia rasimu hiyo, baada ya kukabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete jana. Kutoka kushoto ni Balozi mstaafu Job Lusinde, Sir George Kahama, Hassan Nassor Moyo na Jaji mstaafu, Mark Bomani na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Mirisho Sarakikya
Baadhi ya wananchi na wanazuoni wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhiwa Rais Jakaya Kikwete na Dk. Ali Mohamed Shein, rasimu ya mwisho ya katiba.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiwapongeza wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya katiba baada ya makabidhiano ya Rasimu ya pili ya Katika katika viwanja vya Karimjee Hall jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Kikwete akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti  wa NCCR Mageuzi,  James Mbatia.
Rais Jakaya Kikwete, Dk. Shein, Dk. Bilal, Maalim Seif Sharif Mahad na viongozi wengine wakiwa na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba

RAIS JAKAYA KIKWETE AKABIDHIWA RASMU YA KATIBA MPYA NA MWENYEKITI WA TUME YA KATIBA.

RAIS Kikwete akikabidhiwa rasmu ya Katiba na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji, Joseph Walioba leo, Picha kwa hisani ya richard-mwaikenda.BlogSpot.com
 
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amekabidhiwa rasimu ya pili ya katiba mpya na tume ya katiba inayoongozwa na mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba.
Kikwete amesema kuwa kazi iliyofanyika katika mchakato huo imewezesha makundi mbalimbali katika jamii kuchangia mawazo yao kupitia tume aliyoiunda ili kupata mawazo ya watanzania kuhusiana na katiba wanayoitaka.Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amekabidhiwa pia rasmu hiyo na kueleza kuwa kuwa wajumbe watakaoteuliwa katika bunge la katiba wanapswa kufanya kazi kwa bidii kama ilivyokuwa kwa kamati hii iliyomaliza kazi yake Jaji mstaafu Warioba amesema rasimu hii wanayoiwasilisha ni ndefu kuliko ile ya awali iliyokuwa na ibara 240 wakati hii ina ibara 271 ikiwa ni matokeo ya tume kuzingatia maoni ya mabaraza ya katiba yaliyotoa maoni mengine mapya 
Ameyataja baadhi ya mambo ambayo tume imebaini kuwa yalijadiliwa kwa hisia kali katika rasmu hiyo na ile ya awali kuwa ni suala la muungano hasa kuhusu muundo wake. 

Amesema wakati tume inazindua rasmi ya awali hawakupendekeza kuendelea kuwa na muundo wa serikali mbili ulihitaji ukarabati mkubwa ambao tume ilifikiri hautawezekana, hivyo mabaraza ya katiba yalitoa mapendekezo mengi yaliyoilazimu tume kufanya uchambuzi wa kina na kwamba iliwachukua muda mrefu wa tume.

Jaji Warioba amesema wananchi Zaidi ya 39,000 wa Tanzania bara waliotoa maoni yao kuhusu muungano na kati yao karibu 27,000 walizungumzia muundo na Zanzibar wananchi karibia wote waliotoa maoni walijikita katika muungano ambapo kati ya wananchi 38,000 wa Zanzibar waliotoa maoni 19,000 walizungumzia muundo wa muungano. 

Tanzania bara asilimia 13 walitaka serikali moja, asilimia 24 walipendekeza serikali mbili na 61 walipendekeza serikali tatu, wakati Zanzibar asilimia 34 walipendekeza serikali mbili na asilimia 60 muungano wa mkataba ambapo asilimia 0.1 walihitaji serikali moja. 
Hata hivyo Rasimu hiyo ya katiba iliyokabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeorodhesha malalamiko 10 kwa upande wa Zanzibar na manane ya Tanzania Bara 
Malalamiko matatu makubwa kwa Zanzibar ni Serikali ya Tanganyika kuvaa koti la serikali ya muungano hivyo kupunguza nguvu kwa Zanzibar,Ongezeko la mambo ya Muungano,kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Tanzania bara tume hiyo imeyataja malalamiko kuwa ni kuwa Zanzibar imekuwa nchi huru , ina bendera yake ya Taifa, ina serikali yake ina wimbo wake wa taifa na imebadili katika yake ili itambulike kama nchi wakati Tanzania bara imepoteza utambulisho wake, wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar wakati wenzao wanamiliki Tanzania bara. BBC

HATIMAYE TV IMAAN YA MOROGORO YAPATA RASMI KIBALI KUTOKA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA TCRA

JAJI AUGUSTINO RAMADHANI AWA MCHUNGAJI ANGLIKANA

Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ametawazwa kuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar na kusema ameshangazwa na mashambulizi ya tindikali dhidi ya viongozi wa dini Visiwani humo.
Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kutawazwa ndani ya Kanisa la Anglikana la Minara Miwili Mjini Unguja, Jaji Ramadhan amesema vitendo vya hujuma vinavyofanywa dhidi ya viongozi wa dini na Serikali ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar.
Alisema Wakristo na Waislamu Zanzibar kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi kama ndugu bila ya kubaguana kwa sababu za itikadi ya dini licha ya Waislamu kuwa asilimia 95.
Hata hivyo, alikumbusha kuwa wakristo wana mchango katika harakati za ukombozi wa Zanzibar, ambapo idadi kubwa ya waumini wake walianzisha Chama cha African Association mwaka 1935, ambapo rais wake wa kwanza alikuwa hayati, Mzee Augustino Ramadhan na baadaye akafuata hayati Mzee Abeid Amani Karume.
"Vitendo vya watu kumwagiwa tindikali vinanishangaza, sababu halisi siifahamu, najiuliza haya yametokea wapi, siyo jambo jema wala siyo sifa ya Zanzibar tokea enzi na enzi," alisema.
Alisema wakati umefika na kuwataka viongozi kuwa mstari wa mbele kukemea matukio ya hujuma za tindikali na uhalifu mwingine ikiwemo mashambulizi ya kutumia silaha za moto na watu kupotezewa maisha.
Jaji Augustino amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar na Tanzania, Brigedia Jenerali wa JWTZ pia amewahi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mahakama ya Afrika Mashariki, ambapo amesema kazi ya sheria hazitofautiani na kazi za kiroho kwa vile zote zinahitaji utende haki na kutimiza wajibu upasavyo. Kwa upande wake Askofu Philip Baji wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John cha Dodoma, alisema huu ni wakati mwafaka kwa Serikali kuwalinda viongozi wa dini bila ya kujali tofauti ya madhehebu yao kutokana na kukithiri kwa vitendo vya hujuma.
Chanzo:Mwananchi

MAALIM SEIF: WAZANZIBAR WANATAKA MAMLAKA KAMILI

maalim1 1e311
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema Wazanzibar wanaisubiri kwa hamu Rasimu ya Katiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili kuona kama imezingatia masilahi na matakwa yao katika kupata mamlaka kamili ya Zanzibar. (HM)

Msimamo huo ameutoa kwenye mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika Kinyasini, Mkoa wa Kalazini Unguja na kuhudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Maridhiano inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Mzee Hassan Nassor Moyo.
Aidha, katika mkutano huo, kwa mara ya kwanza Waziri wa zamani wa SMZ na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Mansoor Yussuf Himid alihutubia tangu avuliwe uanachama wa CCM kutokana na madai ya kwenda kinyume na sera, maadili na nidhamu ya chama hicho.
Katika maelezo yake, Maalim Seif alisema wanachodai Wazanzibar
ni mamlaka kamili ni kuifanya Zanzibar ijitegemee kiuchumi, kujipangia na kujiamulia mambo yake ya ndani na nje bila ya kutegemea upande wowote.
Alisema Zanzibar ilikuwa taifa huru lililoungana na Tanganyika kwa ridhaa na siyo mateka wa Tanganyika, hivyo wanayo sababu ya kujitegemea.
"Madai yetu yako wazi, hayana kificho na siyo mageni, tunaisubiri kwa hamu rasimu ya Jaji Warioba, kama ni supu isiyolika, hatutaila tutamrudishia mwenyewe na kuendeleza madai yetu," alisema Maalim Seif.
Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, alisema Zanzibar itasimama wenyewe na kujiendeleza kwa kufuata misingi iliyowekwa na Rais wa Kwanza wa Zanzibar hayati Mzee Abeid Amani Karume.
"Madai yetu ni kama meli iliyobeba watu wengi, ikizama tunazama wote, lengo letu ni kufika salama katika bandari ya matumaini na kila mmoja aweze kunufaika na matunda ya nchi yake," alisema Maalim Seif.
Alisema ikiwa Wazanzibari watapata Serikali, anaamini mengine yatakuja yenyewe na kuinufaisha Zanzibar kiuchumi na kusisitiza kuwa muundo wa Serikali mbili umepitwa na wakati. Chanzo: mwananchi

WARAKA WA ABSALOM KIBANDA KWA RAIS JAKAYA KIKWETE

 Absalom Kibanda
Rais Jakaya Kikwete alipofika Kumjulia Hali Absalom Kibanda nchini afrika ya kusini Mwezi Tarehe 8-2013
---

MHESHIMIWA Rais wangu, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Nakusalimu kwa salamu ya utii inayotambua na kuheshimu kwa dhati mamlaka makubwa na ya juu uliyonayo kama mkuu wa taifa letu ambalo mazingira yake ya leo yanapaswa yawe wenye mwelekeo wa kushangilia kama si kujivunia uhuru ambao tuliupata mwaka 1961 na 1964 kwa kutegemea upande tulipo katika muungano wetu.

Mheshimiwa Rais, najisikia faraja iliyojaa majonzi moyoni kupata fursa hii adhimu kukuandikia waraka ambao msukumo wake unasukwasukwa na dhamira njema kabisa ambayo aghalabu kiini chake si kingine bali mapenzi mema kwa nchi na viongozi wetu wote.

Ni faraja kwa kuwa nimepata fursa ghali na adimu ya kuteta na kiongozi wetu mkuu kwa upendo, uhuru na kwa kujiamini, huku nikiwa na uchungu pia kwa sababu ujumbe ambao unabebwa na waraka huu ni wa kuumiza sana nafsi, roho, akili na mwili.

Mheshimiwa Rais, wewe ni kiongozi wa Watanzania wote tukiwamo sisi ambao baadhi ya wateule wako wameamua kwa sababu wanazozijua wao na wakati mwingine wakidai kwa maelekezo ya wakuu wao kutujengea taswira zinazotufanya tuonekane tu watu wa ovyo na kada ya wanajamii waliokosa utu na eti tunaopaswa kufundishwa hekima na somo la uzalendo ambalo limekuwa sehemu ya makuzi yetu nyumbani, shuleni, jeshini na ndani ya jamii.

Kabla sijafikisha ujumbe ambao nimeubeba kwa mfano wa mzigo mzito moyoni, napenda kwanza kupitia fursa hii kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema na neema kwa kuniwezesha kuuona mwanga wa siku hii njema ya leo ambayo kama si kwa kudra na mapenzi yake, yumkini ingeongeza hesabu za siku ambazo kiwiliwili changu kingekuwa katika kaburi la sahau ambalo kila kukicha linameza roho za makumi kama si mamia ya Watanzania wasio na hatia wanaopoteza maisha kutokana na kazi za mikono ya majahili, miungu watu waliojitwalia haki ya kuchagua aina ya maisha na vifo vya watu wengine. 

Baada ya hilo, kwa niaba ya mamilioni ya Watanzania wenzangu ambao hawana fursa ya kuwasiliana nawe kwa njia kama hii ya waraka niliyoitumia, napenda kutumia pia wasaa huu kukushukuru wewe binafsi kwa namna ulivyojitoa usiku na mchana pasipo kuchoka kuliongoza taifa hili katika mazingira magumu yaliyojaa changamoto za kila namna ambazo wakati mwingine sina shaka hata kidogo kwamba zimekuwa zikikunyima raha na kukosa usingizi.

Wakati nikikuandikia ujumbe huu, picha na taswira yako inayonijia ni ile ya Machi 8, mwaka huu siku uliponitembelea kando ya kitanda nilichokuwa nimelazwa katika Hospitali ya Milpark, Johanesburg kule Afrika Kusini ikiwa ni siku mbili tangu nilipovamiwa, nikajeruhiwa na kupewa ulemavu na majahili ambao hadi leo hii wameweza kuukwepa mkono mrefu wa vyombo vya dola unavyoviongoza.

Mheshimiwa Rais, japo nilikuwa nina maumivu makali na machungu ya kupoteza jicho, kidole na kupasuliwa kwa mifupa ipatayo minane katika paji langu la uso, ukiacha taya lililoachanishwa kikatili na watesi wangu wale, bado ninaweza kukumbuka kwa ufasaha namna ulivyozungumza nami ukionyesha jinsi ulivyokuwa ukiguswa na kuumizwa sana na tukio lile. 

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, tangu niliporejea nchini miezi sita iliyopita sijapata kukutana nawe ana kwa ana ingawa nilipata fursa ya kukutumia salamu zangu za shukrani kupitia kwa marafiki zako kadhaa akiwamo msaidizi na mshauri wako nambari moja, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal ambaye siku zote wakati nikiwa katika matibabu nchini Afrika Kusini na hata baada ya kurejea nchini, alionekana kuwa mtu wa kukosa amani kabisa pasipo kunijulia hali kwa njia ama ya simu, wasaidizi wake na mwisho kwa kuonana nami ana kwa ana. 

Nayarejea haya yote huku nikitambua kwamba, wakati ninapoandika waraka huu ndiyo kwanza umerejea kutoka nchini Marekani ambako ulikwenda kuchunguzwa afya yako ambayo nina matumaini makubwa ni njema hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa, ulikwenda huko siku chache tu baada ya kuiwakilisha vyema nchi yetu katika msiba mzito wa shujaa wa mapambano ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, mzee wetu, Nelson Mandela.

Ninapoyatafakari matibabu ghali niliyopata nchini Afrika Kusini kwa msaada wa mwajiri wangu na safari yako nchini Marekani, vinanikumbusha swali la mmoja wa wasaidizi wangu hapa ofisini aliyetaka kujua ni sababu gani hasa ambazo zimekuwa zikisababisha wasomi na viongozi wetu kuchunguzwa na kutibiwa katika hospitali za nje, tofauti na ilivyokuwa kwa Madiba ambaye kwa nyakati zote tangu afya yake ianze kumtatiza alikuwa akipata matibabu huko huko kwao Afrika Kusini?

Niseme kweli, japo nilikuwa na jibu au majibu ya swali lake, sikuwa na maelezo ya kutosheleza yaliyokuwa na mwelekeo wa kukata kiu ya swali lake, ingawa kwa kupapasa nilifanya kila juhudi kuutetea utaifa wangu na viongozi wake ilhali miye mwenyewe nikiendelea kukosa raha kwa namna nilivyokuwa nikitoa majibu ambayo yalikuwa yakionyesha hali ya kuukubali unyonge, kukiri ufukara, kuficha udhaifu wetu kama taifa na kutetea makosa ambayo aghalab ninyi viongozi wetu na wale wa kabla yenu mngeweza kuwa watu mliostahili kuwa na majibu halisi.

Rais wangu, swali na majibu vilisababisha kimoyomoyo, nijiulize maswali mengi mengine na moja ya maswali hayo yakiwa ni wapi tulipopotea njia hata tukafikia hatua ya kusababisha kuwa na kundi kubwa la watu waliokata tamaa, wanaoteswa na ufukara, ukosefu wa ajira na kila aina ya kero na karaha zinazozonga maisha yao ya kila siku.

Mheshimiwa Rais, hali hiyo ilinipeleka moja kwa moja nchini Afrika Kusini na hususan katika Hospitali ya Milpark ambako huko ndiko miye mwenyewe na Watanzania wenzangu wengine tulikonusuru maisha yetu, huku baadhi kama ilivyo kwa Dk. Sengondo Mvungi wakipoteza maisha yao baada ya kukimbizwa huko. 

Mheshimiwa Rais, naomba unisamehe kwa kulisema hili nitakaloliandika hapa kwamba, jibu nililolipata haraka haraka kuwa moja ya chagizo la matukio ya namna hii kutokea, halikuwa jingine bali ni kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa viongozi wetu hususan wale tuliowapa dhamana ya kuongoza sekta kadhaa nyeti kama ya afya na ustawi wa jamii.

Ushahidi wa kupwaya huko kwa viongozi hususan wale walio chini yako, ndiko huko huko ambako kumedhihirika pia wiki iliyopita bungeni Dodoma, ambako tulishuhudia zahama nyingine iliyowang’oa madarakani mawaziri wako muhimu wanne kwa sababu kama hizo hizo za mkwamo wao au watendaji wa chini yao katika kusimamia ipasavyo na kuchukua hatua kwa wakati, kila yatokeapo matatizo yanayogusa maeneo wanayoyaongoza.

Nitakuwa sijaitendea haki nafsi yangu, mheshimiwa Rais iwapo nitaficha shauku ya moyo wangu ambayo ilikwenda sambamba na tukio lile la Dodoma lililowagusa baadhi ya mawaziri ambao anguko lao linaweza likaelezwa kuwa ni ‘ajali ya kisiasa’ nikitumia msamiati ulioutumia wewe mwenyewe kwa mara ya kwanza ulipozungumzia tukio la kujiuzulu kwa waziri wako mkuu wa kwanza, Edward Lowassa.

Haja ya moyo wangu, nikiwa mhariri, mwanahabari, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na mdadisi wa kawaida tu wa mambo, ilikuwa kuona anguko la namna hiyo hiyo likimfika Waziri wa Habari ambaye amethibitisha pasipo na shaka kuwa pamoja na kuwa msomi wa Shahada ya Falsafa (Phd), ni kiongozi asiyejua anachofanya kwa kiwango cha kuwa mtu ambaye vichwa vya watu wengine ndivyo vinavyofikiri kwa niaba yake. 

Nilitamani afikwe na zahama hiyo si kwa sababu ya kuwa na hasira au kumchuria mabaya, bali kwa kuzingatia ukweli kwamba yeye ni mtu ambaye bado anasongwa na matongotongo ya mfumo wa kibabe wa zama za magazeti ya Serikali na yale ya chama tawala, ambayo yanalazimika kuandika yale tu yanayofurahisha nyoyo na akili za watawala.

Mheshimiwa Rais, ingawa natambua na kuheshimu ukweli mchungu kwamba, suala la nani awe waziri na nani asiwe ni jambo la wewe mwenyewe kupenda na kuchagua na kwamba ulishasema mapema kabisa mbele yetu kwamba urais wako hauna ubia, bado naamini pia kwamba, wewe ni mtu msikivu na mkweli uliye tayari kusikia na kustahimili mambo mengi machungu unayokabiliana nayo kila siku.

Kwa sababu hiyo, basi napenda kukueleza kwa kuweka kumbukumbu sahihi ili mbele ya safari kabla na baada ya kumaliza urais wako uje kuyatafakari na kuukumbuka ushauri huu kwako kwamba, waziri uliyempa dhamana ya kulea na kuendeleza vyombo vya habari, ni mtu wa kuhofiwa, jeuri, mwenye kiburi, asiyeshaurika na dikteta asiyekutakia mema wewe binafsi, vyombo vya habari, serikali yako na taifa kwa ujumla. 

Mheshimiwa rais sijui kama unajua kwamba tangu umteue amefanya kazi na vyombo vya habari vya umma na hata baada ya sisi kufanya juhudi kubwa ya kuwa karibu naye kikazi kwa makusudi na kwa ujeuri mkubwa, amekataa wito na kupuuza maoni na ushauri wetu na kwa namna ya kusikitisha amesikika akitamba waziwazi kwamba anao uwezo wa kulifungia au kulifutia usajili gazeti lolote ambalo ataliona linakwenda kinyume cha maadili ya uandishi wa habari. 

Waziri huyu ambaye alitarajiwa kuwa na silika za kuwa mlezi bora kutokana na jinsia yake na historia yake ya kupata kuwa mwanaharakati kabla ya kuingia serikalini, ndiye ambaye mamlaka makubwa uliyomtwisha, ameyageuza na kuwa mwavuli wa kuvisulubisha vyombo vya habari vyenye uthubutu wa kukosoa serikali na kuandika ukweli mchungu ambao asingependa kuona ukiripotiwa.

Mheshimiwa Rais, pengine baya zaidi kwa tasnia hii ni kwamba waziri huyo ana bahati mbaya ya kuwa na mmoja wa wasaidizi na washauri wake katika sekta yetu ya habari ambaye naye, hulka zake tangu aingie katika tasnia ya habari amekuwa ni mtu wa kujipendekeza, kupenda makuu, kuzusha na kutokuwa na mawazo huru. Huyu si mwingine bali Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO). 

Ni jambo la bahati mbaya kwamba waziri huyu msomi pengine kwa sababu ya kutojua vyema rekodi na historia ya msaidizi wake huyo, ambaye japokuwa naye pia ni mteule wako, amejikuta akiwa mhanga wa fikra pandikizi zinazopenyezwa wizarani chini ya uratibu mahususi unaofanywa na baadhi ya wateule wako ambao wameshaanza kujipanga kusaka urais baada ya wewe kustaafu.

Mheshimiwa Rais, nimelazimika kuyasema yote haya baada ya kula kiapo cha moyoni huku nikirejea mafunzo tuliyokuwa tukikaririshwa utotoni chini ya imani ya wana TANU, ambayo hata sisi ambao hatukuwa wanachama wa chama hicho tulilazimika kuikariri kwa kuitamka kila kukicha; ‘Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.’

Rais wangu, gazeti la MTANZANIA limerejea tena mitaani. Japokuwa ni rahisi kuhesabu miezi, napenda kukueleza kwamba, ilikuwa ni miezi mitatu michungu sana kwetu kihisia na katika hali halisi.

Nitakuwa mzushi sawa sawa na hao ninaowashangaa leo, iwapo nitasema kulikuwa hakuna hitilafu au makosa ya kiuandishi ambayo yaliwapa kisingizio cha mikakati waliyoipanga mapema kabisa, wasaidizi wako hao kwa kulifungia gazeti letu hili.

Mheshimiwa Rais, nasema haya kwa sababu ni ukweli ulio bayana kabisa kwamba, habari zilizoandikwa na kutoa mwanya kwa serikali yako kutuadhibu gazeti hili, hazikulenga kuchochea na wala hazikuchochea kabisa chuki yoyote dhidi ya yeyote na mamlaka unazoziongoza kwa namna na kwa njia yoyote ile.

Siyo siri hata kidogo, mkurugenzi aliyetangaza uamuzi huo alifanya hivyo akijua watu wengi hawajui mapito na dhamira yake. Tunajua yeye alimshauri vibaya waziri na serikali huku akijua vyema kwamba, yuko hapo alipo kwa maelekezo mahususi ya kundi la watu wenye malengo binafsi ambao mheshimiwa rais, niko tayari wakati wowote na mahali popote kukueleza kwa kina na kwa undani ili wakati utakapotaka kuchukua maamuzi ya haki na kweli ujue undani halisi wa mambo haya. 

Leo hii wakati tukirejea tena sokoni, tayari tumeshasikia kuendelea kuwapo kwa mikakati ile ile ya kuhakikisha gazeti hili na jingine ambalo halipendwi na watu hao hao kwa sababu binafsi yakiinaingizwa tena mtegoni na kufungiwa kifungo kingine kama hiki tulichomaliza au kinachofanana na kile kilichoifika MwanaHalisi. 

Mheshimiwa Rais, naandika waraka huu nikikumbuka semi zako mbili unazotumia; ‘tunajenga nyumba moja kwanini tugombee fito?’ na ile ya ‘akili za kuambiwa changanya na zako’ ambazo kwa muktadha wa waraka wangu huu kwako zinaweza zikawa za msaada sana kwako na pengine kwetu sisi wa MTANZANIA ambao tunashangilia kurejea mtaani kwa gazeti letu lililodhulumiwa fursa ya kuchapwa kwa muda wa siku 90.

Nimelazimika kukutumia wewe Rais si kwa lengo la kuchosha akili zako au kukupotezea muda, isipokuwa kwa kutambua hadhi, heshima na mamlaka makubwa uliyonayo juu ya wateule wako hao ambao wameamua kwa sababu ya jeuri za kimamlaka walizonazo kuumiza watu na kutupa sifa na majina mabaya tusiyostahili. Hakika wazungu walikuwa sahihi waliposema ‘power currupts’. 

Mheshimiwa Rais, lingekuwa ni jambo la kheri kwa Serikali na kwa taifa letu zima iwapo kusudi la kufungia magazeti linalopangwa na wateule wako kuwa utamaduni wa kudumu, lingekuwa ni kujenga mustakabali mwema kwako wewe binafsi, chama chako, Serikali unayoiongoza na nchi yetu kuliko hili la sasa lenye dhamira ya kufunga watu midomo, kutesa, kuzusha na kuharibu taswira yetu kama watu binafsi, taasisi na taifa.

Ni kwa sababu hizo, mheshimiwa Rais ndiyo maana baada ya kusukwasukwa na moyo na kuumizwa mno kifikra nikaona nitakuwa sijaitendea haki nafsi yangu na haki za maelfu ya Watanzania ambao tunaamini wanahitaji huduma ya magazeti haya katika kukidhi mahitaji yao muhimu ya kimaisha, kielimu na kiufahamu kila kukicha na kuacha dhamira hizi za kishetani zikiendelea kuongoza sekta yetu.

Mheshimiwa Rais, siyo siri hata kidogo kwamba, ingawa mawazo hasi dhidi ya uhuru wa kikazi na kiwajibikaji wa vyombo vya habari na wanahabari yanaonekana kutawala kauli na maamuzi ya baadhi ya viongozi na washauri wako kwa kiwango cha kukushawishi hata wewe binafsi kukubaliana nayo, ukweli ni kwamba, nyuma ya maneno matamu wanayotumia kutupaka matope, kutujeruhi na kutupa kila aina ya sifa mbaya kuna ajenda za kutuharibia sisi, kukuharibia wewe, kukomoa, kuumiza na zaidi kulikwamisha taifa.

Nitakuwa mhariri nisiyewajibika, iwapo nitakaa kimya ilhali nikijua fika kwamba, leo hii ndani ya wizara iliyopewa dhamana ya kulea vyombo vya habari, baadhi ya wateule wako na watendaji wake wamekalia viti walivyonavyo si kwa sababu ya kuwa kwao na uwezo kustahimili ukosoaji, au upeo wao wa kuchochea maendeleo ya kitaaluma, bali kwa kuendeleza na kuyatumikia matakwa ya utarishi wa kifikra na kimatendo. 

Kwa waraka huu mheshimiwa Rais, wakati tukikuahidi kwa dhati kabisa wewe binafsi na Watanzania wenzetu kwamba, tutaendelea na kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ya uandishi wa habari, sambamba na kuheshimu sheria zilizopo, tunapenda kuliweka hili bayana kwamba, tutakuwa wa mwisho kuwatii viongozi dhalimu, madikteta, waliokosa utu na ambao kwao hila ndiyo msingi mama wa kupotosha na kupindisha mambo kwa sababu tu ya kulinda maslahi na malengo yao binafsi au yale ya makundi yenye hila.

Rais wangu, nimeona nitakuwa mtu nisiyekutakia mema wewe binafsi na taifa kwa ujumla, iwapo nitakaa kimya na kuruhusu fikra za kikaburu zikijijenga vichwani mwa viongozi wetu. 

Mheshimiwa Rais, tutakuwa tumeshindwa kutimiza wajibu wetu kama wanahabari, wahariri na viongozi iwapo tutahalalisha kwa sababu ya ukimya wetu majina mabaya tunayoitwa leo na wateule wako kama wasaliti, wachochezi na wazushi.

Miye binafsi naamini kwa dhati kabisa kwamba iwapo wewe utaamua kwa moyo na nia njema kulinusuru taifa letu na majahili hao walio ndani ya Serikali yako, basi siku moja historia itakuja kuandika kwa usahihi na ufasaha jina lako na letu..

Mungu ibariki Tanzania.

Jumapili, 29 Desemba 2013

KATUNI YA LEO

Picture

MTEMVU AIPIGA JEKI TIMU YA NETIBOLI YA TEMEKE QUEENS MASHINDANO YA KOMBE LA TAIFA 2013

Makala
Rai ya Jenerali
Misafara mirefu, posho kubwa, tija kidogo
Jenerali Ulimwengu
Toleo la 331
25 Dec 2013
PASI na shaka, kwa msomaji aliyefuatilia vilivyo kwa wiki kadhaa sasa (naomba radhi kwa wiki mbili zilizopita) nitakuwa nimeeleweka kuwa ninachokisema katika mfululizo huu ni kwamba diplomasia yetu imeshindwa kutuletea matunda ambayo tungetaraji kuyavuna kama diplomasia yetu ingekuwa imefanya kazi ipasavyo. Pasi na shaka pia, haya ni maoni yangu binafsi ambayo Kiingereza yanaweza kuitwa ‘subjective’ kwa sababu hayana vigezo vya uyakinifu vya kuweza kuyathibitisha.
Hayawezi kuwa na ukweli kama ule uliomo ndani ya uzani wa kilo moja, au ratili moja, au sentimeta moja, au yadi moja.
Kwa sababu ya kukosa uyakinifu wa aina hiyo, mambo kama haya hujadiliwa kwa kuyatolea maelezo marefu ambayo aghalabu huhitaji kuambatanishwa na mifano mingi, na wala hilo halikomeshi malumbano.
Kwa kuwa ni maoni ambayo uyakinifu wake haupimiki yatabakia daima katika medani ya mabishano. Lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya watu wenye akili kuona zoezi la kutoa maoni, hata kama ni ‘subjective,’ kuwa ni kupoteza muda.
Maoni ‘subjective’ yanapogonganishwa na mawazo ‘subjective’ ya mtazamo tofauti yanaanza safari kuelekea mawazo ‘objective’ hata kama si lazima kila mara tufike  huko. Mara nyingi zaidi tunapata fursa na wasaa wa kurekebisha yale ambayo ni dhahiri hayako sawa.
Naomba nirejee nyuma kidogo, nimrudishe msomaji katika mihadhara aliyotoa Mwalimu Julius Nyerere katikati ya miaka ya 1990. Katika mmojawapo wa mihadhara hiyo Mwalimu, ambaye pasi na shaka alikuwa anaukosoa uongozi uliokuwa madarakani wakati huo, alieleza jinsi thamani ya diplomasia ya Tanzania ilivyokuwa imeporomoka.
Alimnukuu mama mmoja kutoka nchi moja jirani ambaye alitaka kujua kutoka kwa Mwalimu nini kilikuwa kimeisibu diplomasia ya Tanzania. Mama huyo, kwa mujibu wa Kambarage, akasema kwamba huko nyuma, katika vikao vya kimataifa, ilikuwa ikitangazwa kwamba ni zamu ya ujumbe wa Tanzania kutoa hotuba, watu waliokuwa wanavuta sigara wanazizima haraka waliwahi kusikiliza hotuba ya Tanzania, na wale waliokuwa wakinywa chai wanaacha chai na kurejea ukumbini.
Mama huyo akaendelea kuumueleza Mwalimu: ‘Siku hizi ikitangazwa kwamba Mtanzania anazungumza, ndipo wajumbe wa nchi nyingine wanaona ni fursa ya kutoka kwenda kuvuta sigara au kunywa chai!’ Sasa, mimi sina shaka kwamba kwa kusema maneno hayo na kwa kutoa mfano huo, Kambarage alikuwa anatamba kwa kuonyesha kwamba utawala wake ulikuwa unajua namna ya kuendesha diplomasia kuliko utawala uliokuja baada yake.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/misafara-mirefu-posho-kubwa-tija-kidogo#sthash.ntvqjdvE.dpuf

 Mbunge wa Temeke, ambaye pia ni Mlezi wa timu ya netiboli ya Temeke Queens, Abbas Mtemvu, akimrejeshea Kombo la ubingwa Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Kibira lililokuwa linashikiliwa na mabingwa watetezi wa michuano ya Taifa Cup, Temeke Queens. Hafla hiyo ilifanyika wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo kwenye Uwanjawa Taifa Dar es Salaam.
 Mtemvu akimkabidhi kocha wa Temeke Queens, Amina Mussa fedha kwa ajili ya posho za wachezaji na viongozi wa timu hiyo inayoshiriki michuano hiyo.

 Mtemvu akiwa na wachezaji wa timu ya Temeke Queens mabingwa watetezi wa mashindano hayo.(P.T)
 Mwanaidi Ngubege wa Temeke Queens (kushoto) akijiandaa kufunga goli dhidi ya timu ya Mkoa wa Katavi.
 Lillian Sylidion wa Temeke akidaka mpira

  Mchezaji Sekela Dominick (kushoto) wa timu ya Temeke Queens akigombea mpira wa juu ya Rose Israel wa timu ya Mkoa wa Katavi katika mashindano ya kuwania Kombe la Taifa (Taifa Cup) siku ya ufunguzi wa michuano ya mchezo wa netiboli, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Temeke Queens ilishinda 58-27. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Benchi la wachezaji wa timu ya Mkoa wa Katavi
Kocha Amina Mussa wa Temeke akitoa mawaidha kwa wachezaji wakati wa mapumziko 
Makala
Rai ya Jenerali
Misafara mirefu, posho kubwa, tija kidogo
Jenerali Ulimwengu
Toleo la 331
25 Dec 2013
PASI na shaka, kwa msomaji aliyefuatilia vilivyo kwa wiki kadhaa sasa (naomba radhi kwa wiki mbili zilizopita) nitakuwa nimeeleweka kuwa ninachokisema katika mfululizo huu ni kwamba diplomasia yetu imeshindwa kutuletea matunda ambayo tungetaraji kuyavuna kama diplomasia yetu ingekuwa imefanya kazi ipasavyo. Pasi na shaka pia, haya ni maoni yangu binafsi ambayo Kiingereza yanaweza kuitwa ‘subjective’ kwa sababu hayana vigezo vya uyakinifu vya kuweza kuyathibitisha.
Hayawezi kuwa na ukweli kama ule uliomo ndani ya uzani wa kilo moja, au ratili moja, au sentimeta moja, au yadi moja.
Kwa sababu ya kukosa uyakinifu wa aina hiyo, mambo kama haya hujadiliwa kwa kuyatolea maelezo marefu ambayo aghalabu huhitaji kuambatanishwa na mifano mingi, na wala hilo halikomeshi malumbano.
Kwa kuwa ni maoni ambayo uyakinifu wake haupimiki yatabakia daima katika medani ya mabishano. Lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya watu wenye akili kuona zoezi la kutoa maoni, hata kama ni ‘subjective,’ kuwa ni kupoteza muda.
Maoni ‘subjective’ yanapogonganishwa na mawazo ‘subjective’ ya mtazamo tofauti yanaanza safari kuelekea mawazo ‘objective’ hata kama si lazima kila mara tufike  huko. Mara nyingi zaidi tunapata fursa na wasaa wa kurekebisha yale ambayo ni dhahiri hayako sawa.
Naomba nirejee nyuma kidogo, nimrudishe msomaji katika mihadhara aliyotoa Mwalimu Julius Nyerere katikati ya miaka ya 1990. Katika mmojawapo wa mihadhara hiyo Mwalimu, ambaye pasi na shaka alikuwa anaukosoa uongozi uliokuwa madarakani wakati huo, alieleza jinsi thamani ya diplomasia ya Tanzania ilivyokuwa imeporomoka.
Alimnukuu mama mmoja kutoka nchi moja jirani ambaye alitaka kujua kutoka kwa Mwalimu nini kilikuwa kimeisibu diplomasia ya Tanzania. Mama huyo, kwa mujibu wa Kambarage, akasema kwamba huko nyuma, katika vikao vya kimataifa, ilikuwa ikitangazwa kwamba ni zamu ya ujumbe wa Tanzania kutoa hotuba, watu waliokuwa wanavuta sigara wanazizima haraka waliwahi kusikiliza hotuba ya Tanzania, na wale waliokuwa wakinywa chai wanaacha chai na kurejea ukumbini.
Mama huyo akaendelea kuumueleza Mwalimu: ‘Siku hizi ikitangazwa kwamba Mtanzania anazungumza, ndipo wajumbe wa nchi nyingine wanaona ni fursa ya kutoka kwenda kuvuta sigara au kunywa chai!’ Sasa, mimi sina shaka kwamba kwa kusema maneno hayo na kwa kutoa mfano huo, Kambarage alikuwa anatamba kwa kuonyesha kwamba utawala wake ulikuwa unajua namna ya kuendesha diplomasia kuliko utawala uliokuja baada yake.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/misafara-mirefu-posho-kubwa-tija-kidogo#sthash.ntvqjdvE.dpuf
Makala
Rai ya Jenerali
Misafara mirefu, posho kubwa, tija kidogo
Jenerali Ulimwengu
Toleo la 331
25 Dec 2013
PASI na shaka, kwa msomaji aliyefuatilia vilivyo kwa wiki kadhaa sasa (naomba radhi kwa wiki mbili zilizopita) nitakuwa nimeeleweka kuwa ninachokisema katika mfululizo huu ni kwamba diplomasia yetu imeshindwa kutuletea matunda ambayo tungetaraji kuyavuna kama diplomasia yetu ingekuwa imefanya kazi ipasavyo. Pasi na shaka pia, haya ni maoni yangu binafsi ambayo Kiingereza yanaweza kuitwa ‘subjective’ kwa sababu hayana vigezo vya uyakinifu vya kuweza kuyathibitisha.
Hayawezi kuwa na ukweli kama ule uliomo ndani ya uzani wa kilo moja, au ratili moja, au sentimeta moja, au yadi moja.
Kwa sababu ya kukosa uyakinifu wa aina hiyo, mambo kama haya hujadiliwa kwa kuyatolea maelezo marefu ambayo aghalabu huhitaji kuambatanishwa na mifano mingi, na wala hilo halikomeshi malumbano.
Kwa kuwa ni maoni ambayo uyakinifu wake haupimiki yatabakia daima katika medani ya mabishano. Lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya watu wenye akili kuona zoezi la kutoa maoni, hata kama ni ‘subjective,’ kuwa ni kupoteza muda.
Maoni ‘subjective’ yanapogonganishwa na mawazo ‘subjective’ ya mtazamo tofauti yanaanza safari kuelekea mawazo ‘objective’ hata kama si lazima kila mara tufike  huko. Mara nyingi zaidi tunapata fursa na wasaa wa kurekebisha yale ambayo ni dhahiri hayako sawa.
Naomba nirejee nyuma kidogo, nimrudishe msomaji katika mihadhara aliyotoa Mwalimu Julius Nyerere katikati ya miaka ya 1990. Katika mmojawapo wa mihadhara hiyo Mwalimu, ambaye pasi na shaka alikuwa anaukosoa uongozi uliokuwa madarakani wakati huo, alieleza jinsi thamani ya diplomasia ya Tanzania ilivyokuwa imeporomoka.
Alimnukuu mama mmoja kutoka nchi moja jirani ambaye alitaka kujua kutoka kwa Mwalimu nini kilikuwa kimeisibu diplomasia ya Tanzania. Mama huyo, kwa mujibu wa Kambarage, akasema kwamba huko nyuma, katika vikao vya kimataifa, ilikuwa ikitangazwa kwamba ni zamu ya ujumbe wa Tanzania kutoa hotuba, watu waliokuwa wanavuta sigara wanazizima haraka waliwahi kusikiliza hotuba ya Tanzania, na wale waliokuwa wakinywa chai wanaacha chai na kurejea ukumbini.
Mama huyo akaendelea kuumueleza Mwalimu: ‘Siku hizi ikitangazwa kwamba Mtanzania anazungumza, ndipo wajumbe wa nchi nyingine wanaona ni fursa ya kutoka kwenda kuvuta sigara au kunywa chai!’ Sasa, mimi sina shaka kwamba kwa kusema maneno hayo na kwa kutoa mfano huo, Kambarage alikuwa anatamba kwa kuonyesha kwamba utawala wake ulikuwa unajua namna ya kuendesha diplomasia kuliko utawala uliokuja baada yake.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/misafara-mirefu-posho-kubwa-tija-kidogo#sthash.ntvqjdvE.dpuf
Makala
Rai ya Jenerali
Misafara mirefu, posho kubwa, tija kidogo
Jenerali Ulimwengu
Toleo la 331
25 Dec 2013
PASI na shaka, kwa msomaji aliyefuatilia vilivyo kwa wiki kadhaa sasa (naomba radhi kwa wiki mbili zilizopita) nitakuwa nimeeleweka kuwa ninachokisema katika mfululizo huu ni kwamba diplomasia yetu imeshindwa kutuletea matunda ambayo tungetaraji kuyavuna kama diplomasia yetu ingekuwa imefanya kazi ipasavyo. Pasi na shaka pia, haya ni maoni yangu binafsi ambayo Kiingereza yanaweza kuitwa ‘subjective’ kwa sababu hayana vigezo vya uyakinifu vya kuweza kuyathibitisha.
Hayawezi kuwa na ukweli kama ule uliomo ndani ya uzani wa kilo moja, au ratili moja, au sentimeta moja, au yadi moja.
Kwa sababu ya kukosa uyakinifu wa aina hiyo, mambo kama haya hujadiliwa kwa kuyatolea maelezo marefu ambayo aghalabu huhitaji kuambatanishwa na mifano mingi, na wala hilo halikomeshi malumbano.
Kwa kuwa ni maoni ambayo uyakinifu wake haupimiki yatabakia daima katika medani ya mabishano. Lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya watu wenye akili kuona zoezi la kutoa maoni, hata kama ni ‘subjective,’ kuwa ni kupoteza muda.
Maoni ‘subjective’ yanapogonganishwa na mawazo ‘subjective’ ya mtazamo tofauti yanaanza safari kuelekea mawazo ‘objective’ hata kama si lazima kila mara tufike  huko. Mara nyingi zaidi tunapata fursa na wasaa wa kurekebisha yale ambayo ni dhahiri hayako sawa.
Naomba nirejee nyuma kidogo, nimrudishe msomaji katika mihadhara aliyotoa Mwalimu Julius Nyerere katikati ya miaka ya 1990. Katika mmojawapo wa mihadhara hiyo Mwalimu, ambaye pasi na shaka alikuwa anaukosoa uongozi uliokuwa madarakani wakati huo, alieleza jinsi thamani ya diplomasia ya Tanzania ilivyokuwa imeporomoka.
Alimnukuu mama mmoja kutoka nchi moja jirani ambaye alitaka kujua kutoka kwa Mwalimu nini kilikuwa kimeisibu diplomasia ya Tanzania. Mama huyo, kwa mujibu wa Kambarage, akasema kwamba huko nyuma, katika vikao vya kimataifa, ilikuwa ikitangazwa kwamba ni zamu ya ujumbe wa Tanzania kutoa hotuba, watu waliokuwa wanavuta sigara wanazizima haraka waliwahi kusikiliza hotuba ya Tanzania, na wale waliokuwa wakinywa chai wanaacha chai na kurejea ukumbini.
Mama huyo akaendelea kuumueleza Mwalimu: ‘Siku hizi ikitangazwa kwamba Mtanzania anazungumza, ndipo wajumbe wa nchi nyingine wanaona ni fursa ya kutoka kwenda kuvuta sigara au kunywa chai!’ Sasa, mimi sina shaka kwamba kwa kusema maneno hayo na kwa kutoa mfano huo, Kambarage alikuwa anatamba kwa kuonyesha kwamba utawala wake ulikuwa unajua namna ya kuendesha diplomasia kuliko utawala uliokuja baada yake.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/misafara-mirefu-posho-kubwa-tija-kidogo#sthash.ntvqjdvE.dpuf

Makala
Rai ya Jenerali
Misafara mirefu, posho kubwa, tija kidogo
Jenerali Ulimwengu
Toleo la 331
25 Dec 2013
PASI na shaka, kwa msomaji aliyefuatilia vilivyo kwa wiki kadhaa sasa (naomba radhi kwa wiki mbili zilizopita) nitakuwa nimeeleweka kuwa ninachokisema katika mfululizo huu ni kwamba diplomasia yetu imeshindwa kutuletea matunda ambayo tungetaraji kuyavuna kama diplomasia yetu ingekuwa imefanya kazi ipasavyo. Pasi na shaka pia, haya ni maoni yangu binafsi ambayo Kiingereza yanaweza kuitwa ‘subjective’ kwa sababu hayana vigezo vya uyakinifu vya kuweza kuyathibitisha.
Hayawezi kuwa na ukweli kama ule uliomo ndani ya uzani wa kilo moja, au ratili moja, au sentimeta moja, au yadi moja.
Kwa sababu ya kukosa uyakinifu wa aina hiyo, mambo kama haya hujadiliwa kwa kuyatolea maelezo marefu ambayo aghalabu huhitaji kuambatanishwa na mifano mingi, na wala hilo halikomeshi malumbano.
Kwa kuwa ni maoni ambayo uyakinifu wake haupimiki yatabakia daima katika medani ya mabishano. Lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya watu wenye akili kuona zoezi la kutoa maoni, hata kama ni ‘subjective,’ kuwa ni kupoteza muda.
Maoni ‘subjective’ yanapogonganishwa na mawazo ‘subjective’ ya mtazamo tofauti yanaanza safari kuelekea mawazo ‘objective’ hata kama si lazima kila mara tufike  huko. Mara nyingi zaidi tunapata fursa na wasaa wa kurekebisha yale ambayo ni dhahiri hayako sawa.
Naomba nirejee nyuma kidogo, nimrudishe msomaji katika mihadhara aliyotoa Mwalimu Julius Nyerere katikati ya miaka ya 1990. Katika mmojawapo wa mihadhara hiyo Mwalimu, ambaye pasi na shaka alikuwa anaukosoa uongozi uliokuwa madarakani wakati huo, alieleza jinsi thamani ya diplomasia ya Tanzania ilivyokuwa imeporomoka.
Alimnukuu mama mmoja kutoka nchi moja jirani ambaye alitaka kujua kutoka kwa Mwalimu nini kilikuwa kimeisibu diplomasia ya Tanzania. Mama huyo, kwa mujibu wa Kambarage, akasema kwamba huko nyuma, katika vikao vya kimataifa, ilikuwa ikitangazwa kwamba ni zamu ya ujumbe wa Tanzania kutoa hotuba, watu waliokuwa wanavuta sigara wanazizima haraka waliwahi kusikiliza hotuba ya Tanzania, na wale waliokuwa wakinywa chai wanaacha chai na kurejea ukumbini.
Mama huyo akaendelea kuumueleza Mwalimu: ‘Siku hizi ikitangazwa kwamba Mtanzania anazungumza, ndipo wajumbe wa nchi nyingine wanaona ni fursa ya kutoka kwenda kuvuta sigara au kunywa chai!’ Sasa, mimi sina shaka kwamba kwa kusema maneno hayo na kwa kutoa mfano huo, Kambarage alikuwa anatamba kwa kuonyesha kwamba utawala wake ulikuwa unajua namna ya kuendesha diplomasia kuliko utawala uliokuja baada yake.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/misafara-mirefu-posho-kubwa-tija-kidogo#sthash.ntvqjdvE.dpuf

KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD

KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD