RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete amefanya ziara ya kikazi mkoani Ruvuma. Akiwa katika ziara hiyo ambayo imefanyika kwa siku saba kuanzia Julai 17 hadi 23, Rais KIKWETE amefanya mambo makubwa ya kimaendeleo ikiwemo kukagua, kuzindua, kufungua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Alhamisi, 24 Julai 2014
Jumanne, 22 Julai 2014
MASHINE ZA KUTOTOLEA VIFARANGA WA KUKU, KANGA,NA BATA
Full Technology And Function
- Digital temperature, humidity and turning frequency displaying.
- Automatic turning system tilting the eggs 45ยบ once per two hour (Setter Only). According your actual request, you can set turning interval time you need.
- Forced air circuit by 1 fan with automatic heating and humidifying system.
- The door is transparent, made of organic glass. You can observe the whole hatching process through the door.
- Inside light.
- Made of polyester, double color coated steel wall construction for a perfect insulation.
- Operates on 220 V, 380W (max power), 50HZ.
- Approx. weight and measures (packed in carton) 45Kg. 670 x 660x940mm
Supplying 3 setting trays and 1 hatching baskets, Setting capacity 210 chicken eggs and hatching capacity 88 eggs.
Range of temperature controlled: 35--39℃
Precision of temperature controlled: 0.1℃
Humidity precision display: 1%RH
Range of humidity controlled: 30-75%RH
Precision of humidity controlled: 2%RH
Angle of eggs-turning: 41-4
- Temperature precision display: 0.1℃ Setting time of eggs-turning: 0- 190 minutes.
FOR DETAIL PLEASE CALL 0767989713/0786989713/0715989713
Jumatano, 16 Julai 2014
MAISHA NI SAFARI NDEFU, HAKUNA KUKATA TAMAA, KUWA MVUMILIVU SONGA MBELE
Ni mwaka sasa toka nimemaliza shahada yangu ya kwanza ya Uchumi kilimo na Biashara. Shukrani kwa mama yangu Bi Swalati A. Ndimbo kwa jitihada zake kubwa kwangu kuhakikisha nasoma. Nakumbuka mama yangu alilazimika kuuza kuni wakati huo ili nipate hela ya madaftari. Namshukuru pia Mjomba 'angu Marehemu Balihua A. Ndimbo, kwa kunisomesha toka kidato cha kwanza hadi cha Sita na kunipa upendo wa hali ya juu. Msingi niliojengewa umekuwa Imara kuendeleza jengo ambalo kwa sasa, lilipofikia, limeanza kupendwa na hivyo kutumiwa na watu , naamini muda si mrefu jengo hilo litaimarika zaidi na kuwa zuri lenye mvuto maradufu . Pia nimshukuru Baba 'angu Mzee Titus F. Ng'oma kwa mchango wake kama Baba. Namshukuru Babu yangu mzee Mwenyekheri M. Ndimbo na Mkewa Bi Brenda M. Ndimbo kwa kupita mikononi mwao. Dr Gabagambi, mwalimu wangu wa somo la Utafiti pamoja na Dr. Mkandara mwalimu wangu mlezi wa taaluma, kwa pamoja nawashukuru sana kwa mchango wao kwangu. Mwisho nawashukuru Maschool mates wangu wote, nitamtaja mmoja moja kwa niaba kuonyesha shukrani zangu, Primary School, Athuman Kayumba, na Yasini Komba (Shule ya msingi Namtumbo na Shule ya Msingi Mgombasi), O- level (Minaki secondari), Shaibu Rajabu, A- level (Umbwe Secondari) Justin Sanya, Certificate in Animal health and Production, Shaibu Ndimbo na Emanuel Maimbi) chuo cha mifugo Madaba na Morogoro), Diploma in Animal Health(chuo cha mifugo Morogoro), Editha Matembe, Bsc. Agricultural Economics and Agribuiness (SUA), Makando Weight G Force (Sufian Makando), Na kwa upande wa kazini namshukuru Mkurugenzi wangu Bwana Johaness B. Kamonga, Mkurugenzi mtendaji wa Matembwe Village Co Ltd, Njombe, Dr. George J. Mkoma, Mkurugenzi wa Kampuni ya Hisa Micro finance and Community Development, Dr. Boniface Tibaijuka, Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma pamoja na Mama Daina Mnywanga Mkuu wa Idara ya Kilimo na Umwagiliaji Halimashauri ya wilaya ya Mvomero. Mwisho aliye juu ya wote ni allah aliyenijalia kufika hapa nilipofika. Alhamdulillah!
Allah Is Great
Alhamisi, 26 Juni 2014
NI LANDMARK HOTEL
Kumekuchaaa Dar es salaam. Ni tarehe 20/09/2014 ndani ya Landmark Hotel, ni semina ya aina yake kuwahi kufanyika. Nitakuwemo katika wale watakao toa mada siku hiyo. Ni fursa pekee kwa wale wanaofuga na wanaohitaji kuanza kufuga nk. Karibu tukutane tuonyeshane utajiri uliojificha katika ufugaji wa kuku, hakuna haja ya kulalamika. Anza sasa kufuga kuku unufaike Kiuchumi.
Ni semina ya aina yake kwasababu mambo mengi yatahusika siku hiyo kama ambavyo yamebainishwa kwenye hilo tangazo hapo juu.
Siyo siku ya kukosa siku hiyo. Ni fursa pekee kwa wafugaji na wadau wa kuku Dar es salaam na maeneo jirani.
Karibu nyote.
Jumatano, 18 Juni 2014
UFUGAJI WA KUKU NDIO MPANGO MZIMA, HARAKA UNATAJIRISHA
Vifaranga wakiwa bandani. Ndivyo inavyotakiwa waonekane wasiwe wamebanana au kujikusanya sehemu moja.
Hapa wamekuwa kidogo ni hatua kwa hatua.Hiki ndicho kiwanda cha kutengeneza chakula cha kuku.
Kazi inaendelea chakula kinatengenezwa na kuchanganywa vyema kiwandani.
Hapa afisa akiwa kazini anawajibiki. Ni Matembwe village company Ltd, Njombe
Kazi inaendelea hakuna kulala mpaka kuku wapate chakula.
Hapa vifaranga ndio kwanza wamezaliwa tayari kwa kuwafanyia sexing kuwatenganisha vidume na vijike ili wapelekewe wateja.
Vifaranga bora kabisa Kutoka Matembwe Njombe.
Sexing Inaendelea hapa. Sexing inayofanyika ni ile ya kutumia mabawa
Kazi ni kazi hakuna kulala. Sexing inaendelea.
Afisa akifanya Post mortem ya kuku aliyekufa masaa kama matano hivi toka aaze kuonyesha dalili ya ugonjwa , baada ya Post mortem alionekana ana msumali kwenye filigisi au gizzard
Hapa chakula kiko tayari kwa kusambazwa madukani kwa ajili ya kuuzwa na kingine kubakizwa tayari kwa kulishwa kuku wa Kampuni.
TANGAZO LA SEMINA YA WADAU WA TASNIA YA KUKU WA DAR-ES- SALAAM
Habarini wadau,
Still niko humu uwanjani.
Leo nina habari njema kwa waazi wa Dar es salaam. Kuna semina kabambe inaratibiwa soon nitawapa habari kamili. Mimi pia nitakuwa mjengoni katika wale watakao wasilisha maada siku hiyo. Kaani mkao wa kula ni semina ya siku moja kiingilio ni tsh 20000/=
Kama kweli wewe ni mfugaji ama unakusudia kuanza ufugaji basi tafadhali usikose siku hiyo. Ukikosa utakuwa umepitwa na mengi.
Wadau mbalimbali wa kuku watakuwepo siku hiyo, mabenki yanayotoa mikopo kwa wafugaji, wafugaji wakubwa wa kuku waliofanikiwa katika ufugaji wao watatoa ushuhuda siku hiyo, wanunuzi wa mazao ya kuku, watu wa mahoteli mbalimbali, supermarkets,nk madaktari na watu waliobobezi katika tasnia ya kuku nk. Watakuwepo pia wazalishaji wa vifaranga, watengenezaji wa vyakula mbalimbali vya kuku, watengenezaji wa Incubators wa ndani ya nchi na wawakilishi wa watengenezaji wa mashine za nje.
Kila kitu utakachohitaji kukifahamu siku hiyo utafahamu. Je wajua ukitaka kuanzisha hatchery hatua gani muhimu za kufuata, nini kinahitajika na wapi uanzie, siku hiyo ni siku muafaka.
Mambo yakikaa sawa tutawajulisha,lini na ukumbi gani semina hiyo itafanyika. Kwa wale watakaohitaji basi tuwasiliane kupitia namba zangu 0767989713, 0715989713 na 0786989713
Kwa pamoja tunaweza kuutokomeza umasikini.
Jumatatu, 9 Juni 2014
UZALENDO NA NIDHAMU KATIKA MATUMIZI YA RASILIMALI ZA UMMA
Kwanini Tanzania masikini. Mimi nadhani viongozi wetu tuliowachagua hawawajibiki vyakutosha kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu. Wanapenda kuishi maisha ya anasa kana kwamba Tanzania na Watanzania ni Matajiri.
Wanasiasa pia wanalifilisi taifa hili. Ebu fikiria kuna ulazima gani wa mbunge mmoja kulipwa tsh 300000/= kwa siku ili hali nchi yetu ni masikini. Kuna ulazima gani wa kununua magari ya kifahari ya shilingi milioni 200 ili hali watanzania wezetu wanakufa kwa njaa, wanafunzi hawana madawati ya kukalia, walimu wanalalamika maslahi madogo, madaktari nao pia.
Wanasiasa pia wanalifilisi taifa hili. Ebu fikiria kuna ulazima gani wa mbunge mmoja kulipwa tsh 300000/= kwa siku ili hali nchi yetu ni masikini. Kuna ulazima gani wa kununua magari ya kifahari ya shilingi milioni 200 ili hali watanzania wezetu wanakufa kwa njaa, wanafunzi hawana madawati ya kukalia, walimu wanalalamika maslahi madogo, madaktari nao pia.
Ningekuwa Rais ningeagiza viongozi wote wa serikali watumie tax gari zinazoendana na uwezo wetu. Wabunge wa bunge la katiba na bunge la bajeti ningewalipa tsh elfu 85 tu kwa siku kama wafanyakazi wengine wanapoenda kufanya kazi nje ya mkoa wake.
Ili tuendelee lazima tukubali kuishi kwa ubahiri na mikati mikubwa ya kuhakikisha kuwa Tanzania na Watanzania tunawakomboa kutoka kwenye lindi la umasikini.
Tujenge miundo mbinu itakayo rahisisha kuchumi wetu upae.
Hakuna faida ya kwenda kuficha nje mabilioni ya pesa ili hali watanzania wenzako wanakufa njaa hapa nchini kwako.
Tujifunze kuhurumiana. Kwa pamoja tunaweza kutokomeza lindi la umaskini katika nchi yetu
Ili tuendelee lazima tukubali kuishi kwa ubahiri na mikati mikubwa ya kuhakikisha kuwa Tanzania na Watanzania tunawakomboa kutoka kwenye lindi la umasikini.
Tujenge miundo mbinu itakayo rahisisha kuchumi wetu upae.
Hakuna faida ya kwenda kuficha nje mabilioni ya pesa ili hali watanzania wenzako wanakufa njaa hapa nchini kwako.
Tujifunze kuhurumiana. Kwa pamoja tunaweza kutokomeza lindi la umaskini katika nchi yetu
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD
KARIBU KWENYE BLOG YETU YA KINASORU EAST AFRICA TANZANIA LTD














